MSEMAJI WA SIMBA HAJI MANARA AFUTIWA ADHABU YA TFF
Haji Manara. KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) , chini ya mwenyekiti wake, Tarimba Abass, leo Jumatatu imefikia uamuzi wa kumfutia adhabu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba , Haji Manara. Kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya Manara kuomba kupitiwa upya adhabu aliyopewa hapo awali ya kufungiwa kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 12 na kulipa faini ya Sh milioni 9. Kutokana na kufutwa kwa adhabu hiyo, Manara kuanzia leo atakuwa huru kuendelea kufanya majukumu yake ya soka ndani ya Simba. Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas akizungumza na wanahabari leo mchana ikiwa ni maamuzi waliyoyafikia ya kamati ya nidhamu na kuwafungulia baadhi ya wanafamilia wa mpira waliokuwa wamefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi. Mbali na Manara, kamati hiyo pia imewafutia adhabu Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Rukwa, Blassy Kiondo, Mwenyekiti wa Kamati ...