SERIKALI inakusudia kuajiri watumishi wapya wa umma 52,436 katika mwaka ujao wa fedha. Aidha, madaktari wapya 258 waliokuwa waende kufanya kazi nchini Kenya, lakini wakakwama kutokana na kuwekewa pingamizi la kimahakama na wenzao wao huko na hivyo Rais, Dk John Magufuli kuamuru waajiriwe mara moja nchini, watarajiwa kuanza kazi keshokutwa Jumatatu. Hayo yalisemwa bungeni juzi usiku na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alipokuwa anatoa ufafanuzi wa lini Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada nyingine, kama ilivyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM). “Azma ya serikali, kwanza kabisa hatuwezi kuajiri wananchi wote, tumekuwa tukisikia hapa wahitimu hawana ajira, wengine wanaendesha bodaboda… tunapopanga idadi ya watumishi wa kuajiriwa, tunaangalia mambo mengi, kuanzia mahitaji, vipaumbele hadi uwezo wa kibajeti. “Tayari tumeshaanza kutoa vibali vya ajira zaidi