JACQUELINE NTUYABALIWE ANYAKUA TUZO ZA A-PRIME DESIGN
Mrembo wa
Tanzania mwenye tamaa ya kuwa na himaya ya samani za kimataifa kupitia
kampuni yake, kama alivyowahi kuelezwa na jarida la Forbes hivi
karibuni, Jacqueline Ntuyabaliwe ametwaa tuzo mbili za ubunifu kupitia
kampuni ya Molocaho by Amorette. Ushindi wake huo unamuingiza katika
kundi la watu wenye ubunifu mkubwa wa bidhaa za majumbani na katika
maofisi, muda mfupi tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. Molocaho by
Amorette kampuni ya kubuni na kutengeneza samani ilizinduliwa Septemba
2016. Miezi michache tu tangu kuundwa kwake inaonesha kukimbia na
kufanikisha tuzo tatu za kimataifa. Katika tuzo zenye ushindani mkali na
heshima kubwa kwenye ubunifu za kimataifa zijulikanzo kama A-Prime
Design (A'Design) zilizofanyika mjini Roma mwishoni mwa wiki Jacqueline
amepata tuzo katika kategori mbalimbali na kuwa wa pili kategori
nyingine.
Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi
Bidhaa
zilizompatia tuzo ni samani na pia za mwanga. Ngorongoro Settee
ilimpatia medali ya shaba kwa upande wa samani na katika bidhaa za
mwanga Sayari Lamp pia ilimpatia tuzo ya shaba. Nafasi ya pili
ilipatikana katika kiti cha Flamingo. Taarifa zilizofikiathebeauty zinasema
kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya
mwaka 2016 na kiti cha Ngorongoro na kategori ya Lighting Products and
Lighting Projects Design Category ya mwaka 2016 ilikuwa na Sayari lamp.
Na Kiti cha Flamingo kilimpatia nafasi ya pili katika kategori ya
Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016.
Muonekano wa kiti cha Ngorongoro Settee uliompatia tuzo Jacqueline
Mengi kupitia kampuni yake ya Molocaho by Amorette.[/caption] A-Prime
Design Shindano aliloshiriki Jacqueline Mengi akiwa na kampuni yake ya
Molocaho by Amorette la A’Design hushirikisha wabunifu, wagunduzi na
makampuni yanayotengeneza bidhaa mbalimbali za ubunifu wa ndani.
Shindano la A' Design limeanzishwa kwa lengo la kuhakikisha kwamba
wabunifu wanakuja na bidhaa bora kabisa zenye ushindani mkali katika
soko la kimataifa. Kwa kawaida tuzo zake hutolewa katika kusanyiko kubwa
la wabunifu linalofanyika Roma, Italia kwa kuratibiwa na OMC Design
Studios SRL . Jacqueline, Miss Tanzania (2000) hivi karibuni alishiriki
tuzo za rais za CTI na ana mafunzo ya Interior Design kutoka Rhodec
International. Kampuni ya Molocaho by Amorette, kampuni ya Tanzania
inajishughulisha na utengenezaji wa samani bora kwa namna mteja
anavyohitaji, nyuzi, taa, urembaji, samani za nje na kwenye bustani.
Sayari Lamp iliyompatia tuzo katika kategori ya Lighting Products and
Lighting Projects Design Category ya mwaka 2016.[/caption] Molocaho
inatengeneza samani zenye mahadhi ya kiafrika ikichanganya utamaduni wa
Tanzania katika mazingira ya kisasa na kumalizia na ubunifu wa
kimataifa. Molocaho, moja ya makampuni ya Afrika Mashariki ya samani
yanayokua kwa kasi, imejipatia nafasi kubwa ya heshima kwa kuhakikisha
kwamba inatumia mali ghafi na mbao njema pekee za Tanzania kutengeneza
samani zenye kwenda kimataifa. Katika mahojiano na jarida maarufu la
Forbes alishawahi kusema kwamba anawania soko la kimataifa kutokana na
ukweli kuwa bidhaa anazotengeneza zimejipambanua kwa wateja.
Muonekano wa kiti cha Flamingo kilimpatia nafasi ya pili katika
kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya
mwaka 2016.[/caption] Jacqueline Ntuyabaliwe, pamoja na kuwa na ratiba
yenye changamoto sana (Yeye ni balozi wa WildAid na yumo ndani ya bodi
kadhaa; mama wa watoto pacha wavulana; mke kwa mfanyabiashara mwenye
mafanikio makubwa na akiendesha taasisi ya hisani ya elimu), huhakikisha
anakagua kila samani inayozalishwa kiwandani kwake kabla ya kuuzwa au
kusafirishwa. Mume wake, Reginald Mengi, ni tajiri mwenye mafanikio
makubwa nchini Tanzania ambaye ameujenga utajiri wake kwa kufanya karibu
kila kitu kuanzia uzalishaji wa kinywaji cha Coca-Cola hadi uchimbaji
wa madini na kumiliki vituo vya televisheni na magazeti. Kwa tuzo hizo
Amorette, inajidhihirisha kuwa chata yenye mafanikio makubwa nchini
Tanzania na huku ikipanda kwa kasi kimataifa.
Comments
Post a Comment