MCHUMBA WA NDIKUMANA AMDUWAZA IRENE UWOYA RWANDA

Yani Uwoya hakutegemea kabisa kama Asma anaweza kumpokea vile. Marehemu Hamad Ndikumana ‘Ndiku’ akiwa na Irene Uwoya.Hakuonesha kinyongo chochote cha kike kama ambavyo wengi wanajua wanawake wanapokutana, hususan kama hawa ambao inafahamika wameshea mwanaume. “Alikuwa mchangamfu kupita maelezo, alimuonesha mitaa na kila walipokuwa wanakwenda walikuwa pamoja utafikiri wamejuana muda mrefu kumbe wala, ghafla wakajikuta wamelikubali tatizo lililotokea na kuona hakuna sababu ya kununiana kwanza ukizingatia wameshajua chanzo cha kifo cha Ndiku ni wanasoka wenzake,” kilisema chanzo hicho.
Taarifa zinaeleza kuwa, familia ipo katika hatua za kisheria kuwashughulikia wote wanaotajwa kuhusika na kifo cha Ndiku kinachosadikika kimetokana na kulishwa sumu Akizingumza na Amani, Uwoya alisema anamshukuru Mungu kupokelewa na Asma jambo ambalo kidogo lilimfanya aduwae kwani hakutarajia kukutana na mwanamke ambaye alikuwa mchumba wa Ndiku na kumjali kiasi hicho. Ndikumana alikutwa na umauti Novemba 14, mwaka huu usiku saa chache baada ya kutoka kwenye mazoezi ya timu yake ya Rayon Sports, timu ambayo alikuwa akiitumikia kama kocha msaidizi.

Comments
Post a Comment