NDUGU WANANCHI NAOMBA NISAIDIENI MWENZENU‏


Ndugu  Peter Mashiku anahitaji msaada wa matibabu ya haraka baada ya kuvimba mkono wa kushoto kwa muda mrefu kutokana na pete alizokuwa amevaa
Ndugu  Peter Mashiku mkazi wa Mwatulole mjini hapa anahitaji msaada wa matibabu ya haraka baada ya kuvimba mkono wa kushoto kwa muda mrefu, sasa (kama anavyoonekana pichani)
Hali hiyo imesababisha bwana mashiku aishi kwenye mazingira magumu kutokana na familia yake kumtenga baada ya kuona vidole na kiganja kinazidi kuvimba siku hadi siku hivyo inamlazimu mtu huyo aishi kwa kudra za Mungu na wasamalia wema huku tatizo likizidi kila siku.
Wakiongea na gazeti hili, wakaazi wa maeneo hayo walisema chanzo cha tatizo hilo ni bwana huyo kuvaa pete zaidi ya tatu kama sehemu ya urembo, jirani mmoja wa karibu ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini
“Tunashangaa hata sisi kwani kufuatana na ucheshi, ukarimu na kulea familia kwanza tulichukua kama mzaha kuona mwenzetu anavaa pete nyingi, baada ya wiki mkono ulianza kuvimba sehemu za vidole “Alisema jirani huyo.
Madaktari wa hospitali ya wilaya hii walisema kwa hatua aliyofikia anahitai msaada mkubwa kifedha ili apate vipimo vya juu katika hospitali kubwa. Waliongeza kuwa pete hizo hivi sasa zinaanza kumuathiri kwa kukata sehemu kadhaa na kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa na wasamalia wema huenda hali ikawa mbaya zaidi.
Kwa mujibu wa daktari wa magonjwa ya msongo wa mawazo (saikolojia) Hellen Eric alisema mtu huyo anaonekana kama ana wazimu, lakini vipimo vinaonyesha hali hiyo inatokana na wingi wa vitu anavyofikiria kuhusu maisha yake.
“Akisaidiwa atarudia hali yake kama mwanzo kwani sio kichaa”
Kwa hivyo kutokana na familia yake kusambaratika na wengine kuwa na hali duni anayetaka kumsaidia mawasilianao 0765 866264

Comments

Popular posts from this blog