Breaking: Halima Mdee Akamatwa Tena Segerea
MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kada wa hicho, Kilewo Mwanga, wamekamatwa leo Ijumaa, Machi 13, 2020, katika Gereza Kuu la Segerea jijini Dar es Salaam, walipokwenda kumpokea Mwenyekiti wa chama hicho wa taifa, Freeman Mbowe, ambaye ameachiwa leo baada ya kulipa faini aliyohukumiwa yeye na wenzake tisa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Jumanne wiki hii.
Askari Magereza wametumia silaha za moto na kufyatua risasi hewani kuwatawanya wafuasi wa chama hicho waliokuwa nje ya gereza hilo kumsubiri Mbowe akiachiwa.
Baadhi ya viongozi na wananchi kadhaa wamejeruhiwa, akiwemo dereva mmoja wa bodaboda ambaye inadaiwa amevunjika mguu.
Comments
Post a Comment