Posts

Figa Ya Sasha Yazua Utata

Image
Sasha Kassim. KALIO la muuza nyago wa video mbalimbali za wanamuziki Bongo, Sasha Kassim limezua utata kwa kudaiwa kuwa si halisi. Chanzo kimepenyeza ubuyu kuwa, Sasha amekuwa ‘akijiedit’ kupitia simu yake hivyo watu kumuona ana kalio kubwa tofauti na uhalisia. Sasha akionyesha figa yake bomba. “Wewe kutana naye hivi laivu halafu utaniambia,” alisema mtoa ubuyu. Alipoulizwa Sasha kuhusiana na hilo alisema; “Siwezi kuwazuia watu kuongea sifoji kitu mimi, siri kubwa ya shepu yangu ni mapozi kwenye picha na aina ya mavazi ninayovaa.”

RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya w

Msigwa afunguka haya Bungeni

Image
Kamatakamata ya viongozi wa vyama vya siasa, wakiwemo wabunge leo Februari1, 2018 imemuibua bungeni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kusema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Msigwa ameibua hoja hiyo katika kipindi cha maswali na majibu, baada ya kuulizwa swali la nyongeza akihoji sababu za wanaokamatwa kushikiliwa kwa muda mrefu katika vituo vya polisi. “Mimi ni mhanga wa jambo hili napenda kujua msingi wake ni nini, lini mambo haya yatakoma,” amesema. Mbunge huyo amehoji lini taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu ambayo ilieleza kuhusu kamatakamata itawasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa. Akijibu suala hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde amesema “..,  naomba wananchi wawe watulivu na kujiepusha kufanya mambo yasiyofaa.” Amesema kwa mujibu wa Katiba, tume hiyo inapaswa kuwasilisha taarifa zake kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya haki za binadamu.

Ridhiwani atoa agizo afisa mtendaji kuondolewa mara moja

Image
Chalinze.  Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete ametaka kuondolewa mara moja kwa ofisa mtendaji wa kata ya Vigwaza, Elizabeth Msenga kwa maelezo kuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Ridhiwani ametoa kauli hiyo leo Februari1, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini humo, kutaka mtendaji huyo kupangiwa eneo jingine la kazi. Amesema haiwezekani wananchi wanapata matatizo na kukosa mtu wa kuwasikiliza na kuwasilisha kero zao sehemu husika. “Yaani akija mbunge ndio wananchi wanalalamika jukwaani. Uzembe huu unasababisha wananchi kuwa na hasira na kukichukia CCM wakidhani hakiwasilizi na hakiwajali kumbe ni uzembe wa mtu mmoja tu,” amesema na kuongeza, "Nimezunguka vijiji zaidi ya vinne kero zinazopewa ni nyingi lakini utatuzi wake upo chini ya Serikali ya kata. Nashangaa hata ofisa mtendaji hayupo katika ziara na si mara ya kwanza, hakuna taarifa ya Serikali iliyoandaliwa.” Wakati ombi lake la kutaka ofisa huyo kuondolewa l

TLS wammwagia sifa Rais Magufuli

Image
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Godwin Ngwilimi amepongeza Rais  John Magufuli kwa kutekeleza matarajio ya watanzania.  Ngwilimi ametoa kauli hiyo leo Februari mosi jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama. Pia, ameomba uwezeshaji wa rasilimali fedha katika muhimili wa mahakama ili kushughulikia changamoto zinazoikabili. "Kama chama cha mawakili, tunakuunga mkono na tunaahidi kutoa ushirikiano kwa mahakama pale inapostahili." Ametoa wito akisema, watumishi wa mahakama, majaji, wasajili, watendaji , makarani  na watumishi wengine, mawakili, wanasheria popote walipo wanatakiwa  kutambua mwelekeo wa nchi unabadilika kwa kasi, matarajio ya wananchi , kuondokana na utamaduni wa kuendelea kufanya kazi kimazoea, kutumia fursa zilizopo ikiwamo Tehama ili kuboresha huduma kwa wananchi. Pia  kuendelea kusimamia maadili ya kitaaluma na uadilifu , hata Mungu anape

Lulu Diva arudisha mahari

Image
MWANAMUZIKI wa kike anayekuja kwa kasi Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amerejesha kwa mikono yake mwenyewe mahari aliyokuwa ametolewa na mchumba wake aliyedumu naye kwa takriban miaka mitatu. Chanzo chetu makini kilisema kuwa, mwanamuziki huyo alikuwa afunge ndoa mwishoni mwa mwaka jana lakini kutokana na kuvuja kwa habari kuwa anatoka na mwanamuziki mwenziye wa Bongo Fleva, mwanaume huyo akadai mahari yake. “Kama kuolewa basi Lulu angeolewa mwaka jana mwishoni lakini mchumba huyo alibaini anatoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake akaomba mahari yake irudishwe,” kilisema chanzo. Gazeti hili lilipompigia simu Lulu na kumuuliza madai hayo alisema, ni kweli alirudisha mahari lakini si kwamba mwanaume huyo alijua anatoka na mwanaume mwingine bali alipata shinikizo kutoka kwa ndugu zake. “Aliposhinikizwa sana nikaona isiwe tabu nikamrudishia mahari yake kwa maana alikuwa akiwasikiliza sana ndugu zake ambao walikuwa hawataki anioe,” alisema Lulu. Na Imelda Mtema

BREAKING NEWS: KAMPUNI YA TTCL “YAFUTWA”

Image
Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya (TTCL), sasa haipo tena, imebadilishwa na kuwa Shirika la (TTCL Corporation). Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa, amesema kuwa anamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuona wa kuwa na shirika la mawasiliano madhubuti kwa ajili ya kuleta maslahi mapana ya nchi, huku akitoa shukrani pia kwa Wabunge wote kwa kukubali kupitisha muswada huo. Aidha Prof Mbarawa, amesema uwepo wa sheria ya shirika la mawasiliano unatoa fursa ya kuboresha sekta kwa kuweka mazingira mazuri ya usimamizi wa miundombinu ya mikakati chini ya shirika hilo. Profesa Mbarawa pia amewajulisha Watanzania wote kuwa mabadiliko ya kuhama kutoka kampuni kuwa shirika la mawasiliano hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zinatolewa na kampuni ya simu ya (TTCL) huku akielezwa kuwa wanaodaiwa na iliyokuwa kampuni hiyo watatakiwa kulia madeni yao kama mikataba yao ina

RAIS WA UGANDA AGUSWA NA KIFO CHA MSANII RADIO

Image
Kufuatia kifo cha msanii wa muziki Radio aliyefariki alfajiri ya leo nchini humo, Rais wa Uganda Yoweri Museven ameonyesha hisia zake kwa kuguswa na kifo cha msanii huyo. Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Museven ameandika “Have been told about the untimely death of musician Moses Ssekibogo aka Mowzey Radio. I had only recently made a financial contribution towards his treatment and hoped he would get better. He was a talented young person with a great future ahead of him. May he rest in peace.” Taarifa za kifo cha msanii huyo zinakuja baada ya siku chache zilizopita Rais Museven kutoa kiasi cha Milioni 30 kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo. Vile vile wasanii mbalimbali kama Navio, Diamond, Eddy Kenzo, Professa Jay na wengineo wametumia kurasa zao za mitandao yao ya kijamii kama Instagram na Twitter kutoa pole kwa familia yake. Baada ya kutangazwa taarifa za kifo mashabiki wa msanii huyo na wa Goodkife walifika hospitali hapo kushuhudia kinachoendele

TAMISEMI Yaagiza Shule Ichunguzwe Baada ya Wanafunzi Wote Kupata 0

Image
WIZARA ya Ofisi ya Rais –Tamisemi kupitia kwa Naibu Wairi wake, Joseph Kakunda imemuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Njombe kuchunguza matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Viziwi Njombe. Akiji alipojibu swali la mbunge wa Buyungu (Chadema), Samson Bilago, bungeni leo Jumatano Januari 31,2018, Kakunda  amesema katika matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), shule hiyo katika matokeo ya mtihani uliofanyika Oktoba na Novemba mwaka jana watahiniwa wote 21 wamepata daraja sifuri (0) yaani wamefeli. Bilago alitaka kujua ni kwa nini shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu zinafanya vibaya kwenye mitihani, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema walimu waliosoma elimu maalumu watapata ajira bila kikwazo cha kusubiri huku akieleza kuwa anasubiri kupelekewa orodha ya walimu hao.

AIBU YA MWAKA..! WANASWA LIVE WAKIFANYA UFUSKA KAZINI!

Image
Baada ya kunaswa. NI aibu kubwa! Tangu kuanza kwa mwaka 2018, yapo yaliyotokea na kusisimua, lakini hili la mrembo kunaswa na mwanaume wakifanya ufuska kwenye eneo la kazi, limeibua hisia za aina yake kuwa huenda maisha hayaendi, Ijumaa Wikienda linaifumua. Habari kamili, tukio hilo lilijiri kwenye eneo la kazi la mrembo huyo ambalo ni saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini yeye akadaiwa kucheza mchezo wake wa ngono. Saluni hiyo ipo maeneo ya Sinza-Kwaremy jijini Dar ambapo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikidaiwa kujihusisha na uchafu huo na kusababisha kero kwa wananchi wenye maadili yao. …Akiwa uchi baada ya kunaswa. OFM KAZINI Kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, kikiwa kimetulia ndani ya mjengo wa makao yake makuu, Sinza-Mori jijini Dar, kilipokea simu kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi  wa saluni hiyo akimshitakia mwenzake kuwa amekuwa akijihusisha na ufuska na wanaume mbalimbali wakiwemo waume za

JPM Amjulia Hali Mzee Majuto Hospitalini, Afunguka Alivyomtabiria Makubwa

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea muigizaji mkongwe, Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa. Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara. “Mimi ndiyo mtu wa kwanza kumtabiri kwamba akiwa Rais itakuwa shughuli. Nilishukuru sana kuchaguliwa huyu bwana, tumepata Rais sio masihara watu wote sasa hivi wana adabu zao wanajua nini maana ya kazi”, alisema Majuto. Pamoja na hayo, Mzee Majuto aliendelea kwa kusema “sisi wazee tunafarijika sasa hivi, viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko kwa uoga maana hataki masihara. Hii ndio raha ya kupata viongozi wenye msimamo”. Kwa upande mwin

Mbunge na Mwanasheria Aliyemwapisha Odinga Atiwa Mbaroni

Image
Mwanasheria TJ Kajwang’ (kushoto) na Mbunge Miguna Miguna wakati wa kumuapisha Odinda. JESHI la Polisi nchini Kenya, leo Januari 31, 2018 mchana limemtia mbaroni mbunge wa Jimbo la Ruaraka, Tom J Kajwang’, ambaye alisimamia “kuapishwa” kwa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga kwenye viwanja vya Uhuru Park jana Jumanne. Kajwang amekamatwa na maofisa hao waliokuwa wamevalia kiraia nje ya Mahakama ya Milimani jijini Nairobi muda mfupi baada ya kuhudhuria katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji George Odunga kusikiliza uamuzi wa kesi aliyowawakilisha wabunge wanaopinga kukatwa mishahara yao na posho nchini humo. Kajwang’ na mwanasheria mwingine Miguna Miguna, ndiyo walisimamia matukio yote ya “kuapishwa” Odinga kama ‘rais wa watu’ katika viwanja vya Uhuru Park. Imeelezwa kuwa, Kajwang’ alikuwa amevaa vazi na wigi ambapo alishangiliwa sana na wafuasi wa Nasa wakati Odinga akila “kiapo”.

WEMA SEPETU TENA,CHUCHU AELEZA KUHUSU WEMA KUPATA MTOTO HUKU KUKIWA NA TETESI NA KUWA NA MIMBA

Image
Baada ya baadhi ya mashabiki kumtolea maneno yasiyofaa Wema Sepetu pindi alipoweka picha ya mtoto na Chuchu Hansy katika mtandao wa Instagram, muigizaji huyo amesema Wema hapaswi kuumizwa na hilo kwani utafika wakati wake atapata mtoto. Chuchu Hans ameiambia E-Newz ya EATV kuwa Wema ni rafiki yake na mara kadhaa wao kama wanawake wamekuwa wakiongea na kumshauri na kumtia Moyo. “Nilishamuambia wewe (Wema) utakuja kupata mtoto il sio pale unapohitaji wewe, ni pale ambapo Mungu amekuandikia muda wako ukifika, kwa hiyo hayo maneno wala asimuumie ni changamoto na kutokana na ustaa alionao,” amesema. Mtoto wa Chuchu Hansi anaitwa ambaye amezaa na muigizaji mwenzake, Ray Kigosi.

ANGALIA MPELELEZI ALIYEPOTEZA MIKONO, MIGUU NA UTUMBO,SASA KULIPWA BIL 245

Image
OFISA wa ujasusi (shushushu) katika jeshi la Marekani, Lisa Maria Carter, wa Florida, Marekani, anajitayarisha kulipwa Sh. bilioni 245 (Dola milioni 109 za Marekani) kutokana na kufanyiwa vibaya oparesheni ya kutibu uvimbe uliokuwa umejitokeza katika sehemu ya uzazi mwaka 2010. Lisa Maria Carter alivyo sasa. Hivi sasa, Carter anabidi ahudumiwe kila kitu kutokana na athari aliyopata kutokana na oparesheni hiyo. Mwaka huo, mwanamke huyo akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa aondoke kwa ndege kwenda Iraq kukusanya habari za ujasusi ambapo aliambiwa alikuwa na uvimbe kwenye sehemu ya uzazi (ovarian cyst). …Anavyotembea kwa kutumia nyenzo maalum Katika oparesheni iliyofuata ya kumtibu, ambayo ilifanyika vibaya, ilisababisha apoteze mikono yake yote, miguu, utumbo na misuli ya tumbo. Hii ilitokana na kumsababishia kukumbwa na bacteria zilizoula mwili wake na kuharibu sehemu mbalimbali. …Akiwa na mtaalam wa tiba Katika upasuaji huo, shinikizo lake la damu lilishuka s

Ikulu: Rais Magufuli Akutana na Maafisa Wakuu wa JWTZ

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo kabla hajaanza kuwatambulisha Maafisa Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (hawaonekani pichani) ambao wanatarajia kustaafu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ambaye aliambatana na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao wanatarajiwa kustaafu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaotarajiwa kustaafu ambao ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibolwa wanne kutoka (kulia), Meja Jenerali Michael

Bunge kuunguruma kesho, wabunge watatu kuapishwa

Image
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza kunguruma kesho (Jumanne) na Mkoani Dodoma kwa kuanza kuapisha Wabunge wapya watatu pamoja na kupitisha miswada miwili ya sheria ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tisa. Hayo yamewekwa wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi za Bunge kupitia Kitengo cha Habari na Mawasiliano na kusema kuwataja wabunge hao ambao watakula kiapo cha uaminifu kuwa ni Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kutokea Songea Mjini, Mhe. Monko Justine Joseph wa Singida Kaskazini na kumaliziwa na Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa wa Longido. Aidha, katika mkutano huo wa 10 kutakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na Wabunge huku wastani wa maswali 16 ya kiwa ya papo kwa hapo kuenda kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo yanatarajiwa kuulizwa siku ya Alhamisi mnamo februari mosi. Kwa upande mwingine, Kamati 16 za Bunge za kudumu

Lita 85 za Gongo zakamatwa Manyara

Image
Jeshi la Polisi mkoani Manyara limesema limekamata mitambo ya kutengenezea pombe haramu ya gongo pamoja na lita 85 za pombe hiyo, ambayo ni kinyume na sheria za nchi. Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga, amesema vifaa hivyo pamoja na pombe imekamatwa kutokana na operesheni maalum inayoendeshwa na jeshi hilo. “Mkoa wetu wa Manyara umeendelea na misako mbali mbali ambapo tumekamata mitambo ya gongo pamoja na gongo huko mbulu, kijiji cha hydom Manyara, walimkata mtu mmoja Moshi Bula mwenye miaka 55, akiwa na mitambo minne ya kutengenezea mitambo ya gongo, hivi sasa yupo mahabusu na taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani,”, amesema Kamanda Senga. Kamanda Senga ameendelea kuelezea kwamba...Sambamba na hilo tumekamata lita 65 za pombe haramu ya moshi pamoja na watu watatu wanaohusika na pombe hiyo, ambao ni Neema Doto Matayo, mwenye miaka 21, Law

Sumaye: wanaojiuzulu nafasi zao hawatambui majukumu yao

Image
picha ya mtandao Waziri Mkuu Mstaafu , Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa kazi ya Mbunge ni kutetea wananchi wa jimbo lake na si kwenda kumsifia Rais na kudai wabunge waliojizulu nafasi zao kwa kigezo cha kumuunga mkono Rais hawakutambua majukumu yao. Sumaye amesema hayo kwenye kampeni za Ubunge wa marudio katika jimbo la Kinondoni zinazoendelea na kusema kuwa kwa Wabunge ambao wamejiuzulu nafasi zao na kwenda chama kingine kugombea tena hawafai kabisa kuwa wabunge kwa kuwa hawatambui maana ya Ubunge. "Kazi ya Mbunge si kwenda kumtetea Rais bali ni kutetea wananchi waliompa kura, kama Mtulia yeye anasema ameondoka na kudharau kura za watu wa Kinondoni kwa sababu amependezeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi akateuliwe na Rais kuwa Mbunge maana kazi yake ndiyo itakuwa kwenda kumtetea na kumsifia Rais. Watu ambao wanahama chama eti kwa sababu Rais ametenda mambo mema pamoja na ukweli kwamba mimi naweza kubishana sana maana hatujaona

Nabii Tito Apandishwa Mahakamani, Anyimwa Dhamana

Image
Onesmo Machibya almaarufu Nabii Tito aliyetengeneza vichwa vya habari kutokana na mahubiri yake ya kuhimiza ulevi na uasherati, amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, na kusomewa mashtaka ya kujaribu kujiua. Nabii Tito alifanya jaribio la kujiua Januari 25, mwaka huu akiwa mahabusu, ambapo inadaiwa kwamba alijikatakata na wembe kwa lengo la kuyakatisha maisha yake. Alipotakiwa kujibu mashtaka yanayomkabili, Nabii Tito awali alisema hakumbuki chochote kwa sababu yeye ni mgonjwa wa akili, lakini alipobanwa kwa mara nyingine, alisema ni kweli alitaka kujiua kwa sababu kuna sauti ndani ya kichwa chake iliyokuwa inamuelekeza kufanya kitendo hicho. Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Nabii Tito amerejeshwa rumande huku akiwekewa mapingamizi saba ya dhamana.

Matukio kwa Picha na Video Utambulisho wa Mbosso WCB

Image
WCB wakiwa katika picha ya pamoja, katikati ni msanii wao mpya, Mbosso. BURUDANI ya aina yake imepigwa na wasanii wa Lebo ya WCB usiku wa kuamikia leo wakati kumtambulisha msanii mpya katika kundi hilo, Mbosso ambaye awali alikuwa Yamoto Band kabla ya kundi hilo kuvunjika. Mbosso, Diamond na Rayvanny wakikamua. WCB ikiongozwa na Lejendari, Diamond Platnumz, wamemtambulisha huyo katika Ukumbi wa Hyatt Legency Hotel jijini dar es Salaam na kuhudhuriwa na mastaa kibao wakiwemo, Wema Sepetu na wengine pamoja na wanahabari. Diamond akimsalimia mama yake, Bi Sanura ukumbini hapo. WCB na mashabiki waki-enyoj event. WCB na mashabiki katika picha ya pamoja.   Diamond akikata mauno.