Breaking News: Corona Yatua Kenya, Mmoja Athibitika


TUKIO la kwanza la virusi vya Corona limethibitishwa nchini Kenya. Wizara ya afya imethibitisha tukio hilo kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe.

Akizungumza na vyombo vya habari waziri huyo amesema kwamba kisa hicho kilithibitishwa Alhamisi usiku.

Amesema tukio hilo ni la kwanza kuripotiwa nchini Kenya tangu kuzuka kwa mlipuko huo mjini Wuhan nchini China. Kisa hicho ni cha raia wa Kenya aliyewasli humu nchini kutoka Marekani kupitia mji London nchini Uingereza tarehe 5 mwezi Machi 2020.

Aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya wizara ya afya nchini Kenya. Hata hivyo, waziri huyo amesema kwamba mgonjwa huyo ambaye ni mwanamke yuko katika hali njema na kwamba viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida.

”Tarahe 5 mwezi Machi, 2020,  aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya serikali lakini sasa viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida ambapo anakula vizuri lakini hawezi kutolewa hadi virusi hivyo vitakapokwisha mwilini.”

Waziri huyo amewataka Wakenya kuwa watulivu na kuacha wasiwasi akisema  serikali ya Kenya kupitia wizara ya afya itaendelea kuimarisha mikakati ili kuhakikisha hakuna usambazaji wa virusi hivyo zaidi.


Comments

Popular posts from this blog