RAIS KIKWETE AMZIKA KISUMO MWANGA
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima
za mwisho mbele ya jeneza la Kada Mkongwe wa CCM Marehemu Mzee Peter
Kisumo wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika huko kijijini kwake
Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mama Hosiana Kisumo Mke wa
Marehemu Peter Kisumo wakati wa mazishi yake huko Usangi Mwanga Mkoani
Kilimanjaro.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo
katika kaburi la Kada Mkongwe wa CCM Marehemu Peter Kisumo wakati wa
mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kilichowekwa
kanisani wakati wa mazishi ya kada mkongwe wa CCM Mzee Peter Kisumo
yaliyofanyika kijijini kwake Usangi-Mwanga Mkoani Kilimnjaro.
(Picha na Freddy Maro)
Comments
Post a Comment