DAKTARI AELEZA SUMU ILIYOMUUA MUME WA ZAMANI WA ZARI,AFICHUA SIRI NZITO
Stori: Waandishi Wetu
KAMPALA:
Imefichuka! Nyuma ya msiba ulioacha historia wa aliyekuwa mzazi mwenza
wa staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ivan
Ssemwanga ‘The Don’ aliyepatwa na umauti wiki iliyopita akiwa amelazwa
kwenye Hospitali ya Steve Biko, Pretoria nchini Afrika Kusini, kuna
mengi yanayosemwa, Wikienda liko bega kwa bega na kinachojiri.
Miongoni mwa yanayosemwa ni madai ya jamaa huyo kupewa sumu iliyomdhuru moyo hivyo kusababisha kifo chake.MADAI YA SUMU
Chanzo
cha ndani ya familia ya Ivan kililieleza gazeti moja maarufu nchini
Uganda kuwa, Ivan alilishwa sumu na watu ambao hawakuwataja na kwamba
mara ya mwisho alikuwa akipata chakula na ndugu zake kabla ya hali yake
kuanza kuwa mbaya kisha siku chache baadaye alikimbizwa katika Hospitali
ya Steve Biko.Gazeti hilo lilimkariri mtu huyo akieleza kuwa, Ivan
hakufa kwa shambulio la moyo wala moyo kushindwa kufanya kazi bali
aliwekewa sumu kali kwenye chakula.
MAUMIVU MAKALI
Sosi huyo
alisema kuwa, baada ya sumu hiyo, muda mwingi Ivan alikuwa akilalamika
maumivu makali ya tumbo na kuomba kuwahishwa hospitalini.Hata hivyo,
mbali na madai hayo, taarifa za kitabibu zilieleza kuwa, Ivan alifariki
dunia kutokana na shambulio la moyo bila kuweka bayana kama alipewa sumu
au la.Katikati ya mkanganyiko huo, Wikienda lilizungumza na daktari
wake aliyekubaliana na maelezo kuwa inawezekana sumu hiyo ndiyo
iliyomdhuru moyo na kumsababishia tatizo la Atrial Fibrillation.
ATRIAL FIBRILLATION NI NINI?
Daktari
huyo alisema kuwa, Atrial Fibrillatoni ni ugonjwa ambao huufanya moyo
badala ya kuwa unadunda kama ilivyo kawaida, uwe unatetemeka na
kusababisha shida katika mfumo mzima wa upumuaji na usukumaji wa
damu.Tatizo hili, huwa linatokea kwenye chemba za juu za moyo (Atria)
ambazo kimsingi misuli yake ndiyo inayosababisha moyo kudunda.
Misuli
hii inapoishiwa nguvu, hushindwa kuzalisha nguvu ya kutosha kusukuma
damu na badala yake, hutetemeka na matokeo yake, damu huanza kuganda
kwenye mishipa (blood clotting) kwa sababu ya kukosekana kwa presha ya
kuisukuma na kuifanya izunguke mwili mzima kisha kurudi tena kwenye
moyo.Kwa baadhi ya watu, tatizo hili hutokea mara moja na kuacha au kwa
kitaalam Sporadic Fibrillation na kwa wengine, ikitokea mara moja
huendelea bila kupata ahueni yoyote au kwa kitaalam Persistent
Fibrillation.
NINI CHA KUFANYA?
“Unapoona
hali ya aina hiyo ni muhimu kuwahi hospitalini baada ya kuona dalili za
ugonjwa huu kwani ukichelewa, husababisha damu kuganda kwenye viungo
muhimu katika mwili, hasa kwenye ubongo.
“Pia
inapotokea damu imeganda kwenye ubongo, husababisha mifumo mingine ya
mwili kama upumuaji na mfumo wa fahamu kuwa kwenye hatari ya kushindwa
kufanya kazi, jambo ambalo ni hatari kwa maisha.
“Inapotokea
damu imegandia kwenye ubongo kutokana na tatizo hili, madaktari ni
lazima wafanye kwanza upasuaji wa kuondoa damu hiyo kwenye ubongo kisha
baada ya hapo ndipo waendelee na kutibu chanzo cha tatizo, ambacho huwa
ni kwenye moyo.
“Mara
zote, Atrial Fibrillation husababisha mgonjwa apatwe na ‘stroke’ na
endapo tatizo hili likiwa ni lile la kuendelea, Persistent Fibrillation,
uwezekano wa mgonjwa kupona huwa mdogo.
NINI KINASABABISHA?
“Yapo
mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha tatizo la Atrial Fibrillation,
miongoni mwa hayo ni matatizo ya shinikizo la damu ya muda mrefu, kuziba
kwa mishipa ya damu kunakoweza kusababishwa na mwili kuwa na mafuta
mengi (cholesterol). “Hii huwapata zaidi watu wanene. Pia matatizo
katika valvu za moyo, huweza kusababisha tatizo hili.
“Atrial
fibrillation inaweza pia kusababishwa na kuumia kifua au upasuaji wa
kifua ambao haukwenda vizuri. Wapo pia watu waliopatwa na tatizo hili
kwa sababu ya kunywa sana pombe kupita kiasi.
UWEZEKANO MDOGO WA KUPONA
“Tiba za
muda mrefu huweza kusababisha mgonjwa akapona ingawa nafasi ya kupona
kwa wagonjwa wanaopatwa na Persistent Fibrillation huwa ni ndogo,”
alisema daktari huyo.
ZARI, MASHEMEJI ZAKE PACHIMBIKA
Hata
hivyo, wakati Ivan akiagwa leo nchini Uganda kisha kuzikwa kesho, kuna
taarifa zilizoenea mno wikiendi iliyopita zikionesha kuwa, katika
kipindi cha kuuguza, Zari alikuwa ‘bize’ akisuguana na kaka wa Ivan
pamoja na mashemeji zake akiwemo King Lawrence juu ya mali alizoacha
marehemu.
IVAN AMEACHA NINI?
Ivan
ameacha shule sita nchini Afrika Kusini, hoteli mbalimbali pamoja na
majumba nchini Uganda. Ameacha pia watoto watatu, Pinto, Raphael na
Quincy.
Comments
Post a Comment