Loveness Diva atukanwa baada ya kumtaka kimapenzi Lulu Michael...."Nampenda sana huyu binti, ningekuwa mwanaume ningemtongoza"
Mwanadada Loveness aka Diva the Boss mtangazaji wa Clouds fm kipindi cha Ala Za Roho, kinachozungumzia maswala ya mapenzi na mahusian juzi usiku alijikuta akielezea hisia zake kwa Muigizaji Elizabeth Michael a.k.a Lulu na kudai kuwa anampenda sana...
"Kutoka moyoni nampenda sana huyu binti, ningekuwa mwanaume ningemfuata na kumtongoza, sema mimi ni mwanamke tu"
Hii ilikuwa kabla ya kucheza wimbo wa atatamani ambayo ni version ilioimbwa na Lulu. Wimbo halisi uliimbwa na Linnah msanii kutoka THT.
Hata hivyo kauli ya Diva imepokelewa kwa hisia tofauti na watu hasa katika mitandao ya kijamii wakimponda Diva kuwa ni lazima atakuwa msagaji. Angalia baadhi ya comments za mashabiki mbalimbali kutoka page ya Bongoswagz
Comments
Post a Comment