MAHAKAMA YATOA AMRI YA MSANII AGNES MASOGANGE AKAMATWE
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes Gerald
maarufu kama Masogange kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya kutumia
dawa za kulevya inayomkabili.
Hati hiyo
ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati
kesi hiyo ilipotajwa.Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai mahakamani
hapo kwamba upelelezi wa kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini
mshtakiwa, wadhamini wake na wakili wake hawakufika hivyo wakili Nkini
akaomba mahakama itoe hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu ni
mara ya pili ameshindwa kufika mahakamani hapo.Hakimu Mashauri alikubali
maombi ya wakili wa Serikali na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa
ambaye ni Masogange.Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa aheshimu
mahakama kutokana na kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa.
Katika
kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya
Februari 7 na 14 mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji
la Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya heroin(Diacety
Imophine). Pia inadaiwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa za
kulevya aina ya oxazepam.
Comments
Post a Comment