IMEFICHUKA! Mume wa Zari anasumbuliwa na ugonjwa huu
KAMPALA: Habari mbaya zilizolifikia mtandao huu zinadai kuwa, aliyekuwa mume wa staa wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Ssemwanga yu hoi bin taaban akisumbuliwa na maradhi ya shambulio la moyo (Coronary Artery Disease). Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya jijini Kampala, Uganda ambako ndiko maskani yake yalipo maeneo ya Munyonyo, pamoja na kwamba ana makazi Pretoria, Afrika Kusini, Ivan alionekana hadharani kwa mara ya mwisho akiwa amedhoofu na rangi ya ngozi kupauka, tofauti na alivyozoeleka kuwa na rangi nyeusi yenye mng’aro alipotinga kwenye Pati ya Blankets and Wine iliyofanyika Kampala hivi karibuni. Chanzo kilichomshuhudia Ivan kilitonya: “Sisi wenyewe tulipomuona kwenye Blankets and Wine Party akiwa na rafiki yake, Ed Cheune, kwanza hatukumtambua, lakini tulipomuangalia vizuri ndipo tukamjua ni yeye. Ukweli tulishtuka sana na tulijua anaumwa. “Tofauti na alivyozoeleka kuwa ni mtu wa bata, lakini siku hiyo alikuwa mpole sana. Al