Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge
- Get link
- X
- Other Apps
Dar es Salaam. Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye
Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi
na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa
kulidanganya Bunge.
Hatua
hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya
mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012.Kamati
hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha
Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu
lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project)
hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.“Ni
vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na
zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa kiasi
cha Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia
Sh252.975bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika
visivyo,” alisema Zitto, ambaye pia ni Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini
(Chadema).Alisema
katika majumuisho ya Bajeti ya wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Mwakyembe
wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Lukuvi walitoa maelezo
yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha.
Alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.
“Tunaomba
fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara,”
Zitto alisema akikariri maneno ya Dk Magufuli wakati anawasilisha
bajeti.
“Fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili,” haya yalikuwa maneno ya Dk Mwakyembe wakati akifanya majumuisho.
“Hizi ni fedha kwa ajili ya counterpart fund,” alimkariri Lukuvi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.
Zitto
alisema CAG alihoji mwaka huu kuhusu matumizi ya fedha hizo na alitoa
taarifa akidai kuwa fedha hizo zilikuwa miradi hewa na kasma kivuli.
Zitto alisema kuwa Dk Magufuli na Katibu Mkuu wake walipohojiwa walidai kutumia fedha hizo kulipa madeni.
“Kwa nini
mlidanganya Bunge? Mliomba fedha za kuanza miradi maalumu. Hamkuomba
fedha za madeni. Kwa nini mliunda kasma kivuli na kuifuta baada ya pesa
kulipwa?” Zitto alimhoji Balozi Mrango.
Katika
majibu yake, Balozi Mrango alisema kwa nia njema, fedha hizo zilitumika
kuwalipa makandarasi waliokuwa wamechachamaa, huku baadhi yao
wakisisitiza kusitisha kuendelea na miradi. Hivyo wakalazimika kuomba
fedha kwa njia hiyo ili miradi kuendelea katika maeneo mbalimbali ya
nchi.
Zitto
hakuridhishwa na majibu hayo akisema hapakuwa na haja ya kutumia fedha
hizo kuwalipa makandarasi wakati kulikuwa na kasma yao ya awali. Alisema
kama kulikuwa na haja hiyo, wizara isingeita mradi rasmi.
“Jambo
hili siyo sahihi hata kidogo kulidanganya Bunge na hadi sasa wewe na
waziri wako hamuonyeshi kukubali kosa hili, hata Waziri Lukuvi naye
alisisitiza bungeni kwamba fedha hizo zinaombwa ili kutekeleza mradi
maalumu lakini sasa imebainika sivyo, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge
tutawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ili wahojiwe nao wajieleze kwa
kulidanganya,” alisema Zitto.
Pia
kamati hiyo imeitaka wizara hiyo kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu matumizi
ya Sh100 bilioni zilizotumika kinyume na maombi yaliyowasilishwa kwenye
Bajeti ya mwaka huo wa fedha.
CAG
ameshauri madeni yote ambayo Wizara ya Ujenzi inadaiwa yaorodheshwe ili
yawe wazi kuepuka migongano katika matumizi ya fedha.
Alipoulizwa
kuhusu madai hayo, Lukuvi alisema haelewi chochote na kusisitiza kuwa
akipata taarifa rasmi za Kamati ya PAC, atatoa ufafanuzi.
Halmashauri zinavyotafuna mabilioni
Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAACc), imeeleza namna
mamilioni ya fedha za Serikali zinavyoibwa kutoka Hazina kupitia
halmashauri za wilaya huku Ilala ikitajwa kuongoza kwa ufisadi huo.
Mwenyekiti
wa LAAC, Rajab Mbarouk Mohammed aliwaambia waandishi wa habari jana
kwamba Hazina imekuwa ikipeleka fedha kwenye halmashauri zikiwa zimezidi
na kwamba kiasi kinachozidi hakirudishwi badala yake huliwa.
Alisema
kamati hiyo imefanya uchunguzi kwenye halmashauri 43 na kubaini kwamba
mtindo huo ndiyo unaotumika kuiba fedha za Serikali.
“Mwaka
2011/12 kiasi cha Sh1.5 bilioni zilipelekwa zikiwa zimezidi kwenye
halmashauri hizo lakini hazikurudishwa Hazina kama inavyoonyesha kwenye
ripoti ya CAG.
Alisema
kati ya kiasi hicho, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilipewa ziada ya
Sh213 milioni ikifuatiwa na Geita iliyopewa Sh129 milioni.
“Fedha
hizo za mishahara zilipelekwa kwenye halmashauri hizo na Hazina kimakosa
zikiwa zimezidi lakini watendaji wa hawakuzirudisha kama wanavyotakiwa
kisheria badala yake zikayeyuka,” alisema.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa uchunguzi huo pia ulibaini kwamba katika halmashauri
hizo 43 kiasi cha Sh693 milioni hulipwa mishahara hewa ambayo
wafanyakazi wake walishakufa na wengine kustaafu.
Alisema
Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ililipa mishahara hewa yenye thamani
ya Sh79.4 milioni ikifuatiwa na Ukerewe iliyolipa Sh57.5 milioni.
Kwa
upande wa fedha za miradi ya maendeleo, mwaka 2011/12, Hazina ilipeleka
katika Halmashauri ya Mbarali, Mbeya Sh724 milioni kwa ajili ya Mradi wa
Maendeleo ya Elimu Sekondari wakati mradi huo ulikuwa ukihitaji Sh70
milioni tu.
“Kiasi
cha Sh654 milioni zilipelekwa kimakosa na Hazina lakini badala ya
kurudishwa zilitumiwa katika mazingira ya kutatanisha,” alisema.
Alisema
Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ilipelekewa ziada ya Sh500 milioni na
Mvomero ilipewa Sh85 milioni. “Kuna mtandao mkubwa wa Hazina na
halmashauri ambao ukiachwa utaendelea kupoteza fedha nyingi za
walipakodi,” alisema.
Mwananchi
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment