Posts

Rose Muhando atiwa mbaroni

Image
Jeshi  la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili, Rose Muhando akituhumiwa kujipati fedha kwa njia ya udanganyifu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora Mgiligimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mwimbaji huyo alikamatwa juzi Wilaya ya Ikungi baada ya wadeni wake ambao ni Waumini wa Kanisa la AICT Singida kupata taarifa kuwa yupo wilayani humo. Inadaiwa kuwa Novemba 3 mwaka jana, mwimbaji huyo alitumiwa fedha na Mwenyekiti wa Kwaya ya Kanisa la AICT Singida, Mashala Japhet Tsh 800,000 ambapo zilitumwa baada ya pande mbili kukubaliana kuwa angekwenda kwenye uzinduzi wa Album ya kwaya na kanisa hilo, hata hivyo hakutokea. Kwa mujibu wa kamanda huyo, uzinduzi wa kwaya hiyo ulikuwa ufanyike Novemba 13 mwaka jana, saa 8 mchana katika uwanja wa Namfua Singida. Novemba 8 mwaka jana, mwimbaji huyo aliomba kutumiwa tena 150,000 kwa ajili ya nauli ya kutoka Dodoma kwend

TAARIFA MPYA ZA MTOTO DOREE WA AJALI YA LUCKY VICENT

Image
Mtoto Doreen Mshana, manusura wa ajali ya Lucky Vincent, ameruhusiwa kutoka Hospitali na sasa ameungana na wenzake wawili katika nyumba maalum wanamoishi, Marekani, jimbo la Iowa. Awali, wanafunzi wengine waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy Hospital, Sioux City, Saidia Awadh na Wilson Tarimo, waliruhusiwa kutoka hospitali walimokuwa wakitibiwa. Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ameandika katika ukurasa wake wa facebook na kueleza kuwa sasa Doreen, ameungana na wenzake baada ya hali yake kuimarika. Doreen, alibaki hospitali hapo kutokana na majereha makubwa aliyopata na hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo. Wanafunzi hao walinusurika katika ajali ya basi la shule ya msingi ya Lucky Vincent, iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva, Mei 6 mwaka huu, Karatu, Arusha.

Breaking News: Halim Mdee na Ester Bulaya wapewa adhabu ya kutohudhuria Bungeni mpaka mwakani

Image
Halima Mdee na Esther Bulaya wamehukumiwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19. Hukumu hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo. Mapema leo, Jumatatu Kamati ya Maadili  ilisema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge. Hata hivyo, Bunge liliendelea  kujadili makosa ya wabunge hao wa Bunda na Kawe. Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao. Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.

Faida ya kula karoti

Image
Ulaji wa karoti kwa wingi, hasa karoti yenye hali ya ubichi husaidia kutibu magonjwa yafutayo; 1. Huongeza kinga za mwili. Pia ni chanzo kizuri cha vitamin na husaidia kuongeza kinga ya mwili hivyo kusaidia mwili kutopata magonjwa. 2. Husaidia kuona vizuri. vitamin A ambayo ina patikana kwa wingi husaidia kuongeza uwezo wa kuona na mawasiliano ya seli. Pia ina madini kama sodiam,sulphur,chlorine na iodine. 3. Husaidia matatizo kutibu matatizo ya ngozi. Juisi ya caroti husaidia sana katika kutibu ngozi iliyo kauka. 4. Kutibu vidonda vya tumbo. Ulaji wa mara kwa mara hupunguza uwezo wa kupata vidonda vya tumbo pamoja na madhara mengine kwenye mfumo wa chakula.

MSANII HARMONIZE WA WCBAACHIA PICHA HIZI NA MPENZI WAKE MPYA (+PICHAZ)

Image
Baada ya Kuachana na mrembo wa filamu Tanzania  Jacqueline Wolper , ilisemekana kuwa WCB super staa  Harmonize  anampenzi mpya, mzungu , ana pesa, kamnunulia gari Harmonize na anamjengea jumba kubwa huko Madale

Fainali Uefa Champions League… Leo Shughuli Ipo

Image
  NA MWANDISHI WETU SIYO siri leo Jumamosi watu duniani watasimamisha shughuli zao kwa muda kutazama fainali ya 62 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inayozikutanisha Juventus na Real Madrid kwenye Uwanja wa Millennium. Mwamuzi Felix Brych wa Ujerumani ndiye atakayechezesha mechi hii kali iliyojaa historia nyingi ambayo ni ngumu kutabiri mshindi moja kwa moja. Mpaka inafi ka fainali chini ya Kocha Massimiliano Allegri, Juventus iliitoa Monaco kwa jumla ya mabao 4-1, wakishinda mabao 2-0 halafu 2-1. Madrid ikiongozwa na Kocha Zinedine Zidane iliitoa Atletico Madrid kwa jumla ya mabao 4-2. Madrid ilishinda 3-0 halafu ikafungwa 2-1. Fainali hii inakumbusha fainali ya Uefa ya Mei 20, 1998 ambapo timu hizi zilikutana kwenye Uwanja wa Amsterdam na Madrid ikashinda bao 1-0 lililofungwa na Predrag Mijatovic. Ni miaka 19 sasa tangu timu hizo zilipokutana katika fainali hiyo, wakati huo Zidane alikuwa akiichezea Juventus sambamba na Kocha wa Chelsea sasa, Antonio Conte. J

KAULI YA MO DEWJI BAADA YA KUKUTANA NA BILL GATES

Image
Tajiri kijana namba moja kwa Afrika, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya METL amefanikiwa kukutana na tajiri namba moja duniani, Bill Gates na kufanikisha moja ya ndoto zake ambapo wameweza kubadilishana mawazo juu ya biashara zao. Dewji na Bill ambaye ni Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, wamekutana wiki hii katika mkutano mkuu wa Giving Pledge. kupitia mitandao ya kijamii, Dewji ameonekana kufurahi zaidi baada ya kukutana na tajiri huyo namba moja duniani. “Ninafarijika na kuhamasika kujifunza kutoka kwa #BillGates hasa leo kwenye mkutano mkuu wa #GivingPledge, pia kupata maarifa juu ya namna ya kuboresha maisha ya wahitaji duniani,” ameandika katika mtandao huo.

MBUGA ZA WANYAMA UNAZOWEZA KUTEMBELEA BURE WIKENDI HII

Image
Siku ya Jumatatu ya Juni 5 itakuwa ni maadhimisho ya ‘Siku ya Mazingira Duniani’ ambayo huadhimishwa na mataifa tofauti duniani ikiwa imebeba kauli mbiu ya ‘Kuwaunganisha Watu na Mazingira Asilia.’ Mapema wiki hii Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba  alitoa taarifa kwa umma kuwa kwa hapa nchini maadhimisho ya siku hiyo kitaifa yatafanyika kijijini Butiama mkoani Mara, mahali alipozaliwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl. Julius Nyerere, ikiwa ni kuenzi jitihada zake za kulinda na kuhifadhi mazingira. Katika kunogesha sherehe hizo Waziri huyo amesema kuwa serikali imetoa ofa kwa wananchi kutembelea hifadhi yoyote ya mbuga ya wanyama bila ya kiingilio chochote kwa siku tatu, kuanzia Ijumaa ya Juni 2 mpaka Jumapili ya Juni 4. Alisema kuwa lengo kubwa ni kuona uwepo wa wanyama na kujifunza kuwa mazingira yanahitaji kulindwa zaidi na zaidi. Kauli hiyo ya Waziri imekuja siku c

KIASI CHA PESA KILICHOKUTWA NYUMBANI KWA IVAN NCHINI AFRIKA KUSINI

Image
Hiki ndicho kiasi cha pesa kilichokutwa nyumbani kwa IVAN nchini South Africa Hiki ndicho kiasi cha pesa kilichokutwa nyumbani kwa IVAN nchini South Africa Inakadiriwa takribani dola milioni 300 na Rand miioni 600 zimekutwa nyumbani kwa Marehemu IVAN

DAKTARI AELEZA SUMU ILIYOMUUA MUME WA ZAMANI WA ZARI,AFICHUA SIRI NZITO

Image
Stori: Waandishi Wetu  KAMPALA: Imefichuka! Nyuma ya msiba ulioacha historia wa aliyekuwa mzazi mwenza wa staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ivan Ssemwanga ‘The Don’ aliyepatwa na umauti wiki iliyopita akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Steve Biko, Pretoria nchini Afrika Kusini, kuna mengi yanayosemwa, Wikienda liko bega kwa bega na kinachojiri. Miongoni mwa yanayosemwa ni madai ya jamaa huyo kupewa sumu iliyomdhuru moyo hivyo kusababisha kifo chake. MADAI YA SUMU Chanzo cha ndani ya familia ya Ivan kililieleza gazeti moja maarufu nchini Uganda kuwa, Ivan alilishwa sumu na watu ambao hawakuwataja na kwamba mara ya mwisho alikuwa akipata chakula na ndugu zake kabla ya hali yake kuanza kuwa mbaya kisha siku chache baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya Steve Biko.Gazeti hilo lilimkariri mtu huyo akieleza kuwa, Ivan hakufa kwa shambulio la moyo wala moyo kushindwa kufanya kazi bali aliwekewa sumu kali kwenye chakula. MAUMIVU MAKALI

Maisha Ya Mke wa Deo Filikunjombe Baada ya Miaka Miwili ya Kifo Cha Mumewe

Image
Mkewe  wa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, marehemu Deo Haule Filikunjombe, Sarah Filikunjombe. STORI: BRIGHTON MASALU NA ANDREW CARLOS, IJUMAA, HABARI MAMA shujaa! Ikiwa imebaki miezi minne na siku kadhaa itimie miaka miwili kutokea kwa kifo cha aliyekuwa kada muaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, marehemu Deo Haule Filikunjombe, mkewe Sarah Filikunjombe (Pichani) amethibitisha ushujaa kwa kuendelea kupambana na changamoto za kimaisha na kufikia vilele mbalimbali vya mafanikio, Ijumaa limemfungia kazi. Mwishoni mwa wiki iliyopita na mwanzoni mwa wiki hii, kwa siku tatu tofauti, waandishi wetu walijipa kazi ya ziada ya kumtafuta Sarah ili kujua nini kimeendelea katika maisha yake baada ya kuondoka kwa mumewe ambapo walibaini mambo mengi mazuri yenye kutia moyo, ambayo mama huyu licha ya kuonekana sistaduu, ameyafanya kwa ujasiri wa kipekee. IJUMAA NYUMBANI KWAKE Hatimaye Jumanne mchana, gazeti hili l