Njemba Amchezea Sharubu JPM, Adaiwa Kumweka Kinyumba Denti Form 2


Denti huyo baada ya kunaswa chumbani.

NJEMBA aliyetajwa kwa jina moja la Sadick anadaiwa kumweka kinyumba denti wa kidato cha pili (jina la mwanafunzi na shule vinahifadhiwa), jambo lililotafsiriwa kuwa ni kuwachezea sharubu viongozi wa ngazi ya juu kabisa nchini akiwemo Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ ambaye ni hivi karibuni tu ameonya
na kutaka zichukuliwe hatua kali kwa wanaojihusisha na mchezo wa mapenzi na wanafunzi.

ONYO LA RAIS
Rais Magufuli alitoa onyo hilo alipokuwa akizindua Barabara ya Bagamoyo-Msata, mkoani Pwani, mwezi uliopita na kuongeza kwamba serikali yake haitagharamia
mwanafunzi aliyepata mimba shuleni.
 
Mwenyekiti wa Mtaa, Adil Omar akiwa na denti.

ONYO LA WAZIRI MKUU
Mbali na Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, akikabidhi vifaa vya maabara kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum hivi karibuni Lugalo jijini Dar alishindilia msumari kwenye onyo hilo, akisema kuwa, yeye pamoja na rais watalala mbele na mtu atakayekaidi agizo hilo.

TUJIUNGE KWENYE TUKIO
Ilikuwa mapema wiki iliyopita ambapo Ijumaa Wikienda lilipokea ‘tipu’ ya kuwepo kwa tukio hilo ambapo denti huyo alinaswa laivu akipika na kupakua nyumbani kwa Sadick ilihali ni muda wa masomo.

Gazeti hili lilifi ka eneo la tukio ambapo denti huyo alinaswa chumbani katika nyumba anayoishi Sadick, Mtaa wa Kiswanya B mjini hapa.
 
…Akiwa kitandani.

Kamanda wa Kikosi cha Kufi chua Maovu (OFM) cha Global Publishers aliyeambatana na wazazi wa denti huyo, Polisi wa Kituo cha Mafi ga na viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Kiswanya walivamia kwenye chumba cha Sadick na kumkuta denti huyo aliyetoroshwa nyumbani kwao kwa siku nne, akiwa amejaa tele akimpikia Sadick chakula cha mchana.

…NA KANGA MOJA
Denti huyo alishuhudiwa akiwa kwenye pilika za kuandaa maakuli hayo akiwa
amejifunga kanga moja tu iliyoishia kifuani! Jamani! Mh! Dunia ina mambo!

Hata hivyo, wakati timu hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Adil Omar ilipovamia nyumbani hapo, denti huyo alikutwa peke yake na alipoulizwa aliko ‘mwenzake’ alisema Sadick alikuwa kazini na kwamba angereja mchana kupata ‘lanchi’.

Rais Magufuli.


Kutokana na wingi wa watu waliofurika kwenye nyumba hiyo, baadhi yao walidaiwa kumtonya Sadick juu ya msala huo hivyo hakurejea na hata alipotafutwa kwenye simu hakupatikana.

MAAGIZO YA POLISI
Kufuatia hali hiyo, polisi walitoa maagizo kwa wapangaji wa nyumbani hiyo, Rehema Mrema na Mwajuma Paul kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa huo mara tu Sadick atakaporejea.

BABA MZAZI ASIMULIA
Akihojiwa na Ijumaa Wikienda eneo hilo la tukio, baba mzazi wa mwanafunzi huyo, Rajab Abdallah, alisimulia:

“Nilikuwa shamba ninalima mpunga ili  ipate fedha ya kumnunulia mwanangu mahitaji muhimu ya shule. Sasa nikiwa huko shambani ndiyo mke wangu akanipigia simu akaniambia mwanangu (anamtaja) hajarudi nyumbani yapata siku tatu na ametafutwa bila mafanikio.
Wakiandikisha maelezo kwa mwenyekiti wa mtaa.

 
 “Ndipo nikaja mjini kumtafuta mwanangu,” alisema mzee huyo na kuongeza:

“Nilipofi ka nyumbani hapa mjini nilipewa taarifa kwamba mke wangu na wanangu wengine walimtafuta mwenzao kila mahali ikiwemo kwa ndugu wote, lakini hakupatikana hivyo nikaamua kutumia mbinu ya kwenda kwa rafiki yake mkubwa kisha nikambana ndipo akanitajia alipo.

“Baada ya kujua alipo, nilikwenda Kituo cha Polisi cha Mafi ga tukapitia kwa mwenyekiti wa mtaa ndiyo tukaja hapa. Wote tumemshuhudia mwanangu akiwa chumbani kwa mwanaume huku nguo za shule na madaftari akiwa navyo kwenye mfuko wa rambo.”

MWANAFUNZI NAYE
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mwanafunzi huyo alikiri kushawishiwa na mwanaume huyo na kwamba ni mpenzi wake wa muda mrefu aliyeahidi kumuoa.

MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA
Kwa upande wake, mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Adil Omar alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake: “Kama ulivyoona muda huu wa shule, mwanafunzi tumemkuta chumbani kwa mwanaume.

“Tulichokifanya kama viongozi wa mtaa, tumefunga mlango na funguo tunazo sambamba na kuweka ushahidi wa maandishi ambapo wapangaji Mwajuma Poul na Rehama Mrema ni mashahidi na Mzee Rajab tumemkabidhi mtoto wake aondoke naye,” alisema mwenyekiti huyo.

Baada ya kutoka hapo, Ijumaa Wikienda lilitinga katika shule anayosoma mwanafunzi huyo na kuzungumza na mkuu wa shule hiyo juu ya maendeleo ya denti huyo na kama ana taarifa za mwanafunzi wake kuwekwa kinyumba na mwanaume ambapo aligoma kutoa ushirikiano.

“Siwezi kukubali wala kukataa kama ni mwanafunzi wetu kwani kidato cha  ili kuna wanafunzi zaidi ya 200 na tumewagawanya katika madarasa manne yaani A,B,C na D.”

SADICK ASAKWA

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, polisi hao walikuwa wakiendelea kumsaka Sadick ili sheria ichukue mkondo wake.

Comments

Popular posts from this blog