BUNGE LAPITISHA SHERIA WANAUME KUOA WANAWAKE WENGI KADRI WAPENDAVYO
Bunge
nchini Kenya limepitisha sheria inayomruhusu mwanaume kuoa wake wengi
atakavyo, na halazimiki kumshauri mke wake juu ya uamuzi huo.
Katika
marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya Kenya yaliyopitishwa Alhamisi
iliyopita,ndoa zote zitatakiwa kusajiliwa na umri wa chini wa mwanamke
kuweza kuolewa umewekwa ili kuzuia ndoa za mapema za watoto, hasa
wasichana.
Siku
hiyo ya Alhamisi Wabunge wote wanaume, ambao ni wengi, waliunga mkono
kuondolewa kwa kipengele katika Sheria hiyo ya Ndoa kilichomtaka
mwanaume afanye mashauriano na mkewe kwanza kabla ya kuoa mwanamke
mwingine.
Wabunge wanawake walilaani
hatua hiyo, walikuja juu na kususia kikao kwa kutoka nje wakidai Sheria
hiyo haiwatendei haki wanawake
Comments
Post a Comment