BREAKING NEWS: NGOMA NI MALI YA AZAM FC, RASMI DILI LIMESHAKAMILIKA, APELEKWA SAUZI
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akiwa ndani ya jezi ya Azam (kulia) akiwa na kiongozi wa Azam. Uongozi wa Azam FC umethibitisha kuwa umeingia makubaliano ya usajili na mshambuliaji Donald Ngoma, kwa ajili ya msimu ujao 2018/2019. Baada ya kuingia makubaliano hayo, muda wowote kuanzia sasa Azam FC inatarajia kumpeleka mchezaji huyo katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya afya ili kuona ni kwa kiasi gani majeraha yaliyokuwa yakimsumbua yamepona. Azam FC inaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo kutoka nchini Zimbabwe aliyewahi kuchezea FC Platinum ya huko kabla ya kuhamia Yanga, ni sehemu tu ya mikakati ya benchi la ufundi na uongozi katika kuboresha kikosi kwenye eneo la ushambuliaji kuelekea msimu ujao. Donald Ngoma akiwa Yanga Aidha kama mambo yataenda vizuri, uongozi wa Azam FC unaamini kuwa Ngoma atakuwa ni miongoni mwa nyota wapya wa timu hiyo watakaoonekana kwenye Kombe la Kagame (C...