Hizi ni aina ya 12 za wanaume ambao binti yeyote atakutana nao katika maisha yake

1. MR. THUG LIFE


Faida zake



a. Hukufurahisha na ya kukusisimua

b. Hufanya ucheke

c. Anakua pembeni yako kwa kila jambo na atakupigania na kukulinda



Hasara



a. Mara nyingi  wanatabia za kunywa pombe na kuvuta sana sigara

b. Kila mra hakosi drama za kukushangaza

c. Atakuwa katika hali hiyo ya ukorofi milele


d. Kushikwa na kuwekwa jela ni kawaida yao kutokana na drama zao



2. MR. KWA SASA SINA MSICHANA




Faida  zake

a. Atakuchukua na kukutoa out kila mara

b. Atakutambulisha kwa marafiki zake wote

c. Atakuwa ni mtu wa kukupa pongezi  wakati wote



Hasara

a. Anamchumba ambaye wako naye kwa muda mrefu

b. Hawezi kukuambia kuwa ana mchumba


c. Baada ya kuteka moyo wako nawe umedata ndio atakuambia kuwa ana mpenzi





3. MR. MAARUFU




Faida zake

a. Atakupa  fedha nyingi  na hakuna kukulizwa maswali

b. Ana style nyingi za jinsi anavyoendesha maisha yake

c. Atakuonyesha baadhi ya mambo mazuri katika maisha yako



Hasara

a. Kamwe usije jaribu kuishika simu yake

b. Anamaamuzi ya kutokukushirikisha,  anaweza kuja nyumbani kwako wakati wowote bila kutoa taarifa


c. Anapenda kuwa karibu na marafiki zake zaidi kuliko wewe.



4. MR. MISHEMISHE A.K.A JEMBE




Faida zake

a. Anaweza kukupa mialiko wewe na marafikio zako katika minuso mbalimbali na kumbi nyingi za

b. Unaweza kuwa na heshima  na kila uongeacho na kuchochea mazungumzo pia

c. Anavaaa nguo za gharama  



Hasara

a. Huwezi kujua kama yeye ni shoga au lah kwani hana kazi, muda wote yupo kwake na huoni dalili za kuhangaika lakini ana maisha mema na pombe kila siku

b. Hujifanya anakuwa mkali ukijaribu kumwelezea juu ya mpango wa mahusiano yenu kwenda mbele

c. Ukiwa bado kwenye mstari wa kupata tiketi uingie kwenye pati, au mnuso unaweza kushuhudia drama pale mlangoni na kisha mkaruhusiwa kuingia


d. Ana rundo la picha za yeye na celebrities kibao lakini hawajuani na mmpoja kati ya hao mastaa



5. MR. MSOMI




Faida zake

a. Muda wote yupo smart

b. Anakujali na kuhakikisha unajisikia vyema

c.Ana kazi nzuri sana



hasara

a. Mambo yake yanaboa sana kwani muda mwingi anahangaika na mambo ya kazi

b. Hata kwa bed ni mvivu sana kwana anakuwas kachoka na majukumu

c. Hayuko smart sana na mambo ya mtaani kama kukutoa out kwani anakuwa busy

d. Daima ni mtu wa kukuliza lini tutaonana tena



6. MR. GETO




Faida zake



a. Hukufanya ucheke

b. Anavutia kuwa naye karibu

c. Ana hasira za haraka, lakini kwa ujumla ni mtu poa

d. Atasema yeye anataka uhusiano wa kweli



Hasara

a. Ana watoto 3 au zaidi kwa mama tofauti

b. Anataka kukutumia apate chakula, fedha za matumizi na sio upendo

c. Na kila ukimwambia ukweli juu ya mambo yake anakataa au kuwa mkali


d. Kama ukikaa naer anaweza rudi hata saa tisa usiku na kujitetea alikuwa na marafiki 



7. MR. RASTA




Faida zake



a. Atakufundisha mambo mengi ya upendo na amani  

b. Yeye ni mwanaharakati au mwanamapinduzi

c. Atakupa maneno na falsafa zenye kukupa msukumo wa amani na ni maneno ya kihalisa yenye hisia

d. Anataka mke na familia



Hasara

a. Atakupiga chini akipata binti wa kizungu

b. Ana hela za kufanyia starehe ila hana kazi maalumu

c. Haimiliki suti nzuri, siku zote amevaa kombati au jinsi na kutokwa na jasho


d. Mwishoni utagundua kuwa alikuwa anakuigizia 



8. MR. FUTURE




Faida zake



a. Atakutambulisha kwa mama yake

b. Ana kazi na atakuwa mtu wa kujirusha na wewe

c. Atakupa fedha za mahitaji yako kama unahitaji

d. Wakati mwingine huenda kanisani Jumapili



Hasara

a. Wakati mwingine naye anataka kuwa mtu wa kuishi free

b. Ni mtu wa kuvaa mikufu na saa fake

c. Kuna wakati yeye yuko busy na kufuatilia michezo aipendayo na kukusahau wewe kama upo


d. Baada ya kuachana ndio utagundua alikuwa ana mabinti kibao.



9. MR. KICHECHE




Faida zake



a. Atakuambia ukweli - kwamba wewe sio mmoja tu kwake

b. Yeye atakwambia kwamba umembadilisha na yuko tayari kutulia na wewe

c. Anakaa kwake ana usafiri na atakuomba uhamie pale make wote



Hasara

a. Hawezi kukutambulisha kuwa wewe ni mpenzi wake mkiwa sehemu hasa akiona kuna wanawake

b. Kwa ujumla yeye ni mzushi wa kila afanyacho

c. Anatarajia wewe kuamini uongo wake wote kwa sababu tu alikuambia ukweli kuhusu wanawake wengine alipkuwa nao


d. Baada ya kumdaka uongo wake atajitetea alishakuambia kuwa alikuwa kicheche 



10. MR.NINA KAZI NZURI




Faida zake



a. Bila shaka ana kazi

b. Hana tabia nyingi mbaya sana

c.Atachukua wajibu wa kukuhudumia wewe wakati wewe ni mgonjwa

d. Atakwambia kwamba yeye ana upendo wa dhati na wewe



Hasara

a. Utadumu naye katika uhusiano wa miaka 2 au zaidi na kisha unakuja kugundua ni mvivu, mpuuzi na bedui  ambaye anataka wewe kufanya kazi zote za mke  lakini si kukupa pete.

b. Atamaliza kwa kukuambia anakupenda ila wewe sio chaguo lake


c. Baada ya kukuacha miezi mitatu baadae anafunga ndoa 



11. MR. RAFIKI WA UHAKIKA




Faida zake



a. Yeye ni rafiki yako bora, uamweleza kila kitu kinachokusibu na mnakwenda pamoja vizuri sana

b. Anatoa ushauri kwa wakati unapopatwa  na matatizo

c. Ni mwanaume wa kweli  

d. mwelewa na anakujali na ni mcheshi wa kupindukia



Hasara



a. Manishia kujirusha na mwishowe unakuja kugundua hana lolote yeye anataka sex basi.


b. Hapo unahitaji kupata mpenzi mpya kwani yeye hana mpango wa maisha na wewe 



12. MR. MWANAUME SAHIHI







Faida zake

a. Yeye anampenda Mungu na anachukua uhusiano wake na Mungu kwa umakini

b. Yeye ni mwelewa, ana kipaji na uwezo wa kukuchukua wewe kiakili na kihisia

c. Naye atakupenda hata wakati wewe haupendeki

d. Yeye ana ujuzi wa kufanya kazi kwa ustadi na anapendwa !

e. Anakubali makosa yake na inajitahidi kuwa mtu bora

f. Anaelewa uhusiano unajengwa kwa  200% . Yeye100% na wewe  100%

g. Yeye hana kundi la watoto wa mama, yeye ni nadhifu zaidi na anakitambua.

h. Yeye ni rafiki wa bora wa kweli na kila kitu unachotaka kwa mwanaume yeye anacho

i. Alikuwa mzuri ulivyokutana naye ila baada ya kukaa naye unagundua anazidi kuwa nadhifi zaidi

j. Anaweza kupangilia mavazi - anajua tofauti kati ya mavazi rasmi , ya kawaida, ya kitaaluma, ya biashara

h. Yeye anampenda mama yake na kuheshimu wanawake



Hasara



a. Hujawahi kutana naye na kama yupo basi ana mke au mchumba .

b. Yeye hataki uhusiano wowote kwa sasa

c. Umeshamsikia sana mtu wa aina hii lakini kamwe hujakutana naye na lazaidi umeshakutana na aina hizo hapo juu za wanaume na wakakuchezea vilivyo
credit-tabasamunafuledi

Comments

Popular posts from this blog