Posts

Mama Mzazi wa Zari, Afariki Dunia!

Image
Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ , Halima Hassan amefariki dunia asubuhi hii, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa hospitali. Zari ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platinums , amethibitisha kifo cha mama yake kupitia ukurasa wake wa Instagram , na haya ndiyo ameyaandika;   Alhamisi iliyopita Gazeti la Amani liliripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga . Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka. Kifo cha mama Zari ambaye alizaliwa Mei 15, 1959, kimekuja ikiwa ni takribani miezi miwili tu tangu mkwe wake, Ivan Semwanga , aliyeaga dunia M

TUNDU LISSU AKAMATWA AKIWA UWANJA WA NDEGE AKIJIANDAA KWENDA RWANDA

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa leo, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martn Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi.Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo. Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kwamba mwanasheria huyo amekamatwa jioni hii. Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kwamba ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Mkuu wa Usalama Barabarani Yamkuta, Afutwa Kazi

Image
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni (kushoto) akiwauliza maswali abiria wa basi la Safari Express lifanyalo safari zake Dar es Salaam – Arusha, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, Pwani. NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo. Masauni akiwa ameambatana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu, alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo, kwa ajili ya kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana. Masauni (kushoto) akimuuliza maswali Dereva wa basi la Safari Express. “Mwaka jana nilipofanya zia

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA MKOA WA SONGWE

Image
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kulia ni mkewe Mary. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songwe, Elias Nawela baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimia wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) alipozungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 20117. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini wa mkoa wa Songwe kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 2017. Kushoto ni Mkewe Mary na Kat

BREAKING NEWS: SIMBA YAMSAJILI KIPA BORA WA COSAFA

Image
Saidi Mohammed. Katika kuendelea kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wa 2017/18, Klabu ya Simba imeendelea kufanya kweli kwa kusajiri wachezaji wanaoweza kuleta ushindani katika kikosi cha kwanza. Habari ni kuwa Simba imemsajili kipa Saidi Mohammed kwa kandarasi ya miaka miwili. Said alikuwa kipa wa Mtibwa Sugar na kwa sasa yupo katika kikosi cha Taifa Stars, pia ndiye aliyekuwa Kipa Bora wa Michuano ya Cosafa iliyofanyika nchini Afrika Kusini, mwaka huu.

Waliomvua mwanamke nguo wahukumiwa kifo Kenya

Image
Wanaume watatu ambao walimvamia, wakamvua nguo na kumuibia mwanamke ndani ya basi la abiria mjini Nairobi, katika kisa ambacho kilirekodiwa na kusambazwa pakubwa katika mitandao ya kijamii miaka mitatu iliyopita, wamehukumiwa kifo kwenye mahakama moja mjini Nairobi. Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa baada ya watatu hao kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia nguvu. Kifungo kingine cha miaka 25 kilitolewa kwa kumvua nguo mwanamke huyo, Jilo Kadida. Kifungo cha miaka 25 hata hivyo kilitupiliwa mbali kwa wanaume hao walikuwa tayari wamehukumiwa kifo. Wanaume hao watatu ni dereva wa basi Nicholas Mwangi, na makondakta wake Meshack Mwangi na Edward Ndung'u. Hakimu wa Nairobi Francis Andayi, alisema kuwa kitendo hicho kilikuwa kibaya walichoonekana kufurahia, kwa sababu walikuwa wakishangilia huku wakimvua nguo mwanamke huyo. Muathiriwa aliiambia mahakama kuwa kulikuwa na karibu wanaume saba ndani ya basi wakati huo, ambao walitaka kumbaka lakini akadanganya kuwa a

Njemba Amchezea Sharubu JPM, Adaiwa Kumweka Kinyumba Denti Form 2

Image
Denti huyo baada ya kunaswa chumbani. NJEMBA aliyetajwa kwa jina moja la Sadick anadaiwa kumweka kinyumba denti wa kidato cha pili (jina la mwanafunzi na shule vinahifadhiwa), jambo lililotafsiriwa kuwa ni kuwachezea sharubu viongozi wa ngazi ya juu kabisa nchini akiwemo Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ ambaye ni hivi karibuni tu ameonya na kutaka zichukuliwe hatua kali kwa wanaojihusisha na mchezo wa mapenzi na wanafunzi. ONYO LA RAIS Rais Magufuli alitoa onyo hilo alipokuwa akizindua Barabara ya Bagamoyo-Msata, mkoani Pwani, mwezi uliopita na kuongeza kwamba serikali yake haitagharamia mwanafunzi aliyepata mimba shuleni.   Mwenyekiti wa Mtaa, Adil Omar akiwa na denti. ONYO LA WAZIRI MKUU Mbali na Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, akikabidhi vifaa vya maabara kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum hivi karibuni Lugalo jijini Dar alishindilia msumari kwenye onyo hilo, akisema kuwa, yeye pamoja na rais watalala mbele na mtu

MSEMAJI WA SIMBA HAJI MANARA AFUTIWA ADHABU YA TFF

Image
Haji Manara. KAMATI ya Nidhamu ya  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) , chini ya mwenyekiti wake, Tarimba Abass, leo Jumatatu imefikia uamuzi wa kumfutia adhabu  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba ,  Haji Manara. Kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya  Manara  kuomba kupitiwa upya adhabu aliyopewa hapo awali ya kufungiwa kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 12 na kulipa faini ya Sh milioni 9. Kutokana na kufutwa kwa adhabu hiyo, Manara kuanzia leo atakuwa huru kuendelea kufanya majukumu yake ya soka ndani ya Simba. Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas akizungumza na wanahabari leo mchana ikiwa ni maamuzi waliyoyafikia ya kamati ya nidhamu na kuwafungulia baadhi ya wanafamilia wa mpira waliokuwa wamefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi. Mbali na Manara, kamati hiyo pia imewafutia adhabu Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Rukwa, Blassy Kiondo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Rukwa, James Mak

Rais Magufuli kuzindua miradi tisa ya barabara na uwanja wa ndege.

Image

DAR: Watuhumiwa 250 Mbaroni, Wamo wa Madawa ya Kulevya

Image
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DCP, Lucas Mkondya akiwaonyesha wanahabari bangi zilizokamatwa na jeshi hilo. JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema kuwa limefanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa 250 kwa makosa mbalimbali ya kihalifu yakiwemo ya kukutwa na madawa ya kulevya. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Lucas Mkondya ameeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kupitia msako mkali kuanzia Julai 16, hadi leo Julai 17 ambapo watuhumiwa hao walikamatwa. Mkondya amesema, miongoni mwa makosa waliyokamatwa nayo watuhumiwa hao ni pamoja na kupatikana na madaya ya kulevya, unyang’anyi wa kutumia silaha, utapeli na kucheza kamari. Aliongeza kuwa upelelezi wa makosa hayo ukikamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria. NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

JK amfuta Machozi Mwakyembe

Image
RAIS Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amefika Nyumbani kwa Dk Harrison Mwakyembe kumfuta Machozi kutokana na Msiba wa Mke wake Linah Mwakyembe. Kikwete alifika Msibani hapo saa sita  mchana  "Mwakyembe ni rafiki yangu wa siku nyingi, hata wakati mama anaumwa aliniambia na nilienda kumjulia hali alipokuwa Muhimbili, nimtake awe mvumilivu tunajua ana majonzi msiba huu ni wetu sote," amesema. Wengine waliofika kumfariji Dk Mwakyembe ni Jaji Mstaafu Damian Lubuva, ambaye pia alimjulia hali Linah wakati akiwa hospitali. "Mwezi uliopita nilienda Aga Khan kumuona mgonjwa mwingine lakini nikakutana na Mwakyembe, akaniambia mkewe amelazwa nikaona si vibaya kwenda kumjulia hali na alikuwa anaonyesha matumaini," amesema. Wengine waliofika kumfariji Dk Mwakyembe ni Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda; Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji; Waziri wa Ulinzi, Dk Hussein Mwinyi; Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga na viongozi wengine

STAA DIAMOND PLATNUMZ,BABU TALE NA MKUBWA FELLA WAKIWA MSIBANI KWA WAZIRI MWAKYEMBE

Image
Mwimbaji wa Bongofleva  Diamond Platnumz,   Mameneja wake  Said Fella  na  Babu Tale ni miongoni mwa mastaa wa Bongo waliofika nyumbani kwa Waziri wa Habari  Dr.  Mwakyembe  kutoa pole kufuatia kifo cha Mke wake  Linah George.

PICHA: KELVIN YONDANI APATA JIKO RASMI

Image
TAARIFA njema ikufikie popote ulipo kuhusu beki kisiki wa  Yanga, Kelvin Patrick Yondani  ambaye ameamua kuachana na ukapera. Mkali huyo alianza kwa  Send Off  kisha akamalizia mambo na mzazi mwenzake ambaye ameishi naye miaka mingi. Yondani anaingia kwenye orodha moja na wanasoka kama Emmanuel Okwi, Ibrahim Ajib, Mwinyi Kazimoto ambao ni wanacheza Ligi Kuu Tanzania Bara. Hongera Yondani kwa kuamua kufanya kweli.

Wanafunzi 10 wafutiwa matokeo ( Kidato cha sita) kwa Udanganyifu

Image
Wanafunzi 10 wamefutiwa matokeo yao baada ya kufanya udanganyifu kwenye mtihani wa Kidato cha sita  Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Necta Dk Charles Msonde  amesema  kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.  Pamoja na hao kumi, matokeo ya watahiniwa wengine 15 yalizuiliwa kwa kuwa hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo.  Watahiniwa hao walishindwa kufanya mitihani kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya baadhi ya mitihani hiyo. ‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama wa watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde. Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018. Wanafunzi 10 wamefutiwa matokeo yao baada ya kufanya udanganyifu kwenye mtihani wa Kidato cha sita  Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani

Simba Kuna Makinikia - Wazee Simba

Image
Wazee wa Klabu ya Simba wametuhumu uongozi wa Klabu hiyo kikihuumu Klabu hicho na kwamba wamemtaka rais John Magufuli kuingilia kati hujma hizo. Wakizungumza na Waandishi wa habari leo wazee hao wameeleza kuwa hujuma hizo zinatokana na Uchu wa madaraka na tamaa ya fedha kwa viongozi hao. Felex Makuwa Mratibu wa wazee hao ameeleza kuwa Serikali kupitia Mamlaka zake iwakamate wahusika na Iwachukulie hatua  

BREAKING NEWS : ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA ACSEE 2017

Image
  Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokoe ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita. Bonyeza HAPA kufatilia matokea ya shule zote Tanzania. BOFYA HAPA KUYAONA

Profesa Jay Afunguka Wema Kukacha Harusi Yake

Image
Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’akifanya yake na mke wake Grace Mgonjo baada ya kufunga ndoa. BAADA ya Jumamosi iliyopita Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kufunga ndoa na mchumba’ke wa kitambo, Grace Mgonjo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo Posta jijini Dar na sherehe kufanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, ameibuka na kufunguka suala la Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu kuikacha harusi yake. Staa wa Bongo, Wema Sepetu. Taarifa za awali kutoka kwa chanzo makini zilieleza kuwa, Profesa Jay na Wema ambaye alihamia Chadema miezi kadhaa iliyopita wana bifu kali japokuwa haijulikani chanzo ni nini, ndiyo maana mwanadada huyo hakuhudhuria kwenye harusi hiyo. “Unajua Wema na Jay hawana uhusiano mzuri tangu ahamie kwenye chama hicho yaani wana bifu ndiyo sababu hata Wema hakuhudhuria kwenye sherehe ya harusi ya Jay

CHAI, KARANGA NA MTINDI KWA HESHIMA YA NDOA!

Image
WAPENDWA wasomaji wangu, bila shaka mko poa mnaendelea vyema na majukumu yenu kama kawaida. Leo kwenye safu hii nitazungumzia umuhimu wa chai kwa mwanamke ili kudumisha uhusiano wako na ndoa kwa ujumla. Nafanya hivi kwa kuwa, wengi wamejikuta wakipoteza ndoa zao kwa kupoteza mvuto na kupuuzia mambo madogomadogo. Sasa leo nakupa tipu juu ya namna chai ya rangi, maziwa ya mtindi, karanga na supu ya pweza vinavyoweza kuinogesha ndoa yako hasa katika eneo la faragha. Mwanamke fanya hivi; kunywa chai kutwa mara tatu. Kumbuka kazi ya chai ni kukupatia joto mwilini. Ukijua kuwa muda wa kukutana na mwenza wako faragha unakaribia, pata kikombe chako cha chai ya moto kisha jirushe uwanjani uone mechi itakavyokuwa bomba. Chai hiyo itakupa nguvu na hivyo kuweza kumudu mikikimikiki ya mwenza wako. Na nikuambie tu kwamba, ukiwa umepata chai yako hiyo, neno; ‘nimechoka mume wangu’ haliwezi kuwepo, labda achoke yeye. Unaachaje sasa kuitumia chai ambayo hata haina kazi kuiandaa

Diwani Chadema Mbaroni kwa Tuhuma za Rushwa

Image
Diwani Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa  Sh.5,000,000/=. kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa  TAKUKURU wilaya ya  Kinondoni Teddy Mjangira, amesema kuwa Watuhumiwa walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha toka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa alitakiwa  na watuhumiwa kuwapa  rushwa ya Sh.10,000,000/= Inadawaiwa Watuhumiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango miji  inashughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo. Uchunguzi wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa kinyume na kifungu namba 15 ch

Majaliwa Amkalia kooni Mkurugenzi Lindi

Image
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Lindi, Samuel Warioba Gunzar leo alijikuta katika wakati mgumu mbele ya waziri mkuu wa Jamuhuri ya Tanzania, Kassim Majaliwa baada ya kukutana na maswali mzito mfululizo kutoka kwa kiongozi huyo wa juu wa nchi.  Hayo yamejiri katika mji mdogo wa Mtama kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa umefurika mamia ya wananchi. Hali ilikuwa mbaya kwa Gunzar kutokana na taarifa iliyotolewa na mbuge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye aliyekueleza waziri mkuu kwamba katika mji huo mdogo in unaokadiriwa kuwa na wakazi takribani 4000 hauna kituo cha afya.  Maelezo ya Nape yalisababisha waziri mkuu amuite mkurugenzi huyo aeleze nikwanini eneo hilo lisiwe na kituo cha afya wakati linaidadi kubwa ya watu. Huku akihoji kwanini imekuwa hivyo wakati kuna madiwani na watendaji katika halmashauri hiyo.  Alisema sera ya afya ipo wazi nasifa za kuwa na zahanati, vituo vya afya na hospitali zinafahamika. "Mkurugenzi  njoo utueleze kwanini hap