MTALII ALIYEKWAMA KILELE CHA MAWENZI MLIMA KILIMANJARO AOKOLEWA.

Mtalii Jeanne Traska kutoka Ujerumani

Bi.Jeanne
Traska kutoka Ujerumani na Muongoza Wageni Athumani Juma wakiwa katika
Lango la Marangu pamoja na vifaa mbalimbali walivyokwama navyo katika
kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro mara baada ya kuokolewa.
Kikosi cha Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa mtaliiBi. Jeanne Traska (32) kutoka Ujerumani pamoja na muongoza wageni Athuman Juma ambao jana walikwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro. Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kufika eneo la kilele cha Mawenzi na kwa kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa kiliweza kuwanasua majira ya kumi na moja jioni.

maalum
iliyoletwa kwa ajili ya zoezi la uokoaji kushindwa kufanya kazi kwa
kuwa mawingu mazito hayakuwezesha marubani kuliona eneo la kilele kwa
urahisi.
Hivi
sasa mtalii huyo pamoja na muongoza wageni wake bado wapo chini ya
uangalizi wa hifadhi kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours
iliyomleta mgeni huyo.
Aidha,
kwa kuwa ni tukio lisilo la kawaida, uongozi wa hifadhi unaendelea
kuchunguza sababu zilizowafanya kuchepuka njia na kuelekea kilele cha
Mawenzi badala ya Kibo. Kwa kawaida Kilele cha Mawenzi huwa hakitumiwi
na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni
amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.
Imetolewa na
Idara ya Mawasiliano
Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa
Tanzania
Tanzania
23.03.2014
Comments
Post a Comment