Posts

KAJALA MASANJA AIBUKA TENA,SASA AMWANIKA MWANAUME WA KUMUOA

Image
MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja, amefunguka kuwa, endapo ataolewa tena, basi kigezo cha kwanza cha huyo mtarajiwa wake kitakuwa ni kudekezwa. Kajala ambaye aliolewa kisha ndoa yake kupata matatizo na mumewe kufungwa gerezani na hivi karibuni kuachiwa, alisema endapo itatokea ameolewa kwa mara nyingine basi kigezo cha huyo mwanaume ni lazima awe anayejua kudekeza. “Nampenda mwanaume mwenye mapenzi ya kweli lakini zaidi ya yote mimi napenda kudekezwa hivyo mwanaume atakayenioa lazima awe na sifa hizo vinginevyo atanisikia kwenye bomba,” alisema Kajala huku akiomba asimzungumzie mumewe ambaye ametoka gerezani hivi karibuni.

Lissu akomalia vyeti vya Bashite kortini

Image
WAWKILI Tundu Lissu na wenzake wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamelikomalia vilivyo sakata maarufu la Bashite linalohusiana na tuhuma za kughushi vyeti vya kielimu linalomkabili mmoja wa wakuu wa mikoa kwa kulifikisha kortini ili lipatiwe ufumbuzi. Aidha, Lissu na wenzake hao wamedhamiria kuona kuwa kigogo huyo anayetuhumiwa kuliacha jina lake halisi la Daudi Albert Bashite kutokana na matokeo mabovu ya sekondari na kutumia jina la mtu mwingine, achukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kufungwa jela kwa kosa la kughushi ikiwa itathibitika kuwa ana hatia. Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Lissu ambaye ni Rais wa TLS, alisema uamuzi huo wa kulifikisha mahakamani suala la Bashite umetokana na maazimio ya baraza la uongozi la chama hicho, lengo likiwa ni kulinda utawala wa sheria na uwajibikaji nchini. Tofauti na matarajio ya baadhi ya watu, sakata hilo la Bashite halikupatiwa jibu kutokana na ripoti ya uhakiki wa vyeti vy...

Tujikumbushe :Hotuba ya Mwalimu Julius K. Nyerere Aliyitoa kwwenye Mei Mosi 1995

Image
Mwalimu Nyerere alialikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifaUwanja wa Sokoine Mjini Mbeya Mei 1, 1995. Katika hotuba yake, Mwalimu alielezea historia ya Vyama vya Wafanyakazi duniani. Aidha alitumia fursa hiyo kutoa maoni yake kuhusu hali ya kisiasa na kiuchumi nchini pamoja na ushauri kuhusu mambo ambayo wananchi wanapaswa kuzingatia wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi wa Oktoba mwaka ule. Hasa sifa za wagombea nafasi za uongozi kuwa ni pamoja na kila mmoja kujiuliza ataifanyia nini nchi yake baada ya kuchaguliwa na anakwenda kufanya nini Ikulu? Ifuatayo ni hotuba ya Mwalimu. Ni muhimu kukumbuka kuwa hotuba hii imefuata mlolongo wa mazungumzo ambayo Baba wa Taifa alikuwa nayo kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ambapo alikuwa anajaribu kuamsha dhamira ya viongozi wetu wa wakati ule. Hotuba hii ni miongoni mwa hotuba ambazo ukweli wa hoja zake ni hazina kubwa kwa vizazi vijavyo vya Watanzania. Mwenyekiti wa OTTU, Vi...

Hiki ni kizaazaa kingine fao la kujitoa

Image
NI kizazaa kingine! Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika(TLS), limeazimia kushirikiana na wadau kwenda mahakamani kuhoji kuhusu utata juu ya fao la kujitoa uanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Hivi karibuni wakati serikali ikiwa katika maandalizi ya kuliondoa fao hilo, kulizuka taharuki kwa baadhi ya wafanyakazi walio wanachama wa mifuko hiyo. Ilielezwa kuwa fao la kujitoa likiondolewa litaletwa fao la kutokuwa na ajira. Katika mapendekezo hayo mapya, inaelezwa kuwa mfanyakazi ambaye amechangia zaidi ya miezi 18, atalipwa asilimia 30 ya mshahara wake wa mwisho baada ya kupoteza ajira. Mbali na hilo, pia atalipwa kwa miezi sita mfululizo, kisha malipo hayo yatasitishwa. Anayestahili malipo hayo ni yule ambaye hakuacha kazi kwa hiari yake (resignation). Inaelezwa katika mapendekezo hayo ya awali kuwa baada ya miaka mitatu tangu kusitishwa kwa fao la kujitoa, mfanyakazi atakayekuwa hajapata ajira ataruhusiwa kuhamisha michango yake kutoka ...

Magufuli aombewa madaraka yasimlevye

Image
RAIS John Magufuli amewaomba  viongozi wa dini nchini wakiwamo maaskofu baada ya kuwataka wamwombee ili kazi yake ya urais isimpe kiburi bali aendelee kuwa mtumishi mwema wa watu. Rais Magufuli alitoa ombi hilo kwa nyakati tofauti jana wakati aliposhiriki ibada ya Jumapili kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Moshi Mjini na Kanisa Kuu la Kiaskofu la Parokia ya Kristo Mfalme (la katoliki), pia la Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro. Magufuli aliomba maaskofu na viongozi wengine wa dini wamuombee wakati akiwa katika kanisa la Usharika wa Moshi, kwenye ibada iliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Askofu Dk. Fedrick Shoo na baadaye katika Kanisa la Kristo Mfalme ambako ibada iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Isaac Amani. Awali, akiwa katika kanisa la KKKT, Askofu Shoo alimuomba Rais Magufuli kujitenga na washauri wanaojikomba na badala yake apokee ushauri unaotolewa na washauri wema na wenye nia ...

Rais Magufuli Apokewa kwa Mapokezi Makubwa Mkoani Kilimanjaro Leo

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Bomang'ombe Wilaya ya Hai waliomsimamisha wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017.   Sehemu ya maelfu ya Wananchi wakimshangilia Rais Magufuli wakati akiongea nao   Mbunge Mstaafu na Mwalimu maarufu nchini Mwalimu Kham akimtyambulisha Rais Magufuli kwa mamia ya wanafunzi waliojitokeza kumlaki   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliofunga barabara kumsimamisha wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro  Wananchi Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliofunga barabara kumsimamisha Rais Magufuli wakimshangilia ...

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA TATU MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO APRIL 27, 2017.

Image
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson akiongoza kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu Mhe. Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017. Naibu Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Nyonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 27, 2017. Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Rita Kabati akiuliza swali katika kikao cha kumi na tatu cha Mkutano wa saba ...

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Atiwa Mbaroni

Image
Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, kwa tuhuma za kumshambulia mwanamke mmoja na kumsababishia maumivu makali mwilini. Msambatavangu, ambaye alikuwa miongoni mwa wanaCCM waliofukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika mwezi Machi, alikamatwa  jana mchana Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Julius Mjengi, alisema kuwa kiongozi mstaafu anatuhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita. Akifafanua, Kamanda Mjengi alibainisha kuwa kiongozi huyo alitenda kosa hilo akiwa na wenzake ambao asingeweza kuweka majina yao hadharani kwani wanaendelea kuwatafuta. “Ni kweli tunamshikilia Jesca Msambatavangu, tumemkamata leo(jana)  saa nane mchana na tunaendelea na uchunguzi dhidi yake,” alisema Mjengi na kuongeza:   “Jesca pamoja na wenzake wanatuhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa, walimshambulia na kisha kumchoma sinda...

Lowassa kumuunga mkono Uhuru Kenyatta.

Image
SIASA za Ukanda wa Afrika Mashariki zimechukua sura mpya baada ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa kutangaza rasmi kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta. Kenyatta aliyeunga ushirika pamoja na William Rutto,  anaingia katika kinyang’anyiro cha kuwania awamu ya pili ya kuiongoza Kenya huku upande wa upinzani ukiwa umepitisha jina la Raila Odinga kupeperusha bendera ya upinzani. Wakati Lowassa akitangaza kumuunga mkono Kenyatta, kwa upande wake Odinga tayari ilishajulikana wazi urafiki wake na Rais Dk. John Magufuli ambao umeanza miaka mingi tangu akiwa Waziri wa Ujenzi. Hatua hiyo ya Lowassa ambaye anatajwa kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi nchini na Afrika Mashariki imekuja baada ya kutembelewa jana nyumbani kwake Monduli na wabunge zaidi ya 20 na maofisa kutoka Kaunti ya Kajiado nchini Kenya. "Mimi naamini Uhuru Kenyatta anao uwezo mkubwa wa kuwaunganisha vema wananchi wa Kenya n...

HUYU NDIO MPENZI MPYA WA FLORA MBASHA ANAETARAJIA KUFUNGANAE NDOA

Image
Kama Basi ulisikia kuwa Flora Mbasha anaolewa tena baada ya kuachana na Emmanuel Mbasha basi inasemekana huyo hapo ndio shemeji yetu mpya wakiwa katika picha ya Pamoja,...

Kama Unaumwa Tumbo Wakati Wa Hedhi soma hapa

Image
KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya. Kutokana na simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata akina mama wengi wakati wa hedhi nimeona ni bora niandike makala hii ili iweze kuwasaidia na wengine kujua nini chanzo na mhusika afanye nini pale anapopatwa na tatizo hilo. Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo. Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu hayo huanza pale yai linapotoka katika mrija (fallopian tube) na kuteremka chini ya mrija huo wakati wa Ovulation. AINA YA MAUMIVU Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.  Ya kwanza  ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku mo...

Mali za Lugumi Mikononi mwa TRA

Image
Kampuni  ya udalali ya Yono, imefanikiwa kukamata mali za wafanyabiashara wanaodaiwa kodi ya serikali inayofikia zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya kukamata mali hizo kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam imefanywa ndani ya wiki moja. Katika operesheni hizo maofisa wa Yono wamekuwa wakishirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato(TRA), ambayo ndiyo imeipa kampuni hiyo kazi ya kukusanya kodi kwenye maeneo mbalimbali nchini. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela, Yono imepewa kazi na TRA kukusanya madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa na Zanzibar. Aliwataka watanzania kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kuleta maendeleo kwa kulipa kodi bila shuruti ili zipatikane fedha za kujenga miundombinu kama barabara, reli, shule, madaraja, hospitali na zahanati. Kuhusu taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hata baadhi ya mali za K...

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA WANANCHI KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO WA TANGANIKA NA ZANZIBAR YENYE KAULI MBIU “MIAKA 53YA MUUNGANO; TUULINDE NA KUUIMARISHA,TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII” APRIL 26,2017

Image
 Amir jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017   Amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipokea heshima na wimbo wa taifa ukipigwa  Amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akilekea kukagua gwaride liloandaliwa na vyombo vya ulizi na usalamaliloandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kusherehekea miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017 Amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride liloandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kusherehekea miaka 53 ya Muungano wa Tanga...