Posts

HII NDIO KAULI YA JUX BAADA YA KUMALIZA MASOMO YAKE

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Jux amesema haikuwa kazi rahisi hadi yeye kumaliza masomo yake ya elimu ya juu nchini China. Muimbaji huyo amesema kuwa katika miaka mitano aliyosoma kuna wakati alikuwa anakosa mitihani kwa sababu ya show lakini anaishukuru familia yake kwa kuwa karibu na yeye. “It’s not easy at all lakini nashukuru sana rafiki zangu ambao wamenizunguka, familia yangu ni watu ambao walikuwa wananipa sana moyo, walinieleza kila kitu kinawezekana usikate tamaa, naweza nikamaliza nikafanya vitu vyote, naweza nikafanya biashara, muziki na kusoma pia,” Jux ameiambia XXL ya Clouds FM. “Namshukuru Mungu nimemaliza leo, so kila kitu kinawezekana naweza nikakuambia muda wako tu unavyoupanga na changamoto zipo nyingi, kushindwa sio tatizo ila hutakiwa kuacha. Kuna mitihani kama miwili hivi nakumbuka nilikuwa nipo Bongo nina show wenzangu wakafanya lakini nilikuja nikarudia, so changamoto kama hizo zinapatikana na inabidi vitu vyote viende kwa wakati

Penny Afungukia Ujauzito Wake

Image
Pennieli Mungilwa.  MTANGAZAJI wa Kipindi cha Harusini kinachorushwa kupitia DSTV, Pennieli Mungilwa amefunguka kuumizwa na uzushi unaosambaa kuwa amenasa ujauzito kitu ambacho kinahatarisha uhusiano wake wa kimapenzi. Akizungumza na Star Mix , Penny alisema kuwa, jambo la mimba ni la heri lakini lazima lisemwe kwa ukweli siyo kuzusha kwa sababu linaleta matatizo makubwa sana kwa mtu ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine. “Yaani sina ujauzito wa mtu yeyote yule na hakuna mtu mbaye hapendi kupata lakini kwa mtu sahihi na wakati muafaka sasa mimi watu wakinibambika hilo wananiletea shida pia kwenye uhusiano wangu nilionao,” alisema Penny. Na Imelda Mtema | Ijumaa | Star Mix

Prof, Muhongo aibuka ajibu tuhuma

Image
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema hahusiki na mikataba yote ya madini. Muhongo alitoa maelezo hayo jana, ikiwa ni siku moja baada ya Nipashe kuripoti kutoonekana kwake bungeni bila ruhusa ya Spika. Aidha, Prof. Muhongo aliidokeza Nipashe chanzo cha kutokuwapo kwake katika chombo hicho cha kutunga sheria kwa wiki tano sasa. Baada Gazeti la Nipashe  jana liliripoti kuhusu kutoonekana bungeni kwa Mbunge huyo wa Musoma Vijijini (CCM) bila ruhusa ya Spika tangu uteuzi wake katika baraza la mawaziri utenguliwe wiki tano zilizopita. Katika ripoti hiyo ya jana, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema ofisi yake haina taarifa za mtaalamu huyo wa kimataifa wa jiolojia na haijui aliko tangu alipoachishwa nafasi ya uwaziri, muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kukabidhiwa ripoti ya kamati ya kwanza ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu (makinikia) Mei 24, mwaka huu. Hata hivyo, jana asubuhi Prof. Muhongo kupitia simu yake ya

GONJWA LA ZARI THE BOSS LADY HOFU YATANDA,SIKU CHACHE MUMEWE KUFARIKI

Image
PRETORIA: Takriban siku 25 baada ya kifo cha aliyekuwa mumewe, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’, staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ameibua hofu kubwa kwa ndugu, jamaa na marafi ki baada ya kupata gonjwa la ghafla lililosababisha kukimbizwa hospitalini akiwa hoi.Kwa mujibu wa mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, mapema wiki hii, Zari alikimbizwa hospitalini huko Pretoria nchini Afrika Kusini na kulazwa kutokana na hali yake kuwa mbaya. Ilifahamika kwamba, Zari alikutwa na hali hiyo siku moja tu tangu mama yake mzazi, Halima Hassan naye alazwe jijini Kampala, Uganda kwa matatizo ya moyo kushindwa kufanya kazi hivyo kupishana kwa saa kadhaa za kukimbizwa hospitalini. NI SIKU CHACHE TANGU AKABIDHIWE OFISI YA IVAN Ilielezwa kwamba, Zari ambaye ni mfanyabiashara wa Uganda mwenye makazi Afrika Kusini alikutwa na hali hiyo ikiwa ni siku chache tangu alipoanza kufanya kazi kwenye ofi si ya Ivan aliyokabidhiwa hivi karibuni huko Pretoria, Juni

HISTORIA YA MUUZA MADAWA YA KULEVYA NGULI DUNIANI PABO ESCOBAR

Image
Katika milima inayotazamana na mji wa Medellín nchini Colombia, yapo majengo ya kifahari kabisa ndani ya milima hiyo ambayo kwa sasa majengo haya yanatumika kama nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki lakini kabla ya watawa hawa kupewa majengo haya mwaka 2007, majengo haya yalikuwa ni gereza ambalo lilijengwa mwaka 1991 kumuhifadhi mfungwa maalumu raia wa Colombia.Gereza hili lilikuwa ni tofauti kabisa na magereza yote ambayo umewahi kuyasikia kwani gereza hili licha ya kuwa mali ya serikali lakini michoro yake ilichorwa na kubuniwa na mfungwa mwenyewe. Si hivyo tu, bali hata maaskari magereza ambao walikuwa wanalinda gereza hili walichaguliwa na mfungwa mwenyewe na hata polisi wa nchi ya Colombia walikuwa hawaruhusiwi kusogolea gereza hilo hata umbali wa maili 12. Kama hiyo haitoshi gereza hili lilikuwa na uwanja wa mpira wa miguu, lilikuwa na bafu lenye Jaccuzi, lilikuwa na bar, lilikuwa na maporomoko ya maji (water falls) yaliyobuniwa kiustadi, na pia chumba (sel

Kauli ya Yanga Kuhusu Kuondoka kwa Niyonzima

Image
TAARIFA KWA UMMA ​ Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu. Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo. Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla. Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo Young Africans Sports club. 21-06-2017.