Matukio yaliyojiri ikiwa ni pamoja na babu abebwa mgongoni kwenda kupiga kura kenya
Leo tarehe 26 Oktoba, 2017 Taifa la Kenya limefanya uchaguzi wa Rais, ambapo kiongozi wa vyama vya upinzani nchini humo, Raila Odinga amesusia uchaguzi huo. Rais Uhuru Kenyatta akipiga kura mapema leo jijini Nairobi katika Shule ya Msingi Mutomo Hadi sasa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaeleza kuwa mtu mmoja amshauawa kwenye vurugu zilizotokea mjini Kisumu na wengine 20 wakijeruhiwa kwenye vurugu zilizoongozwa na wafuasi wa vyama vya upinzani. Misururu mirefu ya wapiga kura, katika shule ya msingi ya Kayole One, Embakasi Central jijini Nairobi Wafuasi wa upinzani wakiweka magogo katikati ya barabara mjini Migori Jaji Mkuu nchini Kenya, George Maraga akipiga kura mapema leo katika shule ya msingi ya Bosose, Nyamira Rais wa zamani wa Kenya, Mwai Kibaki akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Munaini, Othaya. Mpiga kura akiwa na Babu yake mgongoni akimpeleka kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Kaare Kaunti ya Thar...