DINA MARIOS APIGWA MIMBA NA RUBEN "NCHA KALI" ... DINA MARIOS AANIKA LIVE KILA KITU KUHUSU MAHABATI YAO
Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’.
SIYO siri tena! Uhusiano wa kimapenzi kati ya watangazaji nyota Bongo, Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ sasa upo hadharani.
SIYO siri tena! Uhusiano wa kimapenzi kati ya watangazaji nyota Bongo, Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ sasa upo hadharani.
Kwa muda mrefu Dina na Ruben wamekuwa kwenye uhusiano lakini wamekuwa
wakijitahidi kuuficha usijulikane na watu, lakini hata hivyo watu wa
karibu hasa wanaofanya nao kazi, walifahamu juu ya uhusiano huo.
Akizungumza katika Kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Radio Clouds
Fm ya jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita kwa mara ya kwanza Dina
alifunguka kuhusu kuwa na uhusiano na Ruben huku akiweka wazi kuwa ana
mimba yake.
“Ni kweli baba mtarajiwa wa mtoto wangu ni Ruben Ndege ambaye kwa sasa
ni Mkurugenzi wa Skylight Band. Wengi hapa kazini mnajua kuwa tulianza
naye mbali. Kulikuwa na kupanda na kushuka, mara kwa mara lakini
nashukuru sasa uhusiano wetu umeimarika,” alisema Dina.
Alisema, katika muda aliokuwa katika uhusiano na Ruben, kuna wakati
walikuwa wakiachana na kurudiana lakini anamshukuru Mungu kwa
kuwasimamia na kuwafikisha katika hatua hiyo.
Siku hiyo Dina alikuwa akiaga wasikizaji wake, kwa vile atakuwa na
likizo ya uzazi ya miezi minne wakati huu akisubiri kujifungua na kumlea
kichanga chake
tuangaze blog
Comments
Post a Comment