Miaka 20 Tangu Princess Diana Azikwe, Dunia Bado Inamkumbuka
Princess Diana enzi za uhai wake.
Siku ya mazishi ya Princess Diana.
Siku ya mazishi ya Princess Diana.
Mahali alipozikwa.
Jeneza lenye mwili wake.
Septemba 6, 1997 ni siku ambayo haitasahaulika, pale mkwe wa malkia Elizabeth, Princess Diana alipozikwa jijini London. Miaka 20 imepita lakini bado kila inapofika siku hii, Waingereza hukumbuka kifo chake kwa kuzuru kwenye kaburi lake, kuweka maua na kuwasha mishumaa.
Princess Diana ambaye jina lake halisi alikuwa akiitwa Diana Frances Spencer, alikuwa mke wa mtoto mkubwa wa Malkia Elizabeth, Prince Charles na kabla ya kufikwa na umauti, wawili hao waliofunga ndoa iliyoutikisa ulimwengu Julai 29, 1981, walibahatika kupata watoto wawili, William na Harry.
Kifo chake kilisababishwa na ajali mbaya iliyotokea jijini Paris, Ufaransa kwenye daraja la chini la Pont de l’Alma ambapo mwanamama huyo na watu aliokuwa nao ndani ya gari, akiwemo Dodi Fayed na dereva wao, Henri Paul walipoteza maisha huku mtu mmoja tu, Trevor Rees-Jones akinusurika kwenye ajali hiyo.
Mazishi yake, yalirushwa na kituo cha runinga cha nchini humo na kutazamwa na zaidi ya watu milioni 32.1 nchini humo, achilia mbali mamilioni ya watu kutoka sehemu nyingine duniani waliokuwa wakifuatilia mazishi yake, na kuvunja rekodi kwa kuwa tukio lililotazamwa zaidi kwenye runinga kwa kipindi hicho.
Comments
Post a Comment