Picha za Mazishi ya Mama Zari, Uganda
Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Halima Hassan aliyefariki dunia jana asubuhi, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa hospitali amezikwa leo Julai 21, 2017 katika Kitongoji cha Munyonyo, Kampala.
Alhamisi iliyopita Gazeti la Amani liliripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga.
Hali ilivyokuwa nyumbani kwa mama Zari.
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.
Kifo cha mama Zari ambaye alizaliwa Mei 15, 1959, kimekuja ikiwa ni takribani miezi miwili tu tangu mkwe wake, Ivan Semwanga, aliyeaga dunia Mei 25 mwaka huu huko Steve Biko Academic Hospital nchini Pretoria, Afrika Kusini.
Waombolezaji wamefurika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mama huyo ambaye amekuwa maarufu Afrika Mashariki na Kati kupitia kwa mwanaye Zari.
Mmoja wa waombolezaji akigonga pilau.
Pumzika kwa Amani, Halima Hassan.
Comments
Post a Comment