Posts

MWENYEKITI UVCCM APOKELEWA KWA KISHINDO DAR

Image
Mwenyekiti mpya Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),Kheri James akizungumza nawaandishi wa habari ukumbi wa Vijana Kinondoni, Dar es Salaam Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Kilakala (kushoto) akiteta jambo na Kheri James. Baadhi ya vijana wa UVCCM waliohudhuria katika hafla hiyo. MWENYEKITI mpya Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amepokelewa kwa kishindo na vijana wa UVCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akitokea mkoani Dodoma. Hafla hiyo imefanyika jana katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kheri alichaguliwa rasmi kuwa mwenyekiti Desemba 13 mwaka huu katika uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma na kuibuka mshindi kwa kupata kura 319. Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo, Kheri alisema ni wakati wa vijana wa jumuiya hiyo kuwa ngangari katika kupambana na rushwa inayoharibu taswira ya nchi kwani rushwa haijengi bali itawafanya vijana kuwa wasindikizaji tu kati

Zitto Akutana na Kufanya Mazungumzo na Mbowe

Image
Zitto na Mbowe. Katika kikao chake cha juzi, ambacho kiliamua kugomea ushiriki wa uchaguzi wa marudio, Kamati Kuu ya ACT Wazalendo iliuagiza Uongozi wa Taifa wa Chama kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini na kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini kwetu, kwa kuanzisha mazungumzo na vyama vyote vya Upinzani nchini ili kuona njia bora zaidi ya mapambano ya pamoja ya kukabiliana na vitendo vya chama tawala cha kuvuruga chaguzi huru na za haki nchini. Wakati Katibu Mkuu wa chama chetu, ndugu Dorothy Semu, anaendelea na utaratibu rasmi wa kulitekeleza hilo, nilipewa wajibu wa kuanzisha mazungumzo ya Viongozi wa Juu wa vyama hivyo. Jana, nimezungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, ndugu James Mbatia aliye hospitalini KCMC baada ya ajali (namuomba Mola ampe afya njema), pamoja na kukutana na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, ndugu Freeman Mbowe. Nafurahi kwamba mazungumzo yetu yameanza vizuri.

Fanya Haya, Hisia Za Mapenzi Ziendelee!

Image
TUNAISHI kwenye ulimwengu unaoenda kasi sana kiasi kwamba usipokuwa makini, unaweza kujikuta ukimpoteza mtu uliyempenda sana maishani kwa sababu tu ya kujua namna ya kwenda naye sawa wakati ukiendelea na mchakamchaka wa kukimbizana na maisha! Inafahamika kwamba mapenzi ni hisia lakini ni wachache wanaoweza kueleza jinsi ya kufanya hisia za mapenzi ziendelee kuwa hai. Siku hizi ndoa nyingi zinaendelea kuwepo kwa sababu ya kudra tu, unakuta mume na mke wanaishi kwa sababu ya mazoea tu lakini si kwa sababu ya mapenzi! Wengine wanakwambia kabisa, ‘mapenzi yalikuwa wakati tunaanzana’! Wanaishi tu ilimradi siku zinaenda, ilimradi wanawalea watoto lakini si kwa sababu ya upendo kati yao. Wengine wanafikia hatua hata ya kulala mzungu wa nne au kutengana vyumba kabisa! Kwa nje mnawaona kama wanapendana lakini kumbe ndani kuna ufa mkubwa kati yao, hakuna tena mapenzi kati yao. Cha ajabu, utakuta watu hawahawa ambao leo wanaishi kimazoea, wakati wanaanzana walikuwa w

Mo Rasmi Aanza Kumwaga Fedha Simba.

Image
Mohammed Dewji ‘Mo’ MFANYABIASHARA maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameanza rasmi kazi ya kuihudumia Klabu ya Simba. Mo ameanza kuihudumia klabu hiyo baada ya kupita kwenye mchakato wa kumtafuta muwekezaji wa Klabu ya Simba kwa ofa yake ya shilingi bilioni 20 na kupata hisa kwa asil­imia 50 huku 50 zikibaki kwa wanachama. Hata hivyo, bado kuna majadiliano na serikali ambayo inataka mwekezaji wa klabu asizidi asilimia 49. Wachezaji wa timu ya Simba. Awali, mfanyabiashara huyo alikuwa anaihudumia timu hiyo kama mwanachama kabla ya kukabidhiwa na wanachama klabu hiyo na kuwa mwekezaji. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka ndani ya timu hiyo, mfanyabiashara huyo ameanza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo mshahara, posho na mahitaji mengine. Mtoa taarifa huyo alisema, kambi ya maan­dalizi ya mechi ya hatua ya pili ya Kombe la FA dhidi ya Green Warriors aliwezesha yeye kwa kuiweka timu ya Escape Two Hotel, Mbezi Beach jijini Dar

TUNDU LISSU: BADO NINA RISASI MOJA MWILINI

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema mwili wake bado una risasi moja licha ya kutolewa nyingine 15, huku akiweka bayana kuwa kitu anachokikosa zaidi ni kazi yake ya ubunge. Mwanasheria mkuu huyo wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari mara baada ya kufika nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, pia aligusia faraja aliyoipata baada ya kutembelewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi tangu Septemba 7 na ambaye huenda akahamishiwa nje ya bara la Afrika kwa matibabu zaidi, ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Azam, Baruan Muhuza. “Hali yangu ya afya inaendelea vizuri bado nipo hospitali maana yake bado ni mgonjwa lakini niwaeleze Watanzania na wananchi wote wanaofuatilia afya yangu kwamba naendelea vizuri sana,” alisema na kuongeza, “Hivi tunavyozungumza sina jeraha la risasi, risasi 16 zil

TAZAMA PICHA ZA KWENYE USIKU WA WA ZARI ALL WHITE PARTY UGANDA.

Image
  Zari All White Party ni moja kati ya show zinazofanya vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na watu wanaohudhuria show hizo kuwa nadhifu zaidi. Usiku wa kuamkia Ijumaa hii moja ya show hizo ambazo huandaliwa na Zari The Bosslady, imefanyika katika ukumbi wa Guvnor nchini Uganda. Japo Zari alikutana na upinzani mkali kutoka kwa hasimu wake Hamisa Mobetto ambaye na yeye alikuwa na show yake kwa upande wa pili lakini hilo halikuweza kuzuia watu kumiminika katika party hiyo ambapo DJ wa Diamond, Romy Jones alihudhuria pia.

Kigwangalla Awakutanisha Wema na Jokate

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla jana Desemba 21, 2017 aliteua majina mengine ya Kamati ya Kitaifa ya kuandaa mwezi maalum wa maadhimisho ya Urithi wa Tanzania. Miongoni mwa wajumbe walioteuliwa ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jokate Mwegelo na Wema Sepetu ambao wataungana na wajumbe 23 aliowateua awali kuunda Kamati ya Kitaifa ya Kuandaa Mwezi Maalumu wa Maadhimisho ya Urithi wa Tanzania.  

FIFA YATANGAZA MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018

Image
FIFA limetangaza makundi ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwakani nchini Urusi. Makundi ya Kombe la Dunia 2018 Katika makundi hayo makundi yanayoonekana hatari zaidi ni Kundi C ambako kuna Ufaransa, Australia, Peru na Denmark na Kundi F linaloundwa na Ujerumani, Mexico, Sweden na Jamhuri ya watu Korea. Mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo utafanyika kati ya Mwenyeji, Urusi dhidi ya Saudi Arabia tarehe 24 juni 2018 kunako dimba la Luzhniki.

WEMA SEPETU ATANGAZA RASMI KURUDI CCM

Image
  Wema Sepetu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. MSANII maarufu wa Bongo Movie, Wema Sepetu leo Ijumaa, Desemba 1, 2017 ametangaza rasmi kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai kuwa ni kukosa amani ndani ya chama hicho. Wema ambaye ni alikuwa mshindi namba moja wa Taji la Miss Tanzania 2006, amesema Chadema ni kama nyumba inayomkosesha amani hivyo hana haja ya kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo.Amesisitiza kwake amani ni jambo kubwa sana hivyo anandoka ndani ya Chadema na kurejea nyumbani alikokulia kwa maana ya CCM. Wema na mama yake mzazi, Mariam Sepetu walihamia Chadema mwezi Februari mwaka huu baada ya kuhusishwa kwenye sakata la biashara ya madawa ya kulevya ambapo mpaka sasa kesi yake bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Vurugu Zatanda Kenyatta Akiapishwa, Polisi Wafunga Mtaa Kuzuia Mkutano wa NASA

Image
Polisi wakiimarisha ulinzi eneo hilo. MTAA wa Jacaranda jijini Nairobi, Kenya, leo umefungwa na polisi ili kuzuia mkutano wa umoja wa vyama vya upinzani nchini humo, National Super Alliance (NASA) uliopangwa kwa ajili ya kuwakumbuka wafuasi wake 27 waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa marudio uliofanyika zaidi ya wiki moja iliyopita. Mataili yakiwa yamechomwa moto. Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo ambapo Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa kwa kipindi cha pili katika uwanja wa michezo wa Kasarani. Chumba vya kutunzia maiti katika jiji hilo pia kimefungwa na polisi ambapo watu hawatakiwi kufika hapo. Hali ilivyokuwa eneo la tukio. Polisi waliokuwa na zana zote za kuzuia fujo wamekuwa wakirusha mabomu ya machozi sehemu nyingi yakiwemo maeneo ya wafuasi wa NASA ambao wamefunga barabara kadhaa jijini humo. Wafuasi wa NASA wakipambana na polisi. Mpinzani mkuu nchini humo, Raila Odinga, amepinga mipango ya kumwapisha katika nafasi ya urais, a

DIAMOND PLATINUMZ AIBUA MAPYA,AWASHA MOTO UPYA,WEMA SEPETU,ZARI THE BOSS LADY NA HAMISA KUMEKUCHA KUPITIA WIMBO WAKE MPYA- "SIKOMI"

Image
Wakati msanii wa muziki wa Bongo Flava, Diamond Platnumz ameachia ngoma mbili kwa wakati moja ambazo ni Sikomi na Niache, ngoma ya kwanza imekuwa na nguvu na mapokeo makubwa kutokana na ujumbe uliyomo ndani yake.Katika ngoma hiyo ‘Sikomi’ Diamond amezungumzia maisha yake ya kimahusiano na wanawake maarufu kama Wema Sepetu, Penny na baby mama wake, Zari The Boss Lady.Wimbo huo wenye dakika 3:58 Diamond anaeleza baada ya kupambana kwa kipindi kirefu hadi kuja kutoka kimuziki aliamini pengine maisha yake ya kimahusiano yangekuwa vizuri kitu ambacho anakiri hakijamtokea tangu pale alipokutana na mrembo kutoka Bongo Movie. Licha ya kutomtaja mrembo huyo bila shaka anamzungumzia Wema Sepetu kwani ndiye mrembo pekee wa Bongo Movie aliyeanza kudate naye na couple yake kuwa na nguvu zaidi.Hata hivyo katika verse ya pili ya ngoma hiyo ndipo ameweka wazi kuwa anayemzungumzia ni Wema Sepetu kwa kueleza licha ya kumpenda sana lakini bado aliusumbua moyo wake. MOYO ALIUPATI

Mmiliki wa shule ashitakiwa kwa mauaji

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi imewasomea shitaka la mauaji watu watatu wanaotuhumiwa kumuua kijana Humphrey Makundi aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo Moshi. Watuhumiwa hao ni mmiliki wa shule ya Scolastica, Edward Shayo mwenye miaka 63, mlinzi wa shule hiyo Hamis Chacha mwenye miaka 28 na Laban Nabiswa mwenye miaka 37. Upande wa Jamhuri katika shitaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi, Julieti Mawore umewakilishwa na Mwanasheria Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea, Faygrace Sadallah. Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka mbele ya mahakama hiyo, Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshitakiwa wa kwanza, Hamis Chacha wa pili Edward Shayo na wa tatu Laban Nabiswa, walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi. Aidha washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shitaka la mauaji huku akiwataka kusubiri kufany

Biblia ya Jomo Kenyatta Yatumiwa Kumwapisha Uhuru Kenyatta

Image
Mzee Jomo Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kwanza wa Kenya mwaka 1964. KATIKA hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Kenya na Makamu wake, imeelezwa kuwa, nakala ya Biblia iliyotumiwa kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta ni ile iliyotumiwa kumwapisha kwa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta ambaye ni baba’ke rais wa sasa wakati nakala ya Katiba ni iliyotiwa saini wakati wa kurasmishwa kwa Katiba ya sasa mwaka 2010 uwanjani Uhuru Park. Biblia hiyo ilitumika mwaka 1964 kumwapisha Jomo Kenyatta, 2013 kumwapisha Uhuru kenyatta na leo Novemba 28, 2017 kumwapisha Uhuru Kenyatta katika Uwanja wa Kasarani. Uhuru Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kenya mwaka 2013. Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi amemwapisha Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Kenya kwa mhula wa miaka mingine mitano ijayo na William Ruto kuwa Makamu wake. Rais Kenyatta: “Nitatekeleza majukumu yangu, na wajibu wangu katika Ofisi ya rais wa Kenya, na kwamba nitatenda haki kwa wote kwa mujibu wa Katiba hii kama il

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMWAKILISHA JPM KUAPISHWA KWA KENYATTA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta. Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana. Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Nairobi 28 Novemba, 2017. Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Nairobi, kumwakilisha Rais Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa Rais

Kauli ya zitto Kabwe baada ya Rias Magufuli kutohudhuria kuapishwa kwa Kenyatta

Image
Zitto Kabwe amefunguka na kusema kitendo cha Makamu wa Rais Mhe. Samia kupokelewa na Balozi Kenya ni ishara kuwa mahusiano ya Tanzania na Kenya hayapo vizuri na kudai Rais Magufuli kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa Kenyatta inaweza kueleweka. Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kitendo cha Rais Magufuli kutohudhuria kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta inaweza kueleweka kwani kiongozi huyo hakuweza kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame. "Makamu wetu wa Rais kupokelewa na Balozi ( sio hata Waziri wa Mashauri ya Kigeni au Waziri mwengine) ni dalili kuwa mahusiano yetu yanalega lega. Rais kutokwenda Kenya inaweza kueleweka maana hata Rwanda hakwenda kwenye uapishaji wa Paul Kagame" aliandika Zitto Kabwe.

ANGALIA PICHA MAGARI YALIYO FICHWA PORINI NA ALIYEKUWA RAIS WA GAMBIA

Image
Rais wa The Gambia Yahya Jammeh alilazimika kuyaficha magari yake ya kifahari yapatayo 13 katika msitu wa Kanilai, baada ya kubanwa sana kuhusu ufujaji wa fedha……..Magari hayo (Yakiwemo Rolls Royce 2 na Mercedece Benz 3) yaligunduliwa na jeshi la ECOWAS    

Kinana, Nape waunganisha nguvu tena

Image
 Arumeru. Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na mbunge wa Mtama, Nape Nnauye wameunganisha nguvu katika Kata ya Makiba ambako wanampigia debe mgombea wa chama hicho, Samson Laizer. Kinana na Nape wanachukuliwa kama wanasiasa waliofanya kazi kubwa ya kuhuisha nguvu ya CCM kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopita baada ya kuzunguka karibu nchi nzima kupiga siasa na wakati mwingine kudiriki hata kuwasema hadharani mawaziri wa Serikali ya CCM, wakiwaita mizigo. Jana wawili hao waliungana na Mrisho Gambo, ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha na Alexander Mnyeti (Manyara) kuipigia debe CCM. Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Makiba wilayani Arumeru, Kinana alisema ni vigumu vyama vya upinzani kushika nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao. Kinana alisema akiwa katibu mkuu wa CCM ametembelea mikoa, wilaya na kata tofauti ambako ameona wananchi wana imani kubwa na chama hicho. Kinana alisema katika uchaguzi mkuu uliopita wananchi wa eneo hilo walipig

Alichokisema Dk Slaa baada ya kuteuliwa

Image
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua kuwa Balozi wa Tanzania na kusema kuwa yuko tayari kutoa mchango wake katika kulijenga taifa la Tanzania. “Kwa sababu Ubalozi uko kwenye Idara za moja kwa moja za mkuu wa nchi, na bila shaka hakukuwa na sababu mkuu wangu kutotaka kuniteua, ninamshukuru kwa uteuzi huo kwa kuniona, ninachoweza tu kusema katika hatua hiyo ni kwamba ninao wajibu mkubwa hasa katika kipindi hichi cha kulijenga taifa letu,” amesema Dkt. Slaa. Dkt. Slaa ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, na ambaye aliwahi kugombea nafasi ya Urasi kupitia chama hicho, alijiuzulu nafasi yake hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuondoka nchini. Muda mfupi baadaye Dkt. Slaa alitangaza kutojihusisha tena na siasa za hapa nchini na akawa anaishi nchini Canada pamoja na mpenzi wake Josephine Mushumbusi. Dk. Slaa, ambaye kwa sasa ana

BREAKING : AJALI MBAYA YAUWA WATU 10 NA KUJERUHI 24 MKOANI SINGIDA

Image
Gari aina ya Noah iliyopata ajali kwa kugongana na lori katika eneo la Kijiji cha Isuna , mkoani Singida na kusababisha vifo vya abiria 13, jana. Picha na Gasper Andrew <span data-mce-type="bookmark" style="display: inline-block; width: 0px; overflow: hidden; line-height: 0;" class="mce_SELRES_start"></span> Watu kumi wamekufa na wengine 24 kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Noah, katika eneo la Ihuka mkoani Singida. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, dereva wa gari aina ya Toyota Hiace alikuwa akijaribu kulipita gari jingine bila mafanikio, ndipo alipogongana na gari hilo nakusababisha maafa makubwa. Gari aina ya Noah iliyopata ajali kwa kugongana na lori katika eneo la Kijiji cha Isuna , mkoani Singida na kusababisha vifo vya abiria 13, jana. Picha na Gasper AndrewBRE

Rais Magufuli Amtumia Spika Wa Bunge Salamu Za Rambirambi Kifo Cha Gama

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mh. Leonidas Tutubert Gama. Mhe. Leonidas Tutubert Gama amefariki dunia jana tarehe 23 Novemba, 2017 saa 4:25 usiku katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho, iliyopo Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma ambako alikimbizwa kwa matibabu baada ya kuugua ghafla. “Nimepokea kwa mshtuko na majonzi taarifa za kifo cha ghafla cha Mhe. Leonidas Tutubert Gama, nakupa pole Mhe. Spika Job Ndugai, Wabunge na wafanyakazi wa Ofis yako, na kupitia kwako naomba uzifikishe salamu zangu za pole kwa familia ya Marehemu, wananchi wa Jimbo la Songea Mjini na Mkoa mzima wa Ruvuma, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu” amesema Mhe. Rais Magufuli. Aidha,, Mhe. Rais Magufuli amem