FAHAMU UKWELI JUU YA VITA VYA KARANSEBES AMBAVYO ZAIDI YA WANAJESHI 10000 WALIUANA
Unaweza kudhani ni hadithi ya kutunga lakini hii kweli ilitokea! Vita ya Karansebes, ni miongoni mwa matukio yaliyoushangaza sana ulimwengu baada ya wanajeshi wa jeshi moja la Austria, kushambuliana wenyewe kwa wenyewe na kusababisha wanajeshi zaidi ya 10,000 kupoteza maisha. Ilikuwaje? Usiku wa Septemba 17, 1788, wanajeshi zaidi ya 100,000 wa Jeshi la Austria lililokuwa linaundwa na makabila mbalimbali, walikuwa wameweka kambi katika Mji wa Karansebes (Romania ya sasa) wakijiandaa kuvamia Himaya ya Ottoman (Uturuki ya sasa). Ili kurahisisha uvamizi, wanajeshi waligawana katika makundi, wengine wakaenda upande mmoja na wengine upande mwingine. Wakati wakijiandaa kufanya shambulio, kukatokea kutoelewana kati yao, wakaanza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe kimakosa wakidhani wanawapiga wanajeshi wa Ottoman. CHANZO CHAKE KINASHANGAZA Inaelezwa kuwa kundi moja kati ya yale mawili, lilivuka Mto Timis na kuingia Mji wa Hussar uliokuwa ngome ya wanajeshi washiri