Wanafunzi 10 wafutiwa matokeo ( Kidato cha sita) kwa Udanganyifu

Wanafunzi 10 wamefutiwa matokeo yao baada ya kufanya udanganyifu kwenye mtihani wa Kidato cha sita

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Necta Dk Charles Msonde  amesema  kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.

 Pamoja na hao kumi, matokeo ya watahiniwa wengine 15 yalizuiliwa kwa kuwa hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo.

 Watahiniwa hao walishindwa kufanya mitihani kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya baadhi ya mitihani hiyo.

‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama wa watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.

Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018.

Comments

Popular posts from this blog