Posts

FIFA YATANGAZA MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018

Image
FIFA limetangaza makundi ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwakani nchini Urusi. Makundi ya Kombe la Dunia 2018 Katika makundi hayo makundi yanayoonekana hatari zaidi ni Kundi C ambako kuna Ufaransa, Australia, Peru na Denmark na Kundi F linaloundwa na Ujerumani, Mexico, Sweden na Jamhuri ya watu Korea. Mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo utafanyika kati ya Mwenyeji, Urusi dhidi ya Saudi Arabia tarehe 24 juni 2018 kunako dimba la Luzhniki.

WEMA SEPETU ATANGAZA RASMI KURUDI CCM

Image
  Wema Sepetu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. MSANII maarufu wa Bongo Movie, Wema Sepetu leo Ijumaa, Desemba 1, 2017 ametangaza rasmi kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai kuwa ni kukosa amani ndani ya chama hicho. Wema ambaye ni alikuwa mshindi namba moja wa Taji la Miss Tanzania 2006, amesema Chadema ni kama nyumba inayomkosesha amani hivyo hana haja ya kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo.Amesisitiza kwake amani ni jambo kubwa sana hivyo anandoka ndani ya Chadema na kurejea nyumbani alikokulia kwa maana ya CCM. Wema na mama yake mzazi, Mariam Sepetu walihamia Chadema mwezi Februari mwaka huu baada ya kuhusishwa kwenye sakata la biashara ya madawa ya kulevya ambapo mpaka sasa kesi yake bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Vurugu Zatanda Kenyatta Akiapishwa, Polisi Wafunga Mtaa Kuzuia Mkutano wa NASA

Image
Polisi wakiimarisha ulinzi eneo hilo. MTAA wa Jacaranda jijini Nairobi, Kenya, leo umefungwa na polisi ili kuzuia mkutano wa umoja wa vyama vya upinzani nchini humo, National Super Alliance (NASA) uliopangwa kwa ajili ya kuwakumbuka wafuasi wake 27 waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa marudio uliofanyika zaidi ya wiki moja iliyopita. Mataili yakiwa yamechomwa moto. Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo ambapo Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa kwa kipindi cha pili katika uwanja wa michezo wa Kasarani. Chumba vya kutunzia maiti katika jiji hilo pia kimefungwa na polisi ambapo watu hawatakiwi kufika hapo. Hali ilivyokuwa eneo la tukio. Polisi waliokuwa na zana zote za kuzuia fujo wamekuwa wakirusha mabomu ya machozi sehemu nyingi yakiwemo maeneo ya wafuasi wa NASA ambao wamefunga barabara kadhaa jijini humo. Wafuasi wa NASA wakipambana na polisi. Mpinzani mkuu nchini humo, Raila Odinga, amepinga mipango ya kumwapisha katika nafasi ya urais, a

DIAMOND PLATINUMZ AIBUA MAPYA,AWASHA MOTO UPYA,WEMA SEPETU,ZARI THE BOSS LADY NA HAMISA KUMEKUCHA KUPITIA WIMBO WAKE MPYA- "SIKOMI"

Image
Wakati msanii wa muziki wa Bongo Flava, Diamond Platnumz ameachia ngoma mbili kwa wakati moja ambazo ni Sikomi na Niache, ngoma ya kwanza imekuwa na nguvu na mapokeo makubwa kutokana na ujumbe uliyomo ndani yake.Katika ngoma hiyo ‘Sikomi’ Diamond amezungumzia maisha yake ya kimahusiano na wanawake maarufu kama Wema Sepetu, Penny na baby mama wake, Zari The Boss Lady.Wimbo huo wenye dakika 3:58 Diamond anaeleza baada ya kupambana kwa kipindi kirefu hadi kuja kutoka kimuziki aliamini pengine maisha yake ya kimahusiano yangekuwa vizuri kitu ambacho anakiri hakijamtokea tangu pale alipokutana na mrembo kutoka Bongo Movie. Licha ya kutomtaja mrembo huyo bila shaka anamzungumzia Wema Sepetu kwani ndiye mrembo pekee wa Bongo Movie aliyeanza kudate naye na couple yake kuwa na nguvu zaidi.Hata hivyo katika verse ya pili ya ngoma hiyo ndipo ameweka wazi kuwa anayemzungumzia ni Wema Sepetu kwa kueleza licha ya kumpenda sana lakini bado aliusumbua moyo wake. MOYO ALIUPATI

Mmiliki wa shule ashitakiwa kwa mauaji

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi imewasomea shitaka la mauaji watu watatu wanaotuhumiwa kumuua kijana Humphrey Makundi aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo Moshi. Watuhumiwa hao ni mmiliki wa shule ya Scolastica, Edward Shayo mwenye miaka 63, mlinzi wa shule hiyo Hamis Chacha mwenye miaka 28 na Laban Nabiswa mwenye miaka 37. Upande wa Jamhuri katika shitaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi, Julieti Mawore umewakilishwa na Mwanasheria Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea, Faygrace Sadallah. Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka mbele ya mahakama hiyo, Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshitakiwa wa kwanza, Hamis Chacha wa pili Edward Shayo na wa tatu Laban Nabiswa, walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi. Aidha washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shitaka la mauaji huku akiwataka kusubiri kufany

Biblia ya Jomo Kenyatta Yatumiwa Kumwapisha Uhuru Kenyatta

Image
Mzee Jomo Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kwanza wa Kenya mwaka 1964. KATIKA hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Kenya na Makamu wake, imeelezwa kuwa, nakala ya Biblia iliyotumiwa kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta ni ile iliyotumiwa kumwapisha kwa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta ambaye ni baba’ke rais wa sasa wakati nakala ya Katiba ni iliyotiwa saini wakati wa kurasmishwa kwa Katiba ya sasa mwaka 2010 uwanjani Uhuru Park. Biblia hiyo ilitumika mwaka 1964 kumwapisha Jomo Kenyatta, 2013 kumwapisha Uhuru kenyatta na leo Novemba 28, 2017 kumwapisha Uhuru Kenyatta katika Uwanja wa Kasarani. Uhuru Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kenya mwaka 2013. Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi amemwapisha Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Kenya kwa mhula wa miaka mingine mitano ijayo na William Ruto kuwa Makamu wake. Rais Kenyatta: “Nitatekeleza majukumu yangu, na wajibu wangu katika Ofisi ya rais wa Kenya, na kwamba nitatenda haki kwa wote kwa mujibu wa Katiba hii kama il

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMWAKILISHA JPM KUAPISHWA KWA KENYATTA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta. Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana. Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Nairobi 28 Novemba, 2017. Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Nairobi, kumwakilisha Rais Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa Rais

Kauli ya zitto Kabwe baada ya Rias Magufuli kutohudhuria kuapishwa kwa Kenyatta

Image
Zitto Kabwe amefunguka na kusema kitendo cha Makamu wa Rais Mhe. Samia kupokelewa na Balozi Kenya ni ishara kuwa mahusiano ya Tanzania na Kenya hayapo vizuri na kudai Rais Magufuli kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa Kenyatta inaweza kueleweka. Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kitendo cha Rais Magufuli kutohudhuria kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta inaweza kueleweka kwani kiongozi huyo hakuweza kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame. "Makamu wetu wa Rais kupokelewa na Balozi ( sio hata Waziri wa Mashauri ya Kigeni au Waziri mwengine) ni dalili kuwa mahusiano yetu yanalega lega. Rais kutokwenda Kenya inaweza kueleweka maana hata Rwanda hakwenda kwenye uapishaji wa Paul Kagame" aliandika Zitto Kabwe.

ANGALIA PICHA MAGARI YALIYO FICHWA PORINI NA ALIYEKUWA RAIS WA GAMBIA

Image
Rais wa The Gambia Yahya Jammeh alilazimika kuyaficha magari yake ya kifahari yapatayo 13 katika msitu wa Kanilai, baada ya kubanwa sana kuhusu ufujaji wa fedha……..Magari hayo (Yakiwemo Rolls Royce 2 na Mercedece Benz 3) yaligunduliwa na jeshi la ECOWAS    

Kinana, Nape waunganisha nguvu tena

Image
 Arumeru. Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na mbunge wa Mtama, Nape Nnauye wameunganisha nguvu katika Kata ya Makiba ambako wanampigia debe mgombea wa chama hicho, Samson Laizer. Kinana na Nape wanachukuliwa kama wanasiasa waliofanya kazi kubwa ya kuhuisha nguvu ya CCM kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopita baada ya kuzunguka karibu nchi nzima kupiga siasa na wakati mwingine kudiriki hata kuwasema hadharani mawaziri wa Serikali ya CCM, wakiwaita mizigo. Jana wawili hao waliungana na Mrisho Gambo, ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha na Alexander Mnyeti (Manyara) kuipigia debe CCM. Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Makiba wilayani Arumeru, Kinana alisema ni vigumu vyama vya upinzani kushika nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao. Kinana alisema akiwa katibu mkuu wa CCM ametembelea mikoa, wilaya na kata tofauti ambako ameona wananchi wana imani kubwa na chama hicho. Kinana alisema katika uchaguzi mkuu uliopita wananchi wa eneo hilo walipig

Alichokisema Dk Slaa baada ya kuteuliwa

Image
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua kuwa Balozi wa Tanzania na kusema kuwa yuko tayari kutoa mchango wake katika kulijenga taifa la Tanzania. “Kwa sababu Ubalozi uko kwenye Idara za moja kwa moja za mkuu wa nchi, na bila shaka hakukuwa na sababu mkuu wangu kutotaka kuniteua, ninamshukuru kwa uteuzi huo kwa kuniona, ninachoweza tu kusema katika hatua hiyo ni kwamba ninao wajibu mkubwa hasa katika kipindi hichi cha kulijenga taifa letu,” amesema Dkt. Slaa. Dkt. Slaa ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, na ambaye aliwahi kugombea nafasi ya Urasi kupitia chama hicho, alijiuzulu nafasi yake hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuondoka nchini. Muda mfupi baadaye Dkt. Slaa alitangaza kutojihusisha tena na siasa za hapa nchini na akawa anaishi nchini Canada pamoja na mpenzi wake Josephine Mushumbusi. Dk. Slaa, ambaye kwa sasa ana

BREAKING : AJALI MBAYA YAUWA WATU 10 NA KUJERUHI 24 MKOANI SINGIDA

Image
Gari aina ya Noah iliyopata ajali kwa kugongana na lori katika eneo la Kijiji cha Isuna , mkoani Singida na kusababisha vifo vya abiria 13, jana. Picha na Gasper Andrew <span data-mce-type="bookmark" style="display: inline-block; width: 0px; overflow: hidden; line-height: 0;" class="mce_SELRES_start"></span> Watu kumi wamekufa na wengine 24 kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Noah, katika eneo la Ihuka mkoani Singida. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, dereva wa gari aina ya Toyota Hiace alikuwa akijaribu kulipita gari jingine bila mafanikio, ndipo alipogongana na gari hilo nakusababisha maafa makubwa. Gari aina ya Noah iliyopata ajali kwa kugongana na lori katika eneo la Kijiji cha Isuna , mkoani Singida na kusababisha vifo vya abiria 13, jana. Picha na Gasper AndrewBRE

Rais Magufuli Amtumia Spika Wa Bunge Salamu Za Rambirambi Kifo Cha Gama

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mh. Leonidas Tutubert Gama. Mhe. Leonidas Tutubert Gama amefariki dunia jana tarehe 23 Novemba, 2017 saa 4:25 usiku katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho, iliyopo Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma ambako alikimbizwa kwa matibabu baada ya kuugua ghafla. “Nimepokea kwa mshtuko na majonzi taarifa za kifo cha ghafla cha Mhe. Leonidas Tutubert Gama, nakupa pole Mhe. Spika Job Ndugai, Wabunge na wafanyakazi wa Ofis yako, na kupitia kwako naomba uzifikishe salamu zangu za pole kwa familia ya Marehemu, wananchi wa Jimbo la Songea Mjini na Mkoa mzima wa Ruvuma, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu” amesema Mhe. Rais Magufuli. Aidha,, Mhe. Rais Magufuli amem

Wolper Alia Kutengwa na Mastaa

Image
Jacquline Wolper. STAA wa Bongo Movies, Jacquline Wolper amesema kuwa mastaa wengi hawapendi kupeana ‘sapoti’, kiasi kwamba hata kama staa mwenzao akiwa na biashara yake wapo radhi kununua kwingine lakini si kwake, ili tu wamkomoe. Akichonga na gazeti hili, Wolper alijitolea mfano kwa kusema kuwa tangu amejiingiza kwenye biashara ya ushonaji, watu wengi ambao wamekuwa wateja wa biashara zake ni wa kawaida tu na wasanii wenzike hawazidi hata watatu. “Unapofanya maendeleo kwa sisi mastaa wenzako si kwamba wanapenda. Wananuna ndiyo maana huwezi kuwaona wakikusapoti,” alisema Wolper.

Tabia 6 za kufuata kupata ngozi laini bila madoa/beauty habits to get glowing skin

Image
1.TUMIA ANTIOXIDANT SERUM. Sio kila mtu ana bahati ya kupata ngozi laini na nyororo bila kuifanyia kazi. Kwa wengine it a must to work hard ili kupata that perfect skin you have always wanted. So Ladies you have to change your beauty routine, unatakiwa uanze asubuhi yako in a healthy way. Jinsi unavyoanza siku yako itaonesha kwenye uso wako. Antioxidants kama vile Vitamin C&E hulinda ngozi yako ili isi dehydrate na pia zile aging radicals zitalindwa from UV-ray pollution na bad dietary habits(kula vibaya). Paka antioxidant serum baada tu ya kutoka kuoga, subiri dakika chache then paka moisturizer yako. 2.KULA PROTEIN YA KUTOSHA. Kula breakfast ambayo ipo high in protein, husisha mayai, karanga, yogurt nk. Hivi husaidia kujenga collagen ambayo ndio kitu kikubwa ambacho hukusaidia ngozi yako isizeeke mapema. Ngozi yako haitokuwa na mikunjo wala kutepeta. Watu ambao hula protein for breakfast hula kidogo for the rest of the day, na pia protein husai

ANGALIA WEMA SEPETU ALICHOSEMA USIKU HUU AKIWA RWANDA,ATOA YA MOYONI

Image
    Spotted walking out of RBA Television earlier today… This will be the last pic I post kwa Leo… For all my Updates fanya kuDownload app yangu mwenyewe… (Feels good to say that)… Goodnyt World

BREAKING : MBUNGE WA JIMBO LA SONGEA MJINI AFARIKI DUNIA

Image
Taarifa zimetufikia asubuhi hii,zikieleza kuwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Songea Mjini,Mh Leonidas Gama amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo.Mbunge wa Songea Mjini Leonidas Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Peramiho alikokuwa anapatiwa matibabu. Marehemu alipata kuwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya kadhaa zikiwemo Ilala, Muheza, Nachingwea, Newala na Mbeya.Tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu zaidi wa taarifa hiyo.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMINA Post Views: 47

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 24.11.2017

Image