Posts

Dalili za Madhara ya Tezi Dume

Image
Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe za uhai katika tezi la kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalozunguka mirija ya kupitisha haja ndogo( mkojo).Ugonjwa huu kwa sasa unaweza kuwapata vijana wa kiume kuanzia miaka 25 na kuendelea tofauti na awali ilikuwa miaka zaidi ya 50. Dalili za ugonjwa huu; Kwenda haja ndogo mara kwa Mara,hasa usiku. Haja ndogo Za ghafla zisizoweza kudhibitiwa. Mkojo unaotoka kwa udhaifu ama kwa kukatika katika . Damu kuchanganyikana na mkojo. Maumivu  yanaendelea kwenye maeneo ya mgongoni sehemu Za kiunoni,kwenye kinena au sehemu juu ya mapaja. Madhara yake: 1.Kupungua kwa uwezo kufanya tendo la ndoa.Pia kusikia maumivu wakati wa kufikia kilele Na kukosa amani au kuhangaika  wakati wa tendo la ndoa. 2.Uambukizo wa magonjwa kwenye kipofu 3.Uambukizo  mwenge njia ua mkojo au figo. Ndugu ugonjwa huu unaua hata wenye uwezo wa kifedha maana ni hatari sana chukua tahadhari sasa pia msaidie na mtu mwingine

Halima Mdee na Ester Bulaya Kulipwa nusu Mshahara

Image
Wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) ambao wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge, watalipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana nao kwa miezi kumi. Stahiki hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya Bunge inayosema, “mbunge aliyesimamishwa hataingia tena sehemu yoyote ya ukumbi na maeneo ya Bunge kwa muda wote atakapokuwa amesimamishwa na atalipwa nusu mshahara na nusu posho zinazoambatana na mshahara huo.” Vilevile, kutokana na uamuzi huo wabunge hao watakosa siku 65 za Bunge zinazojumuisha siku 25 zilizobaki za Bunge la bajeti linaloendelea, Bunge la Oktoba na lile la Februari, 2018. Vikao vya mabunge hayo mawili; la Oktoba na Februari kila kimoja huwa na mikutano ya wiki mbili mbili. Wabunge hao walisimamishwa juzi kwa azimio la Bunge licha ya kutokuwapo au kujitetea kutokana na tuhuma zilizokuwa zinawakabili za kudharau kiti cha spika. “Tukutane Bunge lijalo la bajeti,” alisema juzi Spika wa Bunge, Job Ndugai. Bunge l

IGP SIRRO AFANYA ZIARA KIBITI,ATANGAZA VITA KALI,ATANGAZA DONGE LA MILIONI 10 s

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amefanya ziara katika maeneo ya Kibiti na Mkuranga kutimiza ahadi baada ya kuombwa na wazee wa maeneo hayo kufuatia mauaji ambayo yamekuwa yakiripotiwa kutokea mara kwa mara.Mara baada ya kuzungumza na wazee hao, IGP Sirro amesema kuwa wazee hao wametoa ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na namna ya kuwapata waharifu ambao wamekuwa wakifanya mauaji katika maeneo hayo. Sirro amewaahidi wananchi wa maeneo hayo kuwa atatoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa raia mwema atakayetoa taarifa sahihi kwa watu wanaofanya mauaji mkoani. Tazama hapa

MSIBA WA IVAN WAMUIBUA BABA YAKE ZARI,AFUNGUKA MENGI MAZITO

Image
Kwa muda mrefu staa wa muziki na mjasiriamali wa Afrika Mashariki, raia wa nchini Uganda, mwenye maskani yake mengine huko Pretoria, Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amekuwa akionekana Bongo na mama yake mzazi, Halima Hassan hivyo kuibua sintofahamu juu ya alipo baba yake, Hassan Tiale. Hata hivyo, kifo cha mkwe wake yaani aliyekuwa mume wa mwanaye, Zari, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ aliyefariki dunia Mei 25, mwaka huu, kimemaliza utata huo baada ya kumuibua mzee huyo aliyekuwa amejaa tele kwenye msiba huo nchini Uganda. Mzee Hassan alikuwa mmoja wa watu lukuki waliohuzunishwa na kifo cha Ivan ambapo alisema kuwa, alilazimika kuacha shughuli zake ili kuhudhuria msiba huo kwa namna alivyokuwa akiivana na Ivan. “Msiba huu umenigusa sana. Nilipigiwa simu nikiwa Nairobi (Kenya) ambako nilikwenda kumuozesha kijana wangu bibi (mke) “Nilisikia Ivan aliteleza kwa ajili ya presha, akaanguka chini, akachukuliwa, akapelekwa hospitalini Afrika Kusini, akawe

MAREHEMU PHILEMON NDESMBURO AZIKWA MKOANI KILIMANJARO

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Freeman Mbowe akiwasili nyumbani kwa marehemu Philemon Ndesamburo wakati alipohudhuria mazishi yake yaliyofanyika leo  Moshi mkoani Kilimanjaro Marehemu Ndesamburo alifariki wiki iliyopita na kuzikwa leo mkoani humo angalia matukio mbalimbali  katika picha kuhusu tukio zima la ibada ya mazishi.(Picha na Dixonbusagagablog).

Wafahamu Wanawake 4,000 Wanaojifunza Kuwa Maninja Iran

Image
 Miongoni mwa wanawake 4,000 wanaochukua mafunzo ya uninja jangwani nchini Iran. WANAWAKE nchini Iran hivi sasa wanajifunza mbinu za wapiganaji wa Ninja kupitia mbinu za Ninjutsu katika klabu ya mafunzo hayo iliyofunguliwa mwaka 1989 iliyopo Jughin, kilomita zipatazo 52 kutoka jiji la Tehran. Mafunzo hayo yanayofanyika jangwani,  yamelenga kuwafanya wanawake hao kuwa ‘kunoichi’, yaani maninja wa kike.  Katika mafunzo yao wanawake hao wanafanya mazoezi ya kupanda na kuruka kutoka katika kuta mbalimbali, kujificha katika milima na kuweza ‘kukata’ shingo ya adui bila kelele yoyote.