Posts

Masharti Mapya Mnada wa Nyumba za Lugumi Kesho

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kevela. ILI kuhakikisha mnada wa nyumba mbili za Lugumi huko JKT Mbweni na Upanga jijini Dar es Salaam unakwenda vizuri, watu watakaofika na kushiriki mnada huo kesho, watabidi kutimiza masharti kadhaa. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kevela, wote watakaofika maeneo hayo watabidi kutoa vitambulisho vyao vya kazini, vya udereva na vya upigaji kura. Isitoshe, kwa mujibu wa Kevela, wote watakaoingia mnadani hapo  itabidi watoe Sh. Milioni mbili kama uhakikisho wao wa dhamira ya kushiriki  na kununua  mali husika, hii ikiwa kwa washangiliaji na watazamaji. Kevela alisema wale watakaoshinda mnada huo, Sh.milioni mbili walizotoa zitakuwa sehemu ya malipo yao, na kwa wale watakaoshindwa, watarudishiwa fedha hiyo baada ya mnada. Alisisitiza pia kwamba washindi wa mnada huo watatakiwa kulipa asilimia 25 ya bei ya nyumba husika waliyoshinda na asilimia 75 iliy

Avuliwa Madaraka Kwa Kumbaka Mwanafunzi

Image
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Abdalah Malela amemvua madaraka Mwalimu Mkuu Masunga Ng’waya wa Shule ya Msingi Mwashagata, iliyopo kijiji hicho kata ya Ihusi kwa kosa la ukosefu wa maadili. Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana, mkurugenzi huyo alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni la baada ya mwalimu mmoja wa shule yake kumrubuni mwanafunzi wake kwa kufanya mapenzi naye tena kwenye nyumba yake, kitendo ambacho ni cha kukosa maadili. “Imebainika hili ni tukio la nne kwa mwalimu huyo kutuhumiwa kufanya mapenzi na wanafunzi tofauti tofauti lakini amekuwa hachukuliwi hatua, lakini mimi kwa mujibu wa sheria nimemvua madaraka mwalimu mkuu huyo ili awe mwalimu wa kawaida, sababu amekosa maadili ya kuendelea kushika wadhifa huo,” alisema mkurugenzi huyo. Aidha, alisema kesi hiyo tayari imefikishwa polisi na wakati wowote mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani. Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga

Miaka 20 Tangu Princess Diana Azikwe, Dunia Bado Inamkumbuka

Image
Princess Diana enzi za uhai wake. Siku ya mazishi ya Princess Diana. Siku ya mazishi ya Princess Diana. Mahali alipozikwa. Jeneza lenye mwili wake. Septemba 6, 1997 ni siku ambayo haitasahaulika, pale mkwe wa malkia Elizabeth, Princess Diana alipozikwa jijini London. Miaka 20 imepita lakini bado kila inapofika siku hii, Waingereza hukumbuka kifo chake kwa kuzuru kwenye kaburi lake, kuweka maua na kuwasha mishumaa. Princess Diana ambaye jina lake halisi alikuwa akiitwa Diana Frances Spencer, alikuwa mke wa mtoto mkubwa wa Malkia Elizabeth, Prince Charles na kabla ya kufikwa na umauti, wawili hao waliofunga ndoa iliyoutikisa ulimwengu Julai 29, 1981, walibahatika kupata watoto wawili, William na Harry. Kifo chake kilisababishwa na ajali mbaya iliyotokea jijini Paris, Ufaransa kwenye daraja la chini la Pont de l’Alma ambapo mwanamama huyo na watu aliokuwa nao ndani ya gari, akiwemo Dodi Fayed na dereva wao, Henri Paul walipoteza maisha huku mtu mmoja

MCHUMBA WA NDIKUMANA AMDUWAZA IRENE UWOYA RWANDA

Image
Mchumba wa marehemu Hamad Ndikumana ‘Ndiku’, Asma amemduwaza mzazi mwenzake na marehemu huyo, muigizaji Irene Uwoya baada ya kumpa mapokezi ya nguvu msanii huyo aliyewasili nchini Rwanda hivi karibuni kuhani msiba. Kwa mujibu wa chanzo makini, mchumba huyo wa Ndiku alimduwaza Uwoya kwani mbali na kumpokea vizuri alikuwa rafiki ghafla na kuzungumza naye kirafiki, kumuonesha mazingira yote ya kule tofauti na jinsi Uwoya alivyotarajia kwa tabia za wanawake wengine. Yani Uwoya hakutegemea kabisa kama Asma anaweza kumpokea vile. Marehemu Hamad Ndikumana ‘Ndiku’ akiwa na Irene Uwoya.Hakuonesha kinyongo chochote cha kike kama ambavyo wengi wanajua wanawake wanapokutana, hususan kama hawa ambao inafahamika wameshea mwanaume. “Alikuwa mchangamfu kupita maelezo, alimuonesha mitaa na kila walipokuwa wanakwenda walikuwa pamoja utafikiri wamejuana muda mrefu kumbe wala, ghafla wakajikuta wamelikubali tatizo lililotokea na kuona hakuna sababu ya kununiana kwanza ukizingatia wa

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 23.11.2017

Image
                           

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image
             

MAGAZETI YA UDAKU LEO STORI KUBWA HIVI NDIVYO LULU ANAVYOISHI GEREZANI,WINGU JEUSI WEMA NA MAMA YAKE KURUDI CCM

Image
MAGAZETI YA UDAKU LEO STORI KUBWA HIVI NDIVYO LULU ANAVYOISHI GEREZANI,WINGU JEUSI WEMA NA MAMA YAKE KURUDI CCM

NAIBU WAZIRI MASAUNI, KAMISHNA JENERALI WAKAGUA MPAKA WA TANZANIA KENYA ULIOPO WILAYANI TARIME

Image
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) wakiangalia jiwe la mpaka unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda, wilayani Tarime ambapo upande wa pili ni Kaunti ya Migori nchini Kenya. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua mipaka na kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kupitia vipenyo katika mipaka hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea alama ya Mpaka unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda wilayani Tarime.Wengine ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua m

NANDY ATOA YA MOYONI,AFUNGUKA TENA KUHUSU KUPENDA

Image
MWANA-DADA anayefanya vizuri katika Bongo Fleva Faustina Charles ‘Nandy’ ameeleza kuwa hampendi mwanaume kwa sababu ya mkwanja isipokuwa anataka mapenzi ya kweli. Akipiga stori na Risasi Vibes, Nandy ambaye anatamba na ngoma ya Kivuruge alisema anachopenda yeye ni mwanaume mcha Mungu na mchapakazi, haijalishi kama hiyo kazi inamuingizia kipato kikubwa au la. “Fedha siyo kigezo cha mwanaume kuwa na mimi, muhimu mtu awe na hofu ya Mungu, asiwe mtu wa kujibweteka awe anajish-ughulisha kwa kazi yoyote ile, tutapambana wote kutafuta maisha hadi mambo yatakapokuwa vizuri na kujivunia kwa pamoja,”alisema. STORI: MAYASA MARIWATA | GLOBAL PUBLISHERS

Jide, FA Wanaurudisha Muziki wa Bongo Juu

Image
Judith Mbibo Wambura. KAMA ilivyokuwa wakati walipotibuana, kwamba watu wachache walio karibu yao ndiyo waliojua chanzo, ndivyo inavyotokea tena sasa hivi inapofahamika kuwa bifu baina yao limeisha. Nawazungumzia ma-legend wawili katika Bongo Fleva, Judith Mbibo Wambura ambaye wengi tunamfahamu kama Lady Jaydee na Hamis Mwinjuma, hapa akifahamika zaidi kama Mwana FA. Na watu wasingejua kirahisi kama wawili hawa wako kwenye ugomvi kama siyo wote wawili kutangaza kufanya shoo kwa siku moja. Jide alikuwa na onyesho lake la kutimiza miaka 13 katika Bongo Fleva ambayo ilipangwa kufanyika pale Nyumbani Lounge huku Mwana FA, akiitangaza siku hiyo kuwa na onyesho alilolipa jina la The Finest, ambalo lilipangwa kupigwa katika viwanja vya Makumbusho, kule Posta, jijini Dar. Hiyo ilikuwa ni Mei 2013. Mwana FA. Shoo zao hizo zilikuwa zipigwe Mei 31, 2013 lakini ghafla likaibuka tukio kubwa Bongo Fleva, baada ya taarifa kuwa rapa mkali, bingwa wa freestyle Bongo,

RC Makonda Atembelea Ofisi za Clouds Media Group Kutoa Pole

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,  Paul Makonda (wa pili kulia),  akinena jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga (kushoto). MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es Salaam mapema leo ametembelea Ofisi za Clouds Media Group kutoa pole ikiwa ni siku moja baada ya ofisi hizo kukumbwa na janga la moto uliotokea hapo jana majira ya saa nne asubuhi. Makonda akiongea na maofisa wa vikosi vya usalama. Viongozi wengine wa serikali waliofika ofisini hapo ni Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, Ally Hapi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta. Hata hivyo, tayari matangazo ya vituo vya Clouds FM na Clouds TV yamerejea hewani baada ya kupotea siku nzima  jana kutokana na hitilafu ya iliyosababishwa na moto huo ambao chanzo chake hadi sasa hakijajulikana.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMJULIA HALI MZEE ABDULRAZACK MUSSA SIMAI ‘KWACHA’ ALIYELAZWA MOI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo alimtembelea na kumjulia hali Mzee Abdulrazack Mussa Simai ‘Kwacha’ ambaye amelazwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI).Mzee Abdulrazack Mussa Simai ‘Kwacha’ ni Mzee wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia alishawahi shika nafasi mbali mbali za Uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Post Views: 50

ENGO LA CLOUDS MEDIA GROUP LAUNGUA MOTO

Image
Mafundi umeme na Zimamoto wakiingia kupitia dirishani katika jengo la Clouds Media Group kuzima moto uliounguza baadhi ya ofisi leo jijini Dar es Salaam. …Juhudi za kuingia ndani zikiendelea. Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (wa pili kulia, T-shirt ya bluu) akiwa na askari, wakiangalia juhudi za kuuzima moto uliotokea. …Akiongea na polisi. Wafanyakazi wa Clouds na wananchi wakiwa nje ya jengo lililoshika moto. Muonekano wa Jengo la Clouds Media Group.   Magari ya Zimamoto yaliyofika kupambana na moto huo. SEHEMU  ya jengo la kituo cha Clouds Media Group lililoko Mikocheni jijini Dar es Salaam limeungua moto leo ambapo Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo hicho, Ruge Mutahaba, amesema moto huo ulitokea bila ya mtu yeyote kuwa na taarifa nao ambapo ulianzia katika studio ndogo ya kurekodia. Aliongeza kwamba kituo hicho si mara ya kwanza kupatwa majanga ya moto ambapo mara ya kwanza walipokuwa katika jengo la Kitegauchumi eneo la

Rais Magufuli awaonya Masha na Msando

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli amewaonya wanachama wapya ambao wamehamia ndani ya chama hicho leo kwenye mkutano mkuu wa NEC unaoendelea Ikulu jijini Dar es salaam. Wanachama hao ambao wamehamia na kutangazwa leo ni Mwanasheria Alberto Msando aliyekuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo, Mbunge wa zamani wa Nyamagana Laurent Masha aliyekuwa mwanachama wa Chadema pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema taifa Patrobas Katambi. Wengine ni Profesa Kitila Mkumbo ambaye naye alikuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo pamoja na Sophia Simba ambaye ameomba kurejeshewa uanachama baada ya kufukuzwa kwa muda Akiongea baada ya kuwapokea wanachama hao Rais Magufuli amesema, “Nawaomba msije mkabadilika tena, mmekuja huku na wanachama wamewakubali msirudi tena kule, hiki ni chama cha wote hata watoto watazaliwa watakikuta na watajiunga kwasababu kina misingi imara, kwahiyo msije huku kujaribu”. Rais Magufuli amemaliza kwa kuwapa ruhusa ya kugo

Profesa Kitila, Katambi, Msando waingia CCM

Image
Dar es salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo ametangazwa rasmi leo Jumanne mbele ya mkutano wa NEC, CCM unaoendelea Ikulu jijini Dar es salaam. Mbali na Profesa Kitila ambaye alikuwa kada wa ACT, pia kuna Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Kitambi ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha, Lawrence Masha, Samson Mwigamba na Albert Msando. Akizungumza mbele ya mkutano huo, Profesa Kitila amesema: "Nguvu ya CCM zipo tano, moja ni kwamba ni chama cha watu, ni chama pekee chenye nguvu siyo chama kuogopa watu, tulijaribu huko tulipokuwa lakini yalishindwa." Kwa upande wake, Masha amesema alipoamua kuondoka, baba yake alisikitishwa na uamuzi huo lakini baada ya kutafakari ameamua kurejea nyumbani. Amesema yeye ni mwanaCCM na kijana alilelewa ndani ya chama hicho. "Mwenyekiti wewe ni mfugaji, ng'ombe akiingia zizini amekatwa mkia unamwangalia mara mbili mbili, mimi sijakatwa mkia ni mwaminifu, ukinihitaji nitumie, kudumu Chama cha Mapind