BABY MADAHA AZIDI KUMWANDAMA DIAMOND

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘amemshika uchawi’ msanii mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kufuatia madai kuwa, kuna msanii maarufu Bongo alikwenda kwa mganga wa kienyeji Tanga akitaka kumfanyizia ‘madongoloji’ mrembo huyo ili mambo yake yaende ndivyo sivyo.
Baby Joseph Madaha.
ILIKUWAJE KWANI?
Desemba 22, mwaka jana, mtu mmoja aliyedai ni sangoma aishiye Tanga mjini alituma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kupitia simu ya chumba cha habari Global akiomba namba ya Baby Madaha.

Mtu huyo alisema anaomba namba hiyo kwa sababu kuna mtu alikwenda kwake (Tanga) akitaka amfanyizie Baby Madaha mambo yaende kombo.

Nasibu Abdul ‘Diamond’.
NAMBA YA BABY MADAHA YARUSHWA
Baada ya meseji hiyo kusomwa, mtu huyo alirushiwa namba ya Baby Madaha kisha ujumbe wake ukafowadiwa kwa mrembo huyo.

BABY MADAHA AENDA HEWANI
Dakika tano baada ya Madaha kufowadiwa ujumbe huo, alikwenda hewani kwa simu iliyomtumia ujumbe ambapo bila salamu alisema:
“Huyo atakuwa Diamond tu, hakuna mwingine. Mimi nimeaga  kwetu, hata siku moja Diamond asifikirie kuwa mambo yangu yanaweza kuniendea kombo.

“Kwa chochote alichonifanyia akae akijua lazima kimrudie hii namba nyingine kabisa, hajui uzito wangu. Ni heri asinifuatilie, kitakachomtokea asubiri tu kukiona, atajuta milele,”alisema msanii huyo.
Alisema: “Tatizo kubwa la Bongo, wasanii hatupendani. Unapokwazana na mtu kidogo tu, basi atakufanyia ubaya mambo yako yayumbe.

“Sababu kubwa ya Diamond kuniendea kwa ‘mtaalam’ ni lile bifu lilozuka baina yangu na yake,” alisema Madaha.
DIAMOND ASAKWA
Baada ya madai ya Baby Madaha, paparazi wetu alimsaka Diamond kwa njia ya simu ili ajibu tuhuma zinazomkabili lakini hakupokea simu.
Ilibidi Amani limtumie ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na kumweleza kila kitu, lakini pia supastaa huyo hakujibu kitu.

Hata hivyo, kufuatia bifu la Diamond na Baby Madaha  kumekuwa na pongezi kwenye mitandao ya kijamii ikimpe 5 Diamond kwamba ukimya wake wa kutojibizana na Madaha ni ukomavu.
Wengi wamesema anachokifanya Diamond ndiyo ustaa na si Baby Madaha ambaye kila kukicha anaweweseka kwa jina la Diamond.

TUJIKUMBUSHE
Awali, wasanii hao waliingia kwenye bifu zito baada ya Baby Madaha kumtupia kashfa nzito Diamond akidai kuwa ni fuska, umaarufu alionao hauendani na ubora wa kazi zake.
Katika madai hayo, Diamond alisema  hawezi kijibizana na mwanadada huyo kutokana na ‘levo’ yake kuwa juu.

Comments

Popular posts from this blog