Posts

MREMBO ALIPIA BANGO KATIKATI YA JIJI AKITANGAZA KUWA BIKIRA,ADAI ANASAKA TENDO KABLA HAJAFA

Image
Katika hali isiyo ya kawaida, muigizaji wa vipindi vya TV mwenye umri wa miaka 40 amelipia ‘Bango’ kubwa katikati ya jiji akijitangaza kuwa ni bikira anayetafuta mwanaume wa kufanya naye tendo la ndoa ili asife bila kujua uhondo wake.Kwa mujibu wa Daily Mirror, Aranya ‘Pui’ Pathumthong ambaye ni muigizaji wa Thailand, aliyeweka bango hilo katika jiji la Bankok, karibu na wilaya ya Lat Phrao amesisitiza kuwa yuko ‘serious’ na tangazo hilo ambalo ameliweka baada ya matangazo yake kupitia mitandao ya kijamii ya mahusiano nchini humo kushindwa kuzaa matunda. Tangazo lake limeandikwa, “I Want You. “40 and a virgin. Pui Aranya is looking for a husband!”Let me get it once before I die.” Linaonesha namba ya simu pia.Aranya ameviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa ameamua kusaka mwanaume kwa mtindo huo ili aweze kuonja raha ya penzi kabla hayafa.Hata hivyo, Polisi jijini humo wameamuru Bango hilo liondolewe ingawa limelipiwa na kuongeza kuwa wanahitaji kumhoji mwanamk...

Marekani: Mtoto Doreen Amemaliza Kufanyiwa Upasuaji wa Uti wa Mgongo

Image
  Taarifa ya Mbunge Lazaro Nyalandu Latest UPDATE: Mei 18, Alhamisi Saa 4:30 Usiku (Masaa ya Afrika Mashariki) Habari za HIVI PUNDE kutoka Hospitali ya Mercy, Sioux City IA MTOTO Doreen amemaliza KUFANYIWA UPASUAJI wa UTI wa MGONGO, kwa KILE ambacho MADKTARI wamesema kumefanikiwa kwa UFANISI Mkubwa, KUPITA matarajio yao. MTOTO Doreen alikuwa afanyiwe UPASUAJI kwa makadrio ya MASAA 5:30, LAKINI zoezi HILO lilikamilika kwa muda wa MASAA 4:00, Huku TEAM ya “Surgical Support” IKIWA na watu 6, na kwa PAMOJA wakiongozwa na MADAKTARI BINGWA 2, Dr. Meyer na Dr. Durward. MTOTO Doreen amehamishwa KUTOKA chumba cha UPASUAJI na kupekewa ICU, na MADAKTARI wamesema KWAKUWA hali yake imeridhisha SANA, BAADAYE Leo watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya UPASUAJI, na kumrudisha WODI ya WATOTO ambako ataendelea na MAPUMZIKO. MUNGU amesikia MAOMBI ya WATANZANIA na WOTE waliotoa SALA na DUA zao kwa ajili ya MTOTO Doreen POPOTE Duniani

STAA WA FILAMU YA KUCH KUCH HOTA HAI REEMA LAGOO AMEFARIKI DUNIA

Image
Reema Lagoo, muigizaji mkongwe kutokea nchini India aliyekuwa akiishi katika mji wa Mumbai amefariki dunia kwa kuugua kifua.Lagoo amefariki akiwa katika hospitali ya Dhirubhai Ambani, masaa machache baada ya kufikishwa hospitalini hapo. Marehemu amepata umaarufu kupitia filamu ya “Kuch Kuch Hota Hai”, Kabla ya umauti wake amekuwa akigiza mara nyingi kama mama kwenye filamu kama vile “Hum Aapke Hain Koun” na “Kal Ho Na Ho”.Lagoo mwenye miaka 59 kabla mauti kumfika, alifikishwa hospitalini hapo lakini alikuwa akilalamika juu ya maumivu makali ya kifua, Alisema msemaji wa Hospitali hiyo Bw. Ram Naraian.Kabla ya mauti kumfika, marehemu amewahi kuigiza filamu kama vile “Maine Pyar Kiya”, “Saajan”, “Vaastav, na “Hum Saath-Saath Hain”., pia alikuwa akionekana kwenye tamthilia iitwayo “Naamkaran”, inayooneshwa Star Plus

Vyakula 9 Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume

Image
  1.Soya (Soy):  Ina kiwango kikubwa cha Isoflavones ambayo ni kiuhalisia ni estrogen. Ulaji wa soya ni sawa na kula kidonge kimoja cha uzazi wa mpango (birth control pill). Kwa kuelewa zaidi madhara ya soya kwa wanaume soma hapa.   2. Licorice:  Huu ni mzizi ambao hutumika hasa kuondoa tatizo la msongo (stress) kwa watu wanaokumbwa na tatizo hilo. Pia mzizi huo hutumika kama sukari kwenye vinywaji kama chai au kahawa badala ya kutumia sukari ya kawaida. Hata hivyo mzizi huu una estrogen ambayo hushusha kiwango cha homoni ya kiume ya testosterone kwa wanaume. Kuna utafiti ulifanywa ambapo wanaume 7 wenye afya walipewa gramu 7 za vidonge vya licorice kila mmoja kila siku. Vidonge hivyo vilikuwa na kiasi cha gramu 0.5 za glycyrrhizic (kiambata kilichomo ndani ya licorice kinachopunguza testosterone kwa mwanaume). Baada ya siku 4 tu kiasi cha homoni ya testosterone kwa kila mwanaume aliyefanyiwa utafiti huo kilipungua kwa kiwango cha nusu ya...

SERENGETI BOYS MGUU NDANI KOMBE LA DUNIA,YAIBUTUA ANGOLA AFCON U-17 NCHINI GABON

Image
Timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya AFCON U17 baada ya kuifunga Angola kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kundi B uliochezwa Uwanja wa L’Amittee mjini Libreville,nchini Gabon. Vijana wa Serengeti Boys ndio walikua wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya sita kipindi cha kwanza baada ya Kelvin Naftal kupasia kamba kwa kichwa akiunganisha krosi ya Nickson Kibabage. Dakika ya 18 Angola walisawazisha bao hilo kupitia kwa Pedro baada ya kutumia vizuri makosa ya safu ya ulinzi ya Serengeti Boys na kufanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare kwa kufungana 1-1.Kipindi cha pili Serengeti waliongeza kasi kutafuta bao na kufanikiwa kufunga dakika ya 69 mfungaji akiwa ni Abdul Suleiman baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Yohana Mkomola. Serengeti Boys imefikisha pointi 4 baada ya kupata pointi moja kwenye mchezo wa kwanza kufuatia kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Mali ambao ndio ma...

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAY 19,2017

Image

Wamarekani Wafanikisha Upasuaji Mkubwa wa Wanafunzi Lucky Vincent

Image
May 18, 2017 Mtoto Wilson      Watoto watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vicent walionusurika katika ajali ya basi, wamefanyiwa upasuaji na sasa wapo wodini wakiendelea na mazoeazi, ila Doreen, jana alipewa MAPUMZIKO maalumu akiwa anaandaliwa tayari kwa UPASUAJI wa uti wa mgongo ‘spine’  unaofanyika leo.   Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyeshiriki katika kuwasafirisha watoto hao, ameandika katika ukurasa wake wa facebook akisema  watoto hao kwa sasa wamewekwa kwenye vyumba vya peke yao.   Mtoto Doreen Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani.   Amefafanua upasuaji waliofanyiwa na kusema mtoto Saidia alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa kulia wa nyonga, mkono wa kulia na kuwekewa ngao kwenye shingo atakayotakiwa kukaa nayo kwa wiki sita.   “Kwa upande wa mtoto Wilson, yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga ya kulia, kiwiko cha kulia kilichokuwa kimevunjika...