MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA KUTUMIA SEHEMU YA MSHAHARA WAKE KUWALIPA WANASHERIA
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kushoto), akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa ya
utatuzi wa migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.
Wanahabari wakiwa katika mkutano na Bwana Makonda.
Waandishi wa habari kutoka vyombombalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema atachukua sehemu ya
mshahara wake kwa ajili ya kuwalipa wanasheria watano watakao kuwa
wanafanya kazi ya kusikiliza na kuwasaidia wananchi wenye migogoro ya
ardhi.
Makonda
alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa ya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika wilaya yake ya
Kinondoni Dar es Salaam leo asubuhi.
"Kama
nilivyobadilisha mfumo mzima wa PF3 ndivyo ninavyofanya kwenye ardhi
nimechukua hatua mahususi kuchukua sehemu ya mshahara wangu na kuajiri
jumla ya wanasheria watano watakao wasaidia wananchi hasa wanyonge
kupata haki zao juu ya madai yao mbalimbali yahusuyo ardhi" alisema
Makonda.
Alisema
wanasheria hao watachukua asilimia 75 ya mshahara wake kwa kazi hiyo
hivyo mwananchi wa Wilaya ya Kinondoni hatatakiwa kulipa hata senti tano
atakapokuwa amekwenda kupata huduma hiyo.
Makonda
alisema kuwa kuanzia Jumatatu ya Juni 15, 2015 wanasheria hao
watakuwepo ofini kwake watakaofanya kazi saa zote kwa lengo la kusaidia
ili wapate uelewa wa kisheria juu ya haki zao zozote kuhusu umiliki wa
ardhi.
Makonda
alisema heshima aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete ya kumteua kuwa mkuu
wa wilaya hiyo kwake anatafsiri kama changamoto kubwa ya kuhakikisha
anashughulikia kwa kina matatizo ya msingi ya wilaya hiyo.
Alisema
katika wakati huu huwezi kutaja changamoto kubwa tatu za wilaya hiyo
ukaacha kutaja migogoro ya ardhi na kuwa kwa ufafanuzi zaidi unaweza
kurejea hotuba yake ya Februari 28, 2015 wakati akianza kazi mambo
aliyoyataja na kuyapa kipaumbele ambapo alitenga kila siku ya Ijumaa
kuwa ni siku ya kukutana na watu wenye migogoro ya ardhi ili kuitatua.
Makonda
alisema ili kumaliza changamoto hiyo ya migogoro ya ardhi kama si
kuipunguza kwa kiwango cha juu kila mkazi wa wilaya hiyo anatakiwa
kuchukua kopi ya hati au nyaraka yoyote ile inayompa uhalali wa kumiliki
ardhi, shamba au kiwanja na kopi hizo zipelekwe kwa ofisi ya mtendaji
wa kata kwani kuanzia Julai 2, 2015 yeye na timu ya watu wa ardhi
atahamishia ofisi yake kwenye kata hizo kwa ajili ya kuzihakiki nyaraka
hizo.
Alisema
pindi watakapo baini kuwa kiwanja kimoja kina zaidi ya mmiliki mmoja
watamtafuta mmiliki halali kupitia vyombo walivyonavyo na atakayebainika
ameghusi atachuliwa hatua.
Alisema
lengo la kuhamishia ofisi yake kwenye kata ni kufuta kabisa uzoefu wa
kusikitisha wa wananchi mmoja kugundua kwamba kiwanja chake kinamilikiwa
na mtu mwingine baada ya kumwaga roli la mchanga ama tofali.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Comments
Post a Comment