Watumishi 2,000 Elimu wapandishwa vyeo


WAZIRI WA ELIMU, PROFESA JOYCE NDALICHAKO.

BUNGE limeelezwa kuwa Jumla ya watumishi 2,272 walipandishwa vyeo katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha 2015/16 huku miongoni mwao 71 walitoka Chuo cha Ualimu Korogwe.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM), aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwapandisha daraja wale waliostahili na kuwa lini itawalipa madai yao ya fedha za likizo ambazo watumishi hawajalipwa kwa muda mrefu na wamekuwa wakishindwa kuzipata kwa wakati.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alibainisha serikali inaendelea kulipa madeni, ikiwamo fedha za likizo kwa walimu au watumishi katika sekta ya Elimu, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi Juni 2016, jumla ya Sh. Bilioni  22.7 zililipwa kwa walimu 63,814.

Aidha, alisema katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi Machi 2017, Sh. Bilioni  10.5 zimelipwa kwa walimu 22,420, hivyo kufanya jumla ya walimu waliolipwa katika kipindi hicho kufikia 86,234 na kwamba katika fedha hizo, Sh. Bilioni 13.4 zililipwa kwa ajili ya madeni ya
fedha za likizo kwa watumishi 6 wa Chuo cha ualimu Korogwe.

“Uhakiki wa madeni ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale
watakaostahili,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog