CHAI, KARANGA NA MTINDI KWA HESHIMA YA NDOA!

WAPENDWA wasomaji wangu, bila shaka mko poa mnaendelea vyema na majukumu yenu kama kawaida. Leo kwenye safu hii nitazungumzia umuhimu wa chai kwa mwanamke ili kudumisha uhusiano wako na ndoa kwa ujumla. Nafanya hivi kwa kuwa, wengi wamejikuta wakipoteza ndoa zao kwa kupoteza mvuto na kupuuzia mambo madogomadogo.
Sasa leo nakupa tipu juu ya namna chai ya rangi, maziwa ya mtindi, karanga na supu ya pweza vinavyoweza kuinogesha ndoa yako hasa katika eneo la faragha.

Mwanamke fanya hivi; kunywa chai kutwa mara tatu. Kumbuka kazi ya chai ni kukupatia joto mwilini. Ukijua kuwa muda wa kukutana na mwenza wako faragha unakaribia, pata kikombe chako cha chai ya moto kisha jirushe uwanjani uone mechi itakavyokuwa bomba. Chai hiyo itakupa nguvu na hivyo kuweza kumudu mikikimikiki ya mwenza wako.
Na nikuambie tu kwamba, ukiwa umepata chai yako hiyo, neno; ‘nimechoka mume wangu’ haliwezi kuwepo, labda achoke yeye. Unaachaje sasa kuitumia chai ambayo hata haina kazi kuiandaa na si kwa gharama kubwa? Kwa mwanaume; wakati mke anakunywa chai, anaweza kumuandalia supu ya pweza ya moto au karanga na mtindi. Nikuambie tu mkubwa mwenzangu kwamba, vitu hivyo vya asili vina nafasi kubwa katika tendo la ndoa hivyo anza kufanya hivyo ili kuijengea ndoa yako heshima.

Comments

Popular posts from this blog