Wema Aibu mpya! Anaswa na mwanaume hotelini
Wem Sepetu ‘Madam’ akidendeka
na mwanaume mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli iliyopo Msasani jijini Dar.
Mwandishi wetu
Licha ya kudai kwamba skendo za
ngono sasa basi, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
amekwaa aibu mpya baada ya picha zake kunaswa akiwa na mwanaume mwingine
kwa mara nyingine, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli iliyotajwa kwa jina la Cape-town
Fish Market iliyopo Msasani jijini Dar.
MADAI MAZITO
Chanzo chetu ambacho ni makini
kilipenyeza kuwa, katika tukio hilo la hivi karibuni, staa huyo alikuwa
hafahamiani na mwanaume huyo, lakini kuna kijana mmoja ambaye mara
nyingi anawakuwadia mastaa wa Bongo kwa matajiri, alidaiwa kumtonya Wema
kuwa kuna ‘mchati’ anataka kutoka naye.
Kilifunguka kwamba, baada ya Wema
kung’atwa sikio juu ya Mkongomani ambaye ana ‘hela chafu’, alidaiwa
kuonekana kuchachawa hivyo eti alikubali kupelekwa kwake akajazwe
‘mihela’.
Wakiwa wamekumbatiana.
WAKUTANA, WAFANYA YAO
Chanzo hicho kilizidi kumwaga habari za
jikoni kuwa baada ya Wema kufika hotelini hapo, alitambulishwa kwa
Mkongo huyo ambapo baada ya kusalimiana tu, walikaa pamoja na kuanza
‘kufanya yao’.
WAJIACHIA PICHA WAAA!
Mpashaji wetu alizidi kufunguka kuwa
baada ya kukaa na kupata kinywaji cha kutosha, walianza kupiga picha
mbalimbali bila kujali kama kuna watu wanaweza kuwapiga picha na baada
ya hapo walianza kupigana mabusu yaliyowaacha hoi wapiga chabo a.k.a
wavimba macho.
“Yaani baada ya pombe kukolea, ilikuwa
ni balaa. Wema wala hakuona aibu tena, walikuwa wakipiga picha
mbalimbali mpaka wanapigana makisi ya mdomoni kitu ambacho watu wengi
walikuwa wakikishangaa sana,” kilisema chanzo hicho.
MKONGO ‘AMB-LOCK’
Mpashaji huyo alidai kwamba, baada ya
Wema na Mkongo huyo kukutana na kumaliza ‘shida’ zao, kila mtu alichukua
hamsini zake huku jamaa huyo ‘akim-block’ Wema kwenye simu.
WEMA ANASEMAJE?
Baada ya kujazwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Wema kusikia anasemaje, lakini simu yake haikuwa hewani.
Alipofuatwa nyumbani, habari
zilizopatikana zilieleza kwamba, Wema alikuwa Dodoma kwenye vikao vya
uteuzi wa wagombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baada ya taarifa hizo, gazeti hili lilitimba kwenye hoteli hiyo kumsaka Mkongo huyo lakini lilielezwa kuwa ameshatimua.
NI AIBU MPYA?
Ukimwacha Mkongo huyo, huko nyuma Wema
aliwahi kuripotiwa kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo, TID, Mr Blue,
marehemu Steven Kanumba, Yusuf Jumbe Yusuf, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na CK huku wengine zikiwa ni skendo tu
na mwenyewe kuzikanusha.
Comments
Post a Comment