BIBI KIZEE AZUA TAFRANI JIJINI MWANZA.......NI BAADA YA KUDAI AMEANGUKA KUTOKA ANGANI AKIWA NA WENZAKE BAADA YA KUGOMBANA WAKAMDONDOSHA.



Kila mtu alikuwa na lake kuhusu bibi huyu anayedaiwa kukutwa akiwa uchi huku wengine wakisema ni mgonjwa wa akili na wengine wakidai ni mchawi kaanguka na ungo.


Alipokuwa akihojiwa amedai ametoka Bariadi lakini wenzie aliokuwa nao walimshusha baada ya kutokea ugomvi.

Amedai walikuwa wanne kwenye safari yao hata hivyo wapo wengine waliosema kuwa ni mgonjwa akili na tangu jana amekuwa akionekana maeneo ya hospitali ya sekoutoure akiranda randa.

Mpaka naondoka eneo hilo Polisi walikuwa wamefika ili kutoa msaada kutokana na kundi la watu waliokuwa wamemzunguka na baadhi yao wakitaka apigwe kwa madai ni mchawi.

Hapa chini ni baadhi ya picha zake.
Akiongea huku akichorachora chini.

 Akihojiwa na watu

Hapa muda mchache baada ya kukutwa na Camera ya Kijukuu blog.

Kundi la watu wakimshangaa bibi

Comments

Popular posts from this blog