Posts

Maisha Ya Mke wa Deo Filikunjombe Baada ya Miaka Miwili ya Kifo Cha Mumewe

Image
Mkewe  wa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, marehemu Deo Haule Filikunjombe, Sarah Filikunjombe. STORI: BRIGHTON MASALU NA ANDREW CARLOS, IJUMAA, HABARI MAMA shujaa! Ikiwa imebaki miezi minne na siku kadhaa itimie miaka miwili kutokea kwa kifo cha aliyekuwa kada muaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, marehemu Deo Haule Filikunjombe, mkewe Sarah Filikunjombe (Pichani) amethibitisha ushujaa kwa kuendelea kupambana na changamoto za kimaisha na kufikia vilele mbalimbali vya mafanikio, Ijumaa limemfungia kazi. Mwishoni mwa wiki iliyopita na mwanzoni mwa wiki hii, kwa siku tatu tofauti, waandishi wetu walijipa kazi ya ziada ya kumtafuta Sarah ili kujua nini kimeendelea katika maisha yake baada ya kuondoka kwa mumewe ambapo walibaini mambo mengi mazuri yenye kutia moyo, ambayo mama huyu licha ya kuonekana sistaduu, ameyafanya kwa ujasiri wa kipekee. IJUMAA NYUMBANI KWAKE Hatimaye Jumanne mchana, gazeti hili l

Undani wa Kifo Cha Mume wa Zari Nyuma ya Pazia

Image
Staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, akiwa na aliyekuwa mume wake Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’ enzi za uhai wake.  STORI: SIFAEL PAUL, RISASI JUMAMOSI, MTANDAO KAMPALA: Kifo cha aliyekuwa mume wa staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’, raia wa Uganda, mwenye maskani yake Johannesburg na Pretoria, Afrika Kusini, kimeibua simulizi nzito nyuma ya pazia. Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Ivan iliyopo Muyenga jijini Kampala, kilichokaririwa na mitandao ya kuaminika nchini Uganda, katika siku za mwisho za maisha yake kabla ya kuripotiwa kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo ambao kitaalam huitwa Coronary Artery Disease (CAD). Ilifahamika kuwa, ugonjwa huo ndiyo uliomsababishia kifo usiku wa kuamkia juzi. Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’ alipokuwa hospitali. MARA YA MWISHO KUONEKANA Habari zilieleza kuwa, Ivan alionekana kwa mara ya mwisho kwenye Pat

EVERTON KUCHEZA NA SIMBA AU YANGA,JULAI 13 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Timu ya Everton ya England yenye wachezaji nyota akiwemo Mbelgiji, Romelu Lukaku, itazuru Tanzania kucheza mechi za kujiandaa na msimu mpya wa 2017/18, tovuti ya klabu hiyo imeandika. Ziara hiyo ambayo itakuwa sehemu ya sherehe zao za udhamini mpya wa kampuni ya SportPesa, itaifikisha The Blues kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam unaomeza mashabiki 60,000 kucheza mechi Alhamisi ya Julai 13. Everton itakuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England daima kucheza mechi ukanda wa Afrika Mashariki – na itamenyana na bingwa wa mashindano ya SportPesa Super Cup. Nchi mbili, Tanzania na Kenya zitakutanisha timu zao nane, nne kutoka kila upande katika michuano hiyo, kuwania nafasi ya kucheza na kikosi cha Ronald Koeman.  Mapema mwezi huu, Everton ilitangaza udhamini mnono wa rekodi na SportPesa wa miaka mitano na baada ya hapo kampuni hiyo ikaingia Afrika Mashariki kufunga ndoa na klabu kadhaa kubwa, zikiwemo SImba na Yanga. Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa

DIAMOND PLATINUMS AMWANDIKIA ZARI THE BOSS LADY UJUMBEE HUU AKIWA MSIBANI

Image
F

Wolper Atokwa na Povu Baada ya Kubanwa Kuhusiana na Madai ya Kunuka Mwili

Image
Staa wa filamu ‘grade one,’ ‘Jacqueline Wolper’. STORI: ALLY KATALAMBULA NA BONIPHACE NGUMIJE, IJUMAA , HABARI Staa wa filamu ‘grade one,’ ‘Jacqueline Wolper’ ametokwa povu si la nchi hii baada ya kubanwa kuhusiana na madai ya kunuka mwili na kusema hajawahi kunuka maishani mwake na kwamba ingekuwa hivyo asingepapatikiwa na wanaume. Hivi karibuni Ijumaa lilimfungia kazi msanii huyo nyumbani kwake na katika moja ya maswali aliyobanwa lilikuwa juu ya ishu iliyosambaa kuwa eti anatoa harufu mbaya sehemu za mwili wake. Katika kuonesha kumaindi ile mbaya kuhusu madaia hayo, mrembo huyo ambaye kiukweli yuko bomba kwa muonekano alifunguka: “Aliyekuambia nanuka nani? Mimi sinuki wala sijawahi kunuka maishani mwangu, kuthibitisha hilo kwanza nisingekuwa napapatikiwa na wanaume kila kukicha sambamba na kuhongwa vitu kibao huku wengine nikiwaacha wakinililia. Hao wanaosema na kusambaza hayo ni njia tu ya kujipatia followers kwenye mitandao yao kupitia mimi.” Wolp

Polepole: Watu wanaishi kwa hofu

Image
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amefunguka na kusema watu wamekuwa na hofu huku wengine wakihama makazi yao mkoani Pwani kutokana na vitendo vya mauaji vinavyoendelea mkoani humo. Polepole amesema wao kama CCM wanaitaka serikali ichukue hatua za haraka katika jambo hilo kwa kuwa ina vyombo vyote vya ulinzi na usalama, hivyo wanataka kuona jambo hilo linapewa umaalum katika kulishugulikia. "Sisi kama chama tumelifuatilia hili suala kwa umakini sana na tumeona ni vyema kusimama na Watanzania wakiwepo na wanachama wa CCM wa maeneo haya, tunatambua wanapitia wakati mgumu sana kwani wapo viongozi wetu, wapo wanachama wa CCM, na watendaji mbalimbali wamepoteza maisha. Wamepoteza maisha si kwa sababu ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu bali maisha yao yamekatizwa kikatili" alisisitiza Polepole Kufuatia mambo haya kuendelea kutokea mkoani Pwani Chama Cha Mapinduzi kimetoa salamu za pole kwa wananchi wote ambao wameguswa na misiba ya watu am

Faida (6) za tangawizi

Image
Siku kadhaa zilizopita tuliona kwa uchache faida za tangawizi, naomba siku ya leo tuendelee faida nyingine za tangawizi ambazo ni; 1. Husaidia wenye kifafa au Msongo wa mawazo Wataalamu wanasema kifafa kinasababishwa na mishipa kuvimba na kukandamiza ubongo na tangawizi inatumika husaidia kuondoa mafuta katika mishipa, kutia joto mwili na kusaidia damu yenye oxygen kusambaa mwilini na kwenye ubongo bila shida. 2. Huondoa gesi tumboni Tangawizi husaidi mmeng'enyo wa chakula tumboni, kwa hiyo husaidia matatizo mengi yanayosababishwa na ulaji. 3. Husaidia kutibu mafua, kikohozi Unachitakiwa kufanya. Changanya mdalasini, pilipili manga kidogo, chemsha kama chai pamoja na tangawizi. Husaidia sana mafua na kikohozi. 4. Huongeza nguvu za kiume Tangawizi inauwezo wa kuongeza joto mwilini, hivyo huamsha mishipa ya fahamu katika mwili wa mwanaume mwenye tatizo hilo. 5.Huongeza maziwa kwa kina mama wanyonyeshao. Kwa kina mama wanaonyenyesha tangawizi inachoche

NAIBU WAZIRI DKT.KINGWANGALLA AMTEMBELEA MZEE MAIGE’NGOSHA ‘ MUHIMBILI

Image
Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kingwangalla akiongea na Mzee Maige ambaye amelazwa kwenye chumba cha kitengo cha dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo asubuhi ya leo mzee huyo alihamishiwa hapo kwa uchunguzi wa afya na matibabu zaidi kutoka hospitali ya Rufaa ya Amana. Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura Renatus Tarimo(kushoto) akimueleza Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto jinsi walivyompokea na kumuhudumia kwenye kitengo chao na hali ilivyo hadi sasa,Dkt. Tarimo amesema hali ya Mzee maige inaendelea vizuri na wameshamfanyia uchunguzi wa awali na wanaendelea na uchunguzi zaidi Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga (katikati) akimueleza jambo Naibu Waziri Dkt. Kingwangalla mara baada ya kutoka kwenye chumba alicholazwa Mzee Maige.Mzee Maige au kwa jina maarufu anajulikana kama Ngosha ndiye aliyebuni Nembo ya Taifa ambayo ina