BONY MWAITEGE AFANYA KWELI TAMASHA LA KRISMAS DODOMA
Mwimbaji wa muziki wa injili nchini Bony Mwaitege akiimbisha mashabiki wake kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati akiimba kwenye tamasha la Krismas lililofanyika leo na kushirikisha waimbaji wa muziki wa injili kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania , Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam na tamasha la leo lilikuwa linahitimisha ziara ya mikoa minne ya Tanzania ambako matamasha hayo yamefanyika ambayo ni Dar es salaam, Morogoro, Tanga, Arusha na tamasha la leo mjini Dodoma.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DODOMA)Mwimbaji wa muziki wa injili nchini Bony Mwaitege akisalimiana na mashabiki wake wakati alipokuwa akiimba kwenye uwanja waJamhuri Mjini Dodoma leo.Mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Tarime na Mwandishi wa vitabu Nyambari Nyangwine akitoa neno kwa mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kulia ni Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion.aadhi ya mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha la Krismas wakiimba pamoja na mwimbaji Upendo Nkone hayupo pichani wakati akifanya vitu vyake jukwaani.Hapa ni kusifu na kuabudu tu.Ikafika saa ya maombiMashabiki wakitoa ushirikiano kwa mwimbaji Upendo Nkone hayupo piuchani.Upendo Nkone akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.Upendo Nkone akicheza na mashabiki wake.Mwimbaji Rose Muhando akikata kiu ya mashabiki wake mjini Dodoma leo.Hii ni sataili ya kucheza kiduku kwa kumsifu yesu kaazi kwelikwe.Upendo Kilahiro akiimba na waimbaji wenzake kutoka kushoto ni Edson Mwasabwite, Tumaini Njole na Faraja Ntaboba.kutoka kulia ni Edson Mwasabite, Tumaini Njole na Faraja Ntaboba kutoka DRC Kongo wakiimba kwa pamoja.Baadhi ya mashabiki wakiwa katika tamasha hilo. Mwimbaji Tumaini Njole akifanya vitu vyake.
Vijana wa kazi The Voice wakifanya vitu vyao katika tamasha hilo.
Comments
Post a Comment