HAIJAWAHI KUTOKEA: Kim Jong-un Avuka Mpaka wa Kijeshi, Aingia Korea Kusini
KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa kuvuka mstari wa kijeshi uliowekwa kuyagawa mataifa ya Korea tangu vita vya Korea vya mwaka 1950-1953, ambapo ameingia Korea Kusini na kukutana na Rais wa nchi hiyo, ambaye amekuwa hasimu wake kwa muda mrefu, Moon Jae-in. , Tukio hilo la kihistoria limetokea leo Aprili 27, 2018 ambapo tukio hilo lilishangiliwa kwa mbwembwe na viongozi wa Korea Kusini na mwenzao wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa kushikana mikono katika mpaka huo kabla ya kukaribishwa na kuingia nchini humo. Hata hivyo shughuli zote za taifa la Korea Kusini zilisimama kwa muda ambapo viongozi hao wawili walisalimiana kwa mikono katikati ya mpaka wa mataifa hayo mawili na baadaye watu walishangaa baada ya Kim kumualika kiongozi wa Korea Kaskazini kuvuka kwa muda mfupi katika mstari wa mpaka wa mataifa hayo mawili kuingia Korea Kaskazini, kabla ya wawili hao kurudi tena Korea Kusini muda wote huo wakiwa wameshi