UNYAMA MZITOOO...ONA HUYU MAMA ALIMCHOMA MOTO MTOTO MIAKA 7..
Tukio hilo la kinyama ambalo ni sehemu ya
matukio ya mateso kwa watoto yanayotokea
kila kukicha maeneo mbalimbali nchini, lilijiri
juzikati katika Mtaa wa Nello Kata ya Kaloleni
wilayani Momba mkoani hapa majira ya saa
11:20 jioni.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya
mashuhuda walisema kuwa mtoto huyo
alikuwa akiishi katika mazingira magumu
almaarufu kwa jina la chokoraa hivyo hana
makazi maalum.
Walifunguka kuwa mara baada ya kuwa na
maisha hayo, ilibidi mama Joy amuombe aishi
naye ambapo mtoto huyo alikubali na kuacha
kulala nje ya nyumba na udokozi kwa kuwa
alikuwa anapata chakula.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, walisikia
kelele za mtoto huyo akilia kwa sauti na
walipotoka kumwangalia ndipo wakakuta
ameungua mikono na alipoulizwa kulikoni
alisema kuwa mama Joy ndiye aliyemchoma
akimsingizia kuwa ameiba kiasi hicho cha
fedha.
Walidai kwamba, baada ya kusikia hivyo,
baadhi ya wananchi wenye hasira kali walianza
kumbonda mama Joy huku wakimkokota
kuelekea Kituo cha Polisi Tunduma ili sheria
ichukue mkondo wake.
Hadi gazeti hili ‘linaanua matanga’ eneo la
tukio mama huyo alikuwa ameshikiliwa polisi
huku mtoto huyo akipelekwa hospitalini kwa
matibabu.

Comments
Post a Comment