Posts

Sakata la Lugumi bado halijachacha

Image
Dar es Salaam. Sakata la mkataba baina ya Kampuni ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, halijafa; ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeliibua ikionyesha madoa lukuki. Sakata hilo lilikuwa kama limezikwa baada ya kamati iliyoundwa na Bunge kulichunguza na baadaye kukabidhi ripoti ofisi ya Spika ambayo ilisema ingeishauri Serikali cha kufanya. Juni 30 mwaka jana, Naibu Spika Tulia Ackson alilieleza Bunge kuwa ametumia kanuni ya 117(17) kuikabidhi Serikali matokeo ya uhakiki uliofanywa na kamati ndogo iliyoundwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Alisema matokeo ya ripoti hiyo yana maoni, ushauri, mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zilizoainishwa na taarifa ya kamati ya PAC na hivyo kuzuia wabunge kujadili suala hilo. Lakini, ripoti ya CAG iliyotolewa wiki iliyopita imeibua upya sakata hilo, ambalo linahusu utekelezwaji mbovu wa mkataba wa uwekaji mashine za kielektroniki za kuchukua alama za

NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA NI MADRID NA MADRID, MONACO NA JUVENTUS

Image
Droo ya Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa imekamilika na Real Madrid atakutana na Atletico Madrid katika mechi ya kwanza ya hatua hiyo.Nusu fainali ya pili, itakuwa ni AS Monaco dhidi ya Juventus mechi ya kwanza ikipigwa nchini Ufaransa.

STAA OMMY DIMPOZ AFUNGUKA HAYA KUHUSU KUPOTEZWA KWENYE MUZIKI

Image
MWANAMUZIKI Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ametoa povu kufuatia madai kuwa, hivi sasa  kapotezwa na vijana wadogo wanaolazimisha ‘kuvaa viatu vyake’. Akipiga stori na Showbiz, Dimpoz alisema hajapotea kwenye gemu kama mashabiki wanavyomchana mitandaoni na kwamba ukimya wake wa muda unatokana na yeye kujipanga katika kuandaa kazi mpya ili iweze kufanya vizuri atakapoiachia. “Siyo kweli kuwa nimepotea, kwanza najiandaa kuachia kazi mpya ambayo ina ubora wa hali ya juu, wanaosema nimepotea wasubiri waone maajabu yangu,” alisema Dimpoz.
Image
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO, DK. HARRISON MWAKYEMBE. WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema yuko tayari kuuachia uwaziri ili aweze kulithibitishia Bunge kuwa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa alihusika katika kashfa ya Richmond. Dk. Mwakyembe alitoa kauli hiyo jana bungeni baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari na Mbunge wa Ubunge Ubungo (Chadema) Said Kubenea kumtuhumu juzi kuwa hakutenda haki mwaka 2008 wakati alipoongoza Kamati Teule ya Bunge kuchunguza kampuni tata ya ufuaji umeme ya Richmond bila kumhoji Lowassa ambaye alituhumiwa. Nassari juzi wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) alisema Dk. Mwakyembe ameikataa ripoti iliyomchunguza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds kwa madai kuwa haikumhoji mkuu huyo wa mkoa ili hali yeye aliendesha Kamati ya Teule ya Bunge ya Richimond na kum

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA UJUMBE TOKA KWA RAIS KAGAME WA RWANDA IKULU DAR ES SALAAM LEO

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017. Wengine ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi Bw. Issa Mugabutsinze.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda uliowasilishwa

Banda sasa huru kuitumikia Simba

Image
BEKI WA SIMBA, ABDI BANDA. BEKI wa Simba, Abdi Banda, yuko huru kuendelea kuitumikia timu yake katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukiongoni imefahamika. Uamuzi wa Banda kurejea uwanjani umetolewa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo imetangaza kumfungia beki huyo mechi mbili kutokana na kosa lake la kumpiga ngumi, kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla katika mechi iliyowakutanisha iliyofanyika Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Taarifa kutoka kwenye kikao hicho ambacho Banda aliitwa kuhojiwa kilieleza kuwa adhabu ya beki huyo ni kutocheza mechi mbili. Awali beki huyo wa Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) alisimamishwa kwa muda usiojulikana na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania maarufu Kamati ya Saa 72. Hatua hiyo ilimfanya beki huyo ashindwe kuitumikia timu yake katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara zilizopita ambazo Simba iliikabili Mbao FC na kupata ushindi wa mabao

Watumishi 2,000 Elimu wapandishwa vyeo

Image
WAZIRI WA ELIMU, PROFESA JOYCE NDALICHAKO. BUNGE limeelezwa kuwa Jumla ya watumishi 2,272 walipandishwa vyeo katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha 2015/16 huku miongoni mwao 71 walitoka Chuo cha Ualimu Korogwe. Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM), aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwapandisha daraja wale waliostahili na kuwa lini itawalipa madai yao ya fedha za likizo ambazo watumishi hawajalipwa kwa muda mrefu na wamekuwa wakishindwa kuzipata kwa wakati. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alibainisha serikali inaendelea kulipa madeni, ikiwamo fedha za likizo kwa walimu au watumishi katika sekta ya Elimu, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi Juni 2016, jumla ya Sh. Bilioni  22.7 zililipwa kwa walimu 63,814. Aidha, alisema katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi Machi 2017,

MCHUNGAJI MREMBO NA MWENYE MVUTO WAKUPAGAWISHA WANAUME HAFANYIWA HILI NA WANAJESHI HAWA

Image
After Nairobi Senator Mike Sonko took to social media and disclosed that he enjoyed sermons from youthful female pastor, Lucy Natasha, she became an instant hit amongst Kenyans. Many adored the youthful pastor for her immense beauty and good sense of fashion that consists of designer clothes and expensive jewellery. And it now seems that Kenyans will keep talking about this s3xy preacher whose beauty is simply irresistible. She recently rocked a red dress during her birth-day and the out-come was just amazing. Check out the photos below.

MAHAKAMA YATOA AMRI YA MSANII AGNES MASOGANGE AKAMATWE

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili. Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati kesi hiyo ilipotajwa.Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi wa kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini mshtakiwa, wadhamini wake na wakili wake hawakufika hivyo wakili Nkini akaomba mahakama itoe hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu ni mara ya pili ameshindwa kufika mahakamani hapo.Hakimu Mashauri alikubali maombi ya wakili wa Serikali na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa aheshimu mahakama kutokana na kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa. Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, alitumia daw

MAAJABU YA DUNIA..:, ANGALIA WATOTO WALA MAYAI YA CHURA NA KUZUNGUMZA LUGHA YA AJABU

Image
Watoto wamekaa na mamayao wakila chakula.nchini Uganda watoto watatu waliofungiwa na baba yao kwa miaka saba wameanza kuzungumza lugha isiyofahamika. Watoto watatu kutoka kijiji cha Barca katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani Oyam nchini Uganda wameanza kuzungumza lugha tofauti isiojulikana baada ya kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo hilo.Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote. Kulingana ma gazeti la the monitor nchini Uganda,watoto hao hawajaathirika kiakili lakini hawawezi kuzungumza na watu wengine.Wanaamini tu kile baba yao anachowaambia. Kulingana na mama yao watoto hao waliweza kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na baba yao. Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao alimzuia kutozungumza nao hatua iliowa

INASIKITISHA LAKINI INAFUNDISHA PIA, KUTANA NA MTU HUYU ALIYEZALIWA KICHWA CHAKE KIKIWA MGONGONI

Image
A man born with physical disabilities so severe his head is Upside-down has defied the odds to become an inspirational public speaker. Claudio Vieira de Oliveira, 37, was born with his neck folded back on itself, as well as badly deformed legs and almost no use of his arms and hands. Doctors told his mother to stop feeding him as a newborn as they believed he had no chance of survival. But Claudio from Monte Santo, Brazil, has overcome his extreme disadvantages to graduate as an accountant and become a public speaker.

Korea Kaskazini inaaminika kumiliki silaha 1000 zenye uwezo tofauti

Image
Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani. Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90. Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti. Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi. Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13. Ishara za kwanza kuhusu utengenezaji huo ulifanyika Septemba 2016 ambapo taifa hilo lilifanyia majaribio mashine mpya ya roketi ambayo baadhi ya watu wanasema inaweza kurusha kombora kutoka bara moja hadi jingine. Idara ya

Kanuni kumi '10' za kuwa mke mwema

Image
UHALISI WA MAISHA: Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo; UVUMILIVU: Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo. UPENDO WA DHATI: Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki

Huyu ndie mwanasayansi alietengeneza virus hatari vya ukimwi

Image
Ameua maelfu na maelfu ya watu, alitengeneza ugonjwa huu mnamo miaka ya 1970, na sasa daktari huyu kwa jina Robert Gallo ametoka adharani na kusema amepata dawa ya kutibu ugonjwa huo. Robert Gallo anaelezwa kwamba alihusika na vita vya kibaiolojia kwa lengo la kuwaondosha watu weusi na mashoga duniani katika miaka ya 1970. Ameua maelfu na maelfu ya watu, alitengeneza ugonjwa huu mnamo miaka ya 1970, na sasa daktari huyu kwa jina Robert Gallo ametoka adharani na kusema amepata dawa ya kutibu ugonjwa huo. Robert Gallo anaelezwa kwamba alihusika na vita vya kibaiolojia kwa lengo la kuwaondosha watu weusi na mashoga duniani katika miaka ya 1970.

Upendo Nkone autaka Ubunge

Image
Mwanamuziki wa injili, Upendo Nkone amesema yuko tayari kutumikia nafasi ya ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo  Rais Magufuli atamteua. Akiwa katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Upendo alisema, anaamini ametumwa na Mungu kufikisha ujumbe wake kupitia uimbaji, lakini pia yuko tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge, na kuweka wazi kuwa si kwa ubunge wa kugombea jimboni. "Sina mpango wa kuwa mwanasiasa, kwahiyo hata ubunge wa kugombea siwezi, lakini kama Rais wangu Magufuli akilala akiota kwamba anipe ubunge viti maalum, kwakweli napokea.... Mh. Magufuli nimeambiwa nigombee ubunge, basi unikumbuke baba" Amesema Upendo Amesema aliwahi kushauriwa kugombea ubunge katika jimbo fulani lakini hakuwa tayari kwa kuwa hapendi kugombea. Akieleza sababu kuu ya kutopenda ubunge wa kugombea, amesema masharti ya kugombea ni lazima uwe kwenye vyama vya siasa jambo ambalo halipendi. Jambo lingine amesema mchakato wa kupata ub

JACQUELINE NTUYABALIWE ANYAKUA TUZO ZA A-PRIME DESIGN

Image
Mrembo wa Tanzania mwenye tamaa ya kuwa na himaya ya samani za kimataifa kupitia kampuni yake, kama alivyowahi kuelezwa na jarida la Forbes hivi karibuni, Jacqueline Ntuyabaliwe ametwaa tuzo mbili za ubunifu kupitia kampuni ya Molocaho by Amorette. Ushindi wake huo unamuingiza katika kundi la watu wenye ubunifu mkubwa wa bidhaa za majumbani na katika maofisi, muda mfupi tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. Molocaho by Amorette kampuni ya kubuni na kutengeneza samani ilizinduliwa Septemba 2016. Miezi michache tu tangu kuundwa kwake inaonesha kukimbia na kufanikisha tuzo tatu za kimataifa. Katika tuzo zenye ushindani mkali na heshima kubwa kwenye ubunifu za kimataifa zijulikanzo kama A-Prime Design (A'Design) zilizofanyika mjini Roma mwishoni mwa wiki Jacqueline amepata tuzo katika kategori mbalimbali na kuwa wa pili kategori nyingine.  Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi Bidhaa zilizompatia tuzo ni samani na pia za mwanga. Ngorongoro Settee ilimpatia medali ya shaba

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA NANE CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 APRIL 18, 2017 MJINI DODOMA

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO). Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais TAMISEMI Mhe. Luaga Mpina akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Mbunge wa Nanyamba (CCM) Mhe. Abdallah Dadi Chikota akiuliza sw