Posts

Njia 10 Za Kupunguza Magonjwa Ya Mlipuko Wa Kuku

Image
Mlipuko wa magonjwa ni moja ya sababu za hasara kubwa kwa wafugaji na vifo vinavyotokea kwa wakati mmoja. Pindi mfugaji anapokumbwa na janga la vifo vya ndege, kabla ya kufikia mwisho wa mzunguko wa uzalishaji hivyo basi asitarajie kupata faida nzuri mara baada ya mauzo. Hasara itokanayo na vifo inaweza kuepukika au kupunguzwa na kutokea kwa kiasi kidogo. Hili linawezekana, ifuatayo ni namna ya kufanikisha hilo;- 1. Osha vyombo vya maji kila wakati na mwaga maji yaliyobaki. Hakikisha unamwaga maji yaliyosalia mbali na kuosha chombo na sabuni kila siku, weka maji safi yasiyo na dawa na wala usitumie maji ya mto au yale usiyoyajua chanzo chake. Kama utaweka maji dawa basi tumia ‘vitamini’ muhimu kama ‘vitalyte’ ambazo zinasaidia kuua vijidudu. 2. Wape maji kabla ya chakula. Ndege wapo tofauti na binadamu au wanyama wengine. Hakikisha unawapa maji kabla ya chakula hasa kama unatumia maranda, hii ni kuhakikisha hawakanyagani wanapogombania chakula sehemu moja. 3

WATANZANIA WATIKISA TENA TUZO ZA AFRIMMA 2017,DARASSA NA DIAMOND NAO NDANI

Image
Majina ya wasanii wanaowania tuzo za mwaka huu za Afrimma yametajwa. Diamond ameongoza kwenye orodha hiyo kwa kutajwa kwenye vipengele vitano. Rayvanny ametajwa katika vipengele vitatu wakati Darassa na Tuddy Thomas wakitajwa kwenye vipengele viwili. Wengine walitajwa ni Alikiba, Lady Jaydee, Vanessa Mdee, Yamoto Band, Dj D-Ommy, Dayna Nyange na Mose Iyobo. Tuzo hizo zitafanyika October 8 ya mwaka huu mjini Texas. Hii ni orodha kamili ya vipengele hivyo. Best Male West Africa Wizkid – Nigeria Falz – Nigeria Serge Beynaud – Ivory Coast Mr Eazi – Nigeria Toofan – Togo Moh Dediouf – Senegal Davido – Nigeria Stonebwoy – Ghana Tekno – Nigeria Kedejevara DJ (Ivory Coast) Best Female West Africa Tiwa Savage – Nigeria Yemi Alade – Nigeria Efya – Ghana Adiouza – Senegal Becca – Ghana Josey – Ivory Coast Mz Vee – Ghana Simi – Nigeria Best Male East Africa Eddy Kenzo – Uganda Diamond Platnumz – Tanzania Jacky Gosee – Et

CHESTER BENNINGTON AFARIKI DUNIA KWA KUJIUA

Image
Msanii wa muziki kutoka Marekani, Chester Bennington amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 41. Chester alikutwa amefariki dunia akidaiwa kujinyonga mwenyewe nyumbani kwake Palos Verdes Estates mjini Los Angles Muimbaji huyo wa Linkin Park pia alikuwa na urafiki wa ukaribu na Chris Cornell amabye na yeye alijiuwa mwezi Mei mwaka huu kwa kuzidisha madawa. Joe Hahn DJ wa kundi la Linkin Park akielekea msibanit Chanzo cha kifo cha Chester kimeelezwa kuwa marehemu alikuwa akinyanyaswa na mwanaume mmoja hali iliyokuwa ikimpelekea kujiona kama mtoto. Kifo hiko kimetokea wakati kundi la Linkin Park, likijiandaa kwenda kufanya photoshoot mjini Hollywood kwa ajili ya wimbo wao mpya. Marehemu ameacha watoto sita aliokuwa amezaa na wanawake wawili tofauti, pia inaelezwa msanii huyo alikuwa akitumia madawa ya kulevya pamoja na pombe kali.

JPM amkaanga mbunge wa upinzani Kigoma

Image
Dar/Kigoma. Rais John Magufuli ‘amemkaanga’ mbunge wa upinzani wa Jimbo la Buyungu, Kigoma huku akisema kuwa wananchi wa eneo hilo wanateseka kutokana na makosa ambayo waliyafanya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015. Akihutubia wananchi wa mkoa huo jana, wakati wa  ziara yake ya kikazi katika Ukanda wa Magharibi, Rais Magufuli alisema maendeleo yanaletwa na chama tawala (CCM) na kwamba wananchi walikosea kuchagua mbunge wa upinzani. Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mbunge wa Jimbo la Buyungu, Kasuku Bilago Samson (Chadema) kuelezea kuwa eneo hilo lina uhaba  mkubwa  wa maji. “Kabla sijazungumza chochote naomba mbunge wa hapa awasalimu,” alisema Rais Magufuli ambaye alikuwa wilayani Kakonko kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kibondo-Nyakanazi. Mara baada ya kusimama, mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kueleza kero ya maji kwenye jimbo lake. “Naomba niseme tunalo tatizo la maji katika Jimbo la Buyungu hususan Kakonko mjini,” alisema. Licha ya

Hatimaye Millen Magese Apata Mtoto Baada ya Upasuaji Mara 13

Image
Happiness Millen Magese akiwa amekumbatia kichanga chake.   Miss Tanzania mwaka 2001, Happiness Millen Magese ambaye anafanya kazi ya uwanamitindo amebahatika kupata mtoto wake wa kwanza Julai 13 mwaka huu.   Millen amewahi kumwaga machozi hadharani akielezea mateso yanayotokana na tatizo aliloligundua kwake toka akiwa na umri wa miaka 13 la mirija yake kuziba mwaka 2007.   Kuna kipindi alikata tamaa mpaka akajiandaa kuondoa kizazi na hapo ni baada ya kufanyiwa  oparesheni zisizopungua 13 ambapo pamoja na hayo, aliambiwa moja ya tiba ya tatizo hilo liitwalo ‘Endometriosis’ kwa kizungu, ni kuzaa.   Baada ya mateso yote usiku na mchana pamoja na kutumia gharama kubwa kwenye matibabu South Africa na Marekani, hatimaye amefanikiwa kupata mtoto wa kiume July 13, 2017 Hospitalini New York Marekani na anaitwa Prince Kairo Michael Magese.   Millen ameeleza namna alivyoteseka huku akimshukuru Mungu kwa muujiza huo wa aina yake wa kumpa mtoto ilihali ali

Picha za Mazishi ya Mama Zari, Uganda

Image
Mama Diamond (wa tatu kushoto) akiwa na mkwe wake, Zari (kushoto kwake). Waombolezaji wakiswali msibani. Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ , Halima Hassan aliyefariki dunia jana asubuhi, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa hospitali amezikwa leo Julai 21, 2017 katika Kitongoji cha Munyonyo, Kampala. Kina mama wakiomboleza. Alhamisi iliyopita Gazeti la Amani liliripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga .   Hali ilivyokuwa nyumbani kwa mama Zari. Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka. Kaburi ambamo mwili wa marehemu ut

ALICHOANDIKA DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU KIFO CHA MAMA YAKE ZARI THE BOSS LADY

Image
Msanii wa Bongo Fleva  Diamond Platnumz  ametumia IG Yake kuweka ujumbe huu kuhusu Kifo cha mama yake  ZARI   ambaye ni mama watoto wawili wa Diamond Platnumz. Diamond PlatnumzMwenyez Mungu ailaze Roho yako Mahali Pema Peponi Amini. Mama mzazi wa Zari amefariki  Asubuhi ya July 20 2017.

Tundu Lissu agoma Kupimwa mkojo

Image
Tundu Lissu(Mb) amekataa kupimwa mkojo baada ya kufikishwa kwa Mkemia   Asema kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi Taarifa za awali ziliarifu kuwa, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa Kituo cha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo. Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika. Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana. "Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema. Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa k

Siku ya Mashujaa Kufanyika nchini kote kwa huduma za kiafya

Image
Meja Jenerali Simon Mumwi ambaye ni Mkuu wa Mipango na Maendeleo wa JWTZ akizungumza na Waandishi wa habari. JESHI la Ulinzi laWananchi wa Tanzania leo limetoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika Julai 25 mwaka huu. Maadhimisho hayo kama ilivyo desturi ya nchi hutoa fursa ya kuwakumbuka mashujaa wa Tanzania waliotoa maisha yao kwa ajili ya kupigania nchi yetu.  

MH. RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI KIGOMA AKITOKEA KAGERA, AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUHUTUBIA WANANCHI KWENYE MIKUTANO YA HADHARA AKIWA NJIANI

Image
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kakonko kabla ya kuzindua Ujenzi wa barabara ya Kibondo -Nyakanazi yenye urefu wa kilometa 54,katika mkoa wa Kigoma Rais yupo mkoani Kigoma kwa Ziara ya siku Tatu Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikazia jambo wakati akiwahutubia wananchi wa Kakonko Kibondo katika mkoa wa Kigoma Rais yupo mkoani Kigoma kwa Ziara ya siku Tatu Wananchi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakisikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Kibondo -Nyakanazi yenye urefu wa kilometa 54,Sherehe zilizo fanyika katika uwanja wa Standi Mpya ya Mabasi Kakonko katika mkoa wa Kigoma Rais yupo mkoani Kigoma kwa Ziara ya siku Tatu Baaadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa na wananchi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakisikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani