Hatimaye Millen Magese Apata Mtoto Baada ya Upasuaji Mara 13
Miss Tanzania mwaka 2001, Happiness Millen Magese ambaye anafanya kazi ya uwanamitindo amebahatika kupata mtoto wake wa kwanza Julai 13 mwaka huu.
Millen amewahi kumwaga machozi
hadharani akielezea mateso yanayotokana na tatizo aliloligundua kwake
toka akiwa na umri wa miaka 13 la mirija yake kuziba mwaka 2007.
Kuna kipindi alikata tamaa mpaka
akajiandaa kuondoa kizazi na hapo ni baada ya kufanyiwa oparesheni
zisizopungua 13 ambapo pamoja na hayo, aliambiwa moja ya tiba ya tatizo
hilo liitwalo ‘Endometriosis’ kwa kizungu, ni kuzaa.
Baada ya mateso yote usiku na mchana
pamoja na kutumia gharama kubwa kwenye matibabu South Africa na
Marekani, hatimaye amefanikiwa kupata mtoto wa kiume July 13, 2017 Hospitalini New York Marekani na anaitwa Prince Kairo Michael Magese.
Millen ameeleza namna alivyoteseka
huku akimshukuru Mungu kwa muujiza huo wa aina yake wa kumpa mtoto
ilihali alikuwa amekwisha kata tamaa.
Haya ndiyo ameyaandika Millen;
Comments
Post a Comment