TONTO DIKEH AOLEWA, ABADILI JINA INSTAGRAM
Muigizaji kiwango kutoka Nigeria, Tonto Dikeh.
Lagos ,NIgeria
MUIGIZAJI
kiwango kutoka Nigeria, Tonto Dikeh ameolewa rasmi na aliyekuwa mpenzi
wake, Churchill Olakunle Oladunni wiki iliyopita.Tarifa za kuolewa
zilianza kuzagaa mapema wiki iliyopita baada ya staa huyo kubadili jina
lake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kujiita, Mrs Tonto Wigo
Dikeh-Churchill.
Lakini
wikiendi iliyopita zilizagaa picha mitandaoni zikimuonyesha staa huyo
akiwa na mumewe huyo mpya lakini kubwa zaidi ni ile ambayo amepiga na
bibi yake wakiwa wanapongezwa kwenye sherehe hiyo.
Tayari
inadaiwa kuwa Tonto ni mjamzito na bibi yake huyo ameonekana kuumia
zaidi baada ya kudai kuwa anamuacha peke yake kwani alizoea kuishi naye
lakini amemtakia maisha mema na mumewe huyo.
Comments
Post a Comment