MWANAMKE MWINGINE TENA ABAKWA HADI KUFA NA MWILI WAKE KUNING'INIZWA JUU YA MTI

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 19 amekutwa amening’inizwa juu ya mti katika kijiji kimoja Kaskazini mwa India, likiwa ni tukio la tatu kutokea ndani ya wiki moja katika Jimbo la Uttar Pradesh.Mwili wa mwanamke huyo umekutwa katika eneo la Moradabad ambapo familia yake imewaambia polisi kuwa alibakwa huku uchunguzi wa madaktari ukiendelea kufanyika.Mwanamke mwingine alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika Jimbo la Uttar Pradesh siku ya Jumatano.Mwezi uliopita mabinti wawili wadogo walibakwa na kundi la watu katika mazingira kama hayo na kuibua maandamano ya hisia kali nchini India.

Siku ya Jumatano, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 nae alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika eneo la Bahraich.
 
Polisi wamesema kuwa alikuwa akipatiwa vitisho na wanakijiji kwa kuuza pombe katika eneo hilo na familia yake ilifungulia kesi watu watano kuhusiana na kifo hicho.

Comments

Popular posts from this blog