Posts

RAIS KIKWETE AZIONYA NCHI CHOKOZI DHIDI YA ARDHI YA TANZANIA

Image
RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali ya Tanzania iko tayari kukabiliana na mtu yeyote atakayejaribu kuichezea au kuichokoza kwa namna yoyote ile, ikiwamo kumega ardhi yake, itamfundisha kama ilivyomfundisha aliyekuwa Rais wa Uganda, Idd Amin Dada, katika Vita ya Kagera.  Kikwete alisema serikali ilimshikisha adabu Amin alipojaribu kumega sehemu ya ardhi ya Tanzania, hivyo haitosita kufanya hivyo tena kwa asiye na nia njema na Tanzania. Kiongozi huyo mkuu wa nchi alitoa onyo hilo jana wakati akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliyofanyika kitaifa katika makaburi yaliyopo Kambi ya Kaboya, wilayani Muleba, mkoani Kagera. Rais Kikwete alisema serikali iko tayari kukabiliana na kupambana kwa nguvu yoyote ile bila kuogopa mtu anayejaribu kuichezea nchi ya Tanzania kwa lengo la kukwaza amani na utulivu uliopo hivi sasa. “Laleni usingizi salama. Msisikilize maneno ya mitaani, kwa sababu jeshi letu liko

HII NDO HALI HALISI YA MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTER ALIYEMWAGIWA TINDIKALI

Image
MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.  Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.  Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki. Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.  Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.  Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mko

MKE ALIYETAKA KUMUUWA MUME NA MTOTO KWA AJILI YA MALI AFIKISHWA MAHAKAMANI ARUSHA

Image
Janeth Jackson anayedaiwa kula njama za kumuua mume wake, Simon Jakson na mtoto wake wa kambo.  Ni mke wa mfanyabiashara maarufu wa Tanzanite Arusha, anayedaiwa kupanga njama za kumuua mumewe na mtoto wa kambo wa kiume anayeishi Bukoba. Arusha. Mwanamke anayedaiwa kupanga njama za kumuua mumewe wa ndoa na mtoto wa mume huyo, amepandishwa mahakamani akiwa na mtuhumiwa mwingine wa mauaji hayo. Janeth Jackson (32), mkazi wa Moshono, Arusha na Novatus Elias, walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha /Arumeru, Devotha Kamuzora, wakisomewa makosa mawili ya kula njama ya kutaka kumuua Simon Jackson ambaye ndiye mume wa Janeth. Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Edna Kasala, alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa wote walitenda kosa la pili la kula njama na kutaka kumuua Desderi Sabas, ambaye ni mtoto wa mke mwingine kwa mume huyo anayeishi Bukoba, mkoani Kagera. Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu

MIRUNGI KILO 50 YAKAMATWA ARUSHA

Image
Dawa za Kulevya aina za Mirungi yenye uzito wa Kilo 50 imekamatwa Jijini Arusha baada ya kutelekezwa kwenye gari na watu wasiofahamika. Duru za Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kwa Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo ACP Liberatus Sabas zimesema Polisi walipokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema Julai 24 mwaka huu majira ya saa 6 za mchana maeneo ya Unga Limited Jijini Arusha kuwepo kwa gari linalosambaza dawa za kulevya zilizopigwa marufu nchini aina ya mirungi. Sabas amelitaja gari lililokamatwa baada ya dereva na waliokuwemo kulitelekeza  na kukimbia kusikojulikana kuwa ni Nissan Wingroad lenye namba za usajili T. 904 BSJ. Hata hivyo ACP Sabas ametoa wito kwa wananchi kupitia Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kuendelea kutoa ushirikiano pindi matukio ya dawa za kulevya yanapojitokeza katika jamii ili kutokomeza mtandao huo.

MWINYI KAZIMOTO AONEKANA MITAA YA DSM,AKANA KWENDA QATAR

Image
Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto ameonekana katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam na kuzua taharuki. Kazimoto alitoroka katika kambi ya timu ya taifa na kuelezwa kuwa alikimbilia Qatar kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa. Lakini kuna taarifa, Kazimoto amemueleza rafiki yake wa karibu kwamba hakwenda Qatar na badala yake alijichimbia jijini Dar, kimyaa. “Anasema kuna mtu alimkasirisha sana katika timu ya taifa, akaamua kujiondoa na kukaa pembeni. “Mwinyi si mtu wa maneno mengi, hivyo aliamua kukaa kimya tu kuacha watu waseme wanachotaka,” alisema rafiki yake huyo na kuongeza. “Ndani ya siku chache huenda akajiunga na kambi ya Simba iliyoko Bamba kama hakutakuwa na tatizo.” Tayari TFF imeishatangaza kuwa itamchukulia hatua kutokana na kitendo cha kutoroka kambini na kulazimisha Kocha Kime Poulsen kumuita kinda, Mudathir Yahya

JK yeyote ambaye atajaribu kuchezea mipaka ya Tanzania atakiona cha mtema kuni.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa yeyote ambaye atajaribu kuchezea usalama na mipaka ya Tanzania atakiona cha mtema kuni.   Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liko imara tayari kulinda mipaka ya Tanzania wakati wowote na saa yoyote. Rais Kikwete ametoa ujumbe huo mzito leo, Alhamisi, Julai 25, 2013, wakati alipozungumza na wananchi wakati Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye Kambi la JWTZ ya Kaboya, Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera. Mara baada ya kushuhudia sherehe za kumbukumbu hizo ambako miongoni mwa mambo mengine ametembelea makaburi ya askari wa Tanzania waliopoteza maisha yao wakati wa kuikomboa nchi kutokana na uvamizi wa Idi Amin wa Uganda na kuona silaha zilizotumika katika vita hivyo vya 1978/79, Rais Kikwete amewaambia mamia kwa mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe hizo: “Laleni usingizi sal

MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA YAFANA MBEYA

Image
Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro mwenye suti ya bluu ambaye pia ni mwenyekiti wa wakuu wa wilaya za mkoa Mbeya ndiye aliongoza maadhimisho hayo akimwakilisha mkuu wa mkoa Abbas Kandoro kulia kwake mkuu wa wilaya ya Mbeya Norman Sigalla  Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akiweka mkuki na ngao kuwakumbuka mashujaa waliokufa vitani Mwakilishi wa mstahiki meya wa jiji la mbeya akiweka shada lake Mzee Ernest Waya akiweka upinde na mshale kuwakumbuka wenzake aliokuanao vitani enzi hizo... Chifu Lyoto alikuwepo kuweka mshda kuwakumbuka mashujaa Viongozi mbali mbali wa dini waliwaombea duwa mashujaa wetu Mzee Ernest Paulo Waya aliyepigana vita kuu ya pili vya Dunia alikuwepo kuwakumbuka wenzake Picha na Mbeya yetu

RAIS KIKWETE AFUNGUA JENGO LA MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akikata utepe akisaidiwa na  Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman wakifungua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 NA FULLSHANGWE Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika ufunguzi huo wakiondoka baada ya uzinduzi huo Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa baada ya kufungua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa baada ya kufungua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa mahakama nchini mara  baada ya kufungua  rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondioka baada ya kufungua  rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013

MABINTI WAJIREKODI WAKIWA UCHI..... VIDEO YAVUJA

Image
Maadili ya kitanzania yamekuwa yakiporomoka  kila  kukicha  hasa kwa  watoto wa kike  ambao  wengi wao wamekuwa wakiendekeza  ufaska  wa   tamaduni  za  nchi  za  ng'ambo  wa  kujirekodi  wakiwa  uchi  na  kujipiga  wakiwa  uchi. Hii  ni  video  ya  mabinti  hao   walioamua  kujiumbua  wenyewe( Ni sharti uwe mtu mzima ) << BOFYA  HAPA  KUICHEIKI  ILIKO>>

PESA MWANAHARAMU:.. LADY GAGA AKUBALI KUPIGWA UCHI ILI KUUPAMBA UKURASA WA MBELE WA GAZETI

Image
  Lady  Gaga  ametoa  kali  ya  mwaka  baada  ya  kukubali  kufotolewa  akiwa  mtupu  ili  kuupamba  ukurasa  wa  mbele  wa  gazeti  la  V magazine... Baadhi  ya  fans  wake  wamefunguka  na  kudai  kuwa  uroho  wa  pesa  utamponza  huku wengine wakidai   kuwa  msanii  huyo  atakuwa  amekubali  kuanikwa  hivyo  ili  kuvuta  "attention"  ya  mashabiki  wake  kwa  ujio  wa  albam yake  mpya  itakayoitwa  Artpop Albamu hiyo inatarajiwa kuwa   sokoni mwezi wa 11 na nyimbo ya kwanza kutoka kwenye  album   hiyo  itatambulishwa mwezi wa nane tarehe 19.

KWA WADADA AMBAO HAWAJA OLEWA NA WANAPENDA MAISHA YA NDOA

Image

UJUMBE MZITO KUTOKA KWA IRENE UWOYA KWENDA KWA JOHARI

Image
Katika pita pita zetu leo hii tuliweza kupata ujumbe mmoja mzito na wa kutia moyo toka kwa mwanadada Irene Uwoya aliomwandikia mkongwe wa bongo movies nchini kwa upande wa kinadada Blandina Chagula maarufu kama Johari wiki chache zilizopita. Ujumbe huu wa Irene ni ujumbe wa kutia moyo na unaweza kuwa kama “Motivation message” kwa wadada wengi hapa mjini ili badala ya kukaa na kuwaza kupata mali au mafanikio kwa njia za mkato au zisizo halali basi wafanye kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi. Tukinukuu ujumbe huo Irene kwa Johari aliandika…. “Wewe nimwanamke wapekee...mchapakaz sana...atawaongeee vp kaza moyo...one thng u hav to know if God say yes no body I mean no body can say no...so don gv r f*ck Hii inawahusu wadada wote jamani. Nyie ni wanawake wapekee, wachapakazi, kazeni moyo. If God say yes, nobody can say no (Mungu akisema ndio hakuna awezaye kusema hapana)

Huyu ndo Mtu Ambaye Hajaoga Wala Kukata Nywele kwa Zaidi ya Miaka 37

Image
Mr Singh na Mkewe Hakika haya tunaweza kuyaita mafanikio ya ajabu kwa mzee huyu kutokana maamuzi yake. Labda tumite Mr Adui wa Maji ila jina lake kamili ni Mr Kailash Singh akiwa na ndiye anayeshikilia rekodi ya mtu anayenuka zaidi kutokana na kutokuoga kwa zaidi ya miaka 37 sasa. Mr Singh, 65, hajaoga na hata kukata nywele zake zenye urefu wa futi 6 toka mwaka 1974, mda mfupi mara baada ya kutoka kuoa. Akielezea juu ya uamuzi wake wakushangaza, Mr Singh anasema mchungaji alimuahidi zawadi ya mtoto wa kiume kama atafata ushauri.  Licha ya majirani kuwa wanamtania na kumdhihaki jamaa huyo walishindwa kubadili maamuzi yake na namna ya kipekee alifanikiwa kumshawishi mke wake, ila cha ajabu zaidi ni pale ambapo imani yake imeonekana kumdanganya kwani ameishia kupata watoto saba ambao wote ni wa kike.

DIWANI CHAMBO WA CCM AMTWANGA MKEWE............................

Image
Mke wa Diwani, Imelda Chambo akiwa kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Kwa mujibu wa mashuhuda, ugomvi huo ulichukua nafasi Alhamisi iliyopita saa 6 usiku nyumbani kwa wanandoa hao, Kihonda. Mke naye ni Diwani wa Kata ya Mkundi kwa ‘leseni’ ya CCM. Inadaiwa kuwa, baada ya mheshimiwa diwani kumtwanga mkewe na kummwagisha damu, mke naye alichukua chupa ya bia na ‘kujirudishia’’, wote wakawa chapachapa kwa damu. Siku ya tukio, paparazi wetu alipofika nyumbani kwa wanandoa hao alikuta tayari wameshakimbizwa hospitalini ndipo alielezwa kuwa chanzo cha ugomvi wao ni wivu wa mapenzi.  Paparazi wetu alitinga hospitali ya mkoa na kumkuta mke wa diwani huyo akiwa hoi kwenye wadi namba tatu. na GPL Akizungumza kwa tabu na gazeti hili, Diwani Imelda alisema ndoa yao imedumu kwa miaka 30 na kubahatika kuzaa watoto watatu. “Naweza kusema nusu ya maisha yetu ya ndoa ni migogoro na mapigano. “Ugomvi wa leo hauna kichwa

WEMA SEPETU HATIMAYE AVUTAMKOKOMPYA.

Image
Hiindiogari mpya wema kama inavyoonekana katika picha   Haya ndio Maneno ya Martin Kadinda aliyoandika facebook na kuweka picha ya Wema akiwa na gari hilo "samahani kwa ubora wa picha kuwa hafifu....... Ila huyu dada anapenda pink kupitiliza..... haya she gat new pink Car.... mkutane barabarani..." aliandika Martin.

BAADA YA KUPIGWA CHINI BIG BROTHER, HUDDAH AAMUA KUMALIZA HASIRA ZAKE KWA KUJIPIGA UCHI

Image
Wengi waliamini  kwamba    Big Brother  imempa  fundisho  mrembo  huyu  na  kutegemea  mabadiliko   makubwa  ikiwa  ni  pamoja  na  kuuuheshimu  mwili  wake  baada  ya  Video  zake  za  uchi  kuvuja  akioga  bafuni... Hali  imekuwa  ni  tofauti  kwa  mrembo  huyu  asiyeijua  thamani  ya  mwili  wake.Tabia  ni  ngozi.Skendo,picha  za  uchi  huenda  ziko  katika  mishipa  ya  damu  yake.... Hizi  ni  picha  zake  za  nusu  uchi  alizotupia  mtandaoni.  

Msafara wa Baba Mtakatifu Francis 1 wapotea njia nchini Brazil ukitokea uwanja wa ndege.

Image
  Maelfu ya wananchi wa Brazil katika mitaa ya Rio de Janeiro wameivamia na kulizunguka gari lilokuwa limembeba  Baba Mtakatifu Francis 1 wakati msafara wake ulipopotea njia ulipokuwa ukitokea uwanja wa ndege alipowasili nchini humo kwa ziara. Katibu wa Usafiri wa Rio Carlos Osorio amesema gari aina ya Fiat alilokuwemo Baba Mtakatifu lilikuwa likitokea uwanja wa ndege kuelekea katikati ya mji, lilipita njia tofauti lilipofika katika mgawanyiko wa barabara 12 unaofahamika kama Avenida Presidente Vargas. Badala ya kupita njia za upande wa kushoto za mgawanyiko huo ambako hakukuwa na msongamano wa magari, gari hilo lilipita njia za upande wa kulia ambako kuna magari mengi yakiwemo mabasi na teksi nyingi, hatua iliyosababisha gari hilo kusimama. Maelfu ya watu waliokuwa wamejipanga mitaani walilikimbilia gari hilo na kufika katika dirisha la upande alipokaa , huku wengi wao wakimpiga picha. Msemaji wa Vatican Padri Federico Lombardi amet

Bomu lanaswa ziara ya Papa Francis nchini Brazil

Image
  Mbali ya kufurahia mapokezi makubwa nchini Brazil, ziara ya Papa Francis imeingia doa baada ya bomu kugunduliwa chooni katika mji ambao atauzuru leo. Bomu hilo la kutengenezwa kienyeji liligunduliwa na maofisa usalama likiwa katika choo katika Kanisa la Bikira Maria wa Aparecida katika mji huo mdogo ambao kiongozi huyo atautembelea kama sehemu ya ziara yake kwa kwanza nje ya Vatican. “Lilikuwa bomu la kutengenezwa kienyeji lenye uwezekano mdogo wa kusababisha maafa,” imeeleza taarifa ya Jeshi la Anga la Brazil. “Ni tukio linaloshtua, limefanyiwa kazi na wana usalama ambao wamejiandaa vyema kwa ziara hii. Kwa hakika haliwezi kuzua hofu, vikosi vya usalama vimejiandaa kikamilifu kwa matukio kama haya.” Kulingana na vyombo hivyo, bomu hilo liliteguliwa na kisha kuharibiwa baada ya kugundulika kwake katika mji huo mdogo kwenye viunga vya Rio de Janeiro baada ya mazoezi ya vikosi vya usalama, limeeleza gazeti la Grupo Estado. Bikira Maria wa Aparecid